Kinachomsumbua huyo ndugu yako ni mapepo/majini ambayo humjia ndotoni na kufanya nae mapenzi.
Hawa kwa majina mengine unaweza kuwaita "Wake au waume wa kiroho". Kimsingi haya ni mashetani/majini/mapepo ambayo yanaweza kumuingilia mtu akiwa amelala. Nimesema wake au waume wa kiroho ili kukuelewesha kuwa;majini haya huwa yanakuwa yamefunga ndoa na mtu na hivyo kuwa na uhalali wa kumwingilia kimwili huyo mtu ndotoni.Ndoa hiyo inaweza kuwa ilifungwa baharini,angani na pengine nchi kavu( Muulize kama alishawahi kuota amefunga ndoa na mtu). Jini akiwa amefunga ndoa na mtu pasipo muhusika kujua anakuwa anatekeleza majukumu ya tendo la ndoa na mtu ambaye amefunga naye ndoa hiyo,
Kawaida mtu ambaye anasumbuliwa na majini/mapepo haya huota ndoto kuwa anaingiliwa kimwili na mtu huku amelala, majini haya yanaweza kuvaa umbo lolote lile pindi yanapokuja kumwingilia mtu. Mtu anaweza kuota anaingiliwa na Kaka/dada yake,baba/mama yake,ndugu yake yeyote,au mtu wa aina yoyote ama anamfahamu au hamfahamu. Wakati mwingine majini/mapepo haya huvaa sura za wanyama(ng'ombe,mbuzi,kondoo,mbwa) au mnyama mwingine wa aina yoyote. Lengo hapo la kujibadilisha maumbo ni ili 'muingiliwa' asijue kuwa aliingiliwa na jini au pepo bali aichukulie kama ndoto tu ya kawaida,lakini kimsingi ni hao hao majini.
Wakati mwingine muingiliwa si lazima awe amelala tu usiku,anaweza akaingiliwa hata mchana,yani tuseme anaweza kuwa amepumzika mahala fulani halafu akasinzia kidogo na katika kausingizi hakohako kadogo ka mchana jini huyo anaweza kumjia na kufanya nae mapenzi.
KWA NINI HII HUTOKEA?
Kitendo cha jini kumuingilia mtu akiwa amelala huwa kinatokea kutokana na 'hati miliki' ambayo jini huyo anakuwa nayo dhidi ya mtu husika. Kama nilivyosema hapo juu ya kwamba,jini huyo huwa anakuwa amefunga ndoa na muhusika kwa hiyo anakuwa ana haki ya kumuingilia mtu huyo kimwili.
'Mke au mume huyo wa kiroho' ambao kimsingi ni majini au mapepo anaweza kumwingilia mtu wa aina yoyote,yaani wa kiume au wa kike. Kama ni mwanaume anaweza kuota anafanya mapenzi na mwanamke lakini pia wakati mwingine anaweza kuota anaingiliwa kinyume na maumbile na mwanaume mwenzake ambaye ni jini aliyemjia katika sura fulani.
(Yapo mambo mengi ya kueleza hapa ambayo siwezi kuyaweka yote hapa sababu ya muda na kuandika, lakini ikumbukwe tu kuwa tatizo hili linawapata watu wengi sana,yani kuna watu wengi ambao wameoa na kuolewa rohoni ingawa wao hawajui,wanajiridhisha kwa kuziita 'ndoto nyevu', hii haipo hivyo.
SULUHISHO:
Kinachoweza kuondoa tatizo hili ni MAOMBI pekee.
Kuna maombi fulani maalum ambayo muhusika anaweza kufanyiwa ili kuwandoa majini/mapepo hao. Lakini pia muhusika atapaswa kufundishwa jinsi ya kuomba maombi hayo ili wakati mwingine ajitenge mwenyewe na majini hao. Hii inawezekanakabisa na tatizo kuisha kabisa.
Kwa msaada zaidi NiPM nikupe mwongozo maana siwezi kuweka kila kitu hapa .
Hakuna linaloshindikana kwa yeye aaminiye.