Anasema ananipenda ila hataki kuolewa kwa sasa

SuperHb

JF-Expert Member
Mar 21, 2016
895
696
Habari ndugu zangu,

Kuna binti nimekuwa nae kwenye mahusiano takribani miezi kama mitatu hivi...muda wote wa mahusiano yetu alikuwa anakuja Nyumbani kwangu...anaweza akalala kwa siku mbili,,siku nyingine anashinda kwangu na kuondoka,,,alikuwa ananifanyia kila kitu kama mke aliolewa...

UTATA UNAPOANZIA
Kilichofanya niwaletee uzi huu...kuna mambo niliyawaza sana....nikawa najiuliza kwanini awe anakuja na kuondoka??,,na kwanini awe ana anakuja analala siku inayofata anaondoka...?,,,,kwa upendo wangu kwake sikutaka nimchezee;nikaamua nimueleza swala la kumuoa awe mke...akawa kama anaruka hivi,,,kama analeta vikwazo japo sio vya moja kwa moja,,mara anasema kwanza nimtamfutie shughuli yoyote ya kufanya ndo nitamuoa...mimi nilimuambia nimuoe kwanza maswala ya ya kazi au shughuli ya kufanya nitaishughulikia nikiwa nae,,maana hata mimi sipendi niende kazini mke nimuache ndani bure tu.Nikaona kama analeta kama mgomo fulani...

MSIMAMO NILIYOUWEKA KWAKE
Siku zilizidi kwenda,,akawa anakuja home kwangu na kuondoka kama kawaida yake...siku hiyo alipokuja niliamua kumpa msimamo wangu,nilimuambia Kama yu tiyari kuolewa akae hapa hakuna kuondoka....kama anaona hawezi kuolewa anaweza kuondoka...huyu alichonijibu ni kwamba Nanukuu "Ukiona nimeondoka hutaona narudi kwako tena" mimi sikujibu chochote yeye akafungua mlango akaondoka,,,baada ya muda kama nusu saa alinitumia sms ikisema "Nisamee niliyokwambia nilikuwa nakutania" sikujibu meseji yake baadae kama dakika 10,,,akanipigia nakuniambia kwamba alikuwa ananitania,,,Ngoja afikirie atanipa jibu,,,mimi nilichomwambia nakupa siku tatu zikizidi hizo Mapenzi mimi na wewe basi,akasema sawa.

Sasa hivi siku tatu nilizompa zimeshapita...tunaelekea wiki yuko kimya...hata sijampia kumuulizia kulikoni...yuko kimya mpka saaa..
Sasa ndugu naomba Maoni yenu...vyovyote itakavyokuwa nitayapokea....NASHUKURU
 
Kwann unafosi ndoa mkuu kwa mda mchache mliokuwa kwenye mahusiano
Alf acha yeye ndo apambanie hiyo ndoa na sio wew mkuu unayumba
 
Nimeishia hapa," Kuna binti nimekuwa nae kwenye mahusiano miezi 3"
Yani unataka akukubalie ndoa huyo binti mwerevu sana, wewe ndo unamatatizo hebu tuachie huyo binti it seems you are so desperate for marriage. Huu Uzi ulioanzisha kafumie nguo
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom