Kwa muda mliokuwa mbali inawezekana kabisa akawa na mfumo mwingine wa maisha (kakua) hivyo itakua ngumu kukuamini kwa haraka kuwa unampenda na unamhitaji hii ni kutokana na matapeli wa mapenzi. Kama ndiyo: Nenda nae taratibu ili akuamini na kukuingize katika moyo wake mwishowe utafurahi.
Pia inawezekana ana mpenzi mwingine anayempenda japo akawa haeleweki hivyo akakuweka wewe kana backup, ikitokea alipo pakashindikana basi arudishe majeshi kwako kwa akili. Hapa unatakiwa kuwa makini maana ni wachache sana wanaokiri kuwa na wenza wakati wenza hao hawaeleweki. Hivyo kuwa makini katika kumsoma kisha fanya maamuza sahihi badala ya kuumia moyoni kwani mapenzi hayakuanza leo.
Sikatai ila Mbona alikubali kuwa na mimi