Mbishi 4 real
JF-Expert Member
- Jan 16, 2014
- 640
- 657
Habari zenu wana MMU,
Kuna binti moja nimesoma nae chuo kimoja na darasa moja na wote tumemaliza mwaka mmoja.Huyu binti alikua akinihusudu sana kiasi cha kunitumia sms za mitego mara kwa mara mpaka mida mibaya kipindi bado tupo chuoni.
Baada ya kusoma alama za nyakati nami nikamtongoza na akawa na dalili zote za kunikubalia ingawa bado alikua ananizungushazungusha dizaini kama kunipa kama namaanisha au la.
Baada ya muda flani kupita me nikapata girlfriend mwingine ambaye hakua mwanazuoni wa chuo nilichosoma mimi.
Kwasasa nimezaa na huyo binti ambaye hatukusoma chuo kimoja mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitatu ila chakushangaza yule binti niliyesoma nae darasa moja amekua akinidadisi sana kuhusu huyu mpenzi wangu mpya kwa maswali kama "harusi lini ?","mnakaa pamoja ?"...sasa kwa maswali yake nashindwa hata nimueleweje...naombeni msaada wa mawazo.