Ananiomba nijifanye mimi ndiye niliyempa ujauzito

lyenyi

JF-Expert Member
Mar 4, 2020
2,532
7,000
Wakuu habari!

Katika hali isiyo ya KAWAIDA Kuna dada ambaye tunafahamiana lakini sio wapenzi kabisa, na hatujawahi kuwa wapenzi.

Huyu dada juzi amenifuata na KUJIELEZA kuwa alikuwa na mahusiano na mtu lakini hakujua kuwa ni Mme wa mtu hadi hivi karibuni ndio amejua.

Hivyo anaomba Mimi nimfichie aibu kwa wazazi wake, maana alishapanga kwenda kumtambulisha huyo jamaa wiki ijayo, na pia ana ujauzito wa miezi mitano.

Hivyo anaomba Mimi ndio NIJIFANYE mhusika Kwa gharama zake, posa mahali eti atatoa mwenyewe Mimi niwape wazazi wake halafu baada ya muda NIJIFANYE nimemuacha.

Binafsi hilo jambo nimekataa ila nimemwambia kuwa nafikiria ila kiukweli kutoka moyoni siwezi kulikubali.

Ndugu zangu humu tupo wengi je Kuna mwingine yaliwahi kumkuta haya?

Uliyamalizaje?
HIVI KWELI MIMI NIWE MCHUMBA WA MCHONGO!!?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom