Anaomba msaada wa ushauri wa kisheria

tanga kwetu

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2010
Messages
2,193
Points
2,000

tanga kwetu

JF-Expert Member
Joined May 12, 2010
2,193 2,000
Naomba wajuzi wa sheria mumsaidie ushauri wa nini afanye huyu dada kwa kisa cha kweli kilichompata kazini kwake.

yeye anafanya nyumbani kwa afisa ubalozi (mzungu) wa moja ya balozi za nchi za Scandinavia jijini Dar. Kazi yake ni mpishi na jiko lipo karibu sana na ofisi binafsi ya huyo afisa balozi. Ikitokea akifanya usafi wa nje wa jiko pia hufuta na dirisha la ofisi ya huyo afisa. Hapo nyumbani kuna wafanyakazi wengine kama vile dereva wa familia na walinzi wawili (dereva na mlinzi mmoja ambao wanaishi humo humo na familia zao). Huyu dada amefanya kazi ya upishi na afisa huyu kwa miaka mi5 sasa ila kazi hiyo kwenye nyumba hiyo hiyo (maana huwa wanabadilishwa hao maafisa ubalozi) kwa miaka 15 sasa. Jumla ya maafisa aliowahi kufanya nao kazi ni watatu na wote waliopita walikuwa wanam-reccomend yeye kwa ufanisi na tabia zake nzuri.

Mwanzoni mwa mwaka huu (February) kuna kiasi cha 1.9 Milioni TShs. kilipotea ofisini kwa afisa huyo katika mazingira ya kutatanisha na haikujulikana aliyechukua. Maafisa wa Polisi walifika nyumbani hapo na kuwahoji wafanyakazi wote. Hawakuwahi kupelekwa kituoni wala hawakuwahi kuchukuliwa maelezo.

Jana, wakati huyo mdada anafanya usafi aliona kuna chenjichenji mezani kwenye ofisi ya huyo balozi. Anakisia ni kati ya 20,000 na 30,000TShs. Kwa shida aliyobanwa nayo maana katoka kwenye msiba wa mwanae wiki iliyopita akashawishika na kudokoa 2,000 TShs. Laa haula, kumbe tangu upotevu ule utokee yile afisa alikuwa ametegeshea camera ya siri (CCTV). Kwa ushahidi huo, yule afisa alileta maafisa Polisi watatu (wanaume wawili na mwanamle mmoja) kumhoji huyu mdada. Mahojiano hayo yalijaa vitisho na alipigwa sana hata kupelekea kujikojolea na kuanza ku-bleed kabla ya siku zake. Hata hao maafisa wa Polisi waliona hivi vitu. Walimshinikiza akiri kwamba aliiba ile pesa ya awali lakini yeye alikataa katakata. Hatimaye, amepewa wiki 1 arejeshe otherwise anafungwa jela.

Wafanyakazi wengine wanaamini, mmoja wa walinzi (ambaye haishi pale) ndiye aliyeiba zile pesa. wanasema wiki ileile iliyopotea pesa, alifanya shopping kubwa ya fenicha ambayo wanaamini ilitokana na zile pesa.

Kwa vile yeye anaamini hajachukua zile pesa na pia hana uwezo wa kulipa hizo pesa anasema hayuko tayari kulipa hizo pesa na yuko tayari kwa kesi. Aliniomba ushauri nami nimeamua ku-share nanyi. Naomba ushauri wenu.

I submit
 

Forum statistics

Threads 1,390,006
Members 528,077
Posts 34,040,783
Top