Anamuomba mume wangu jioni na usiku tu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anamuomba mume wangu jioni na usiku tu!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jul 17, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,433
  Likes Received: 5,688
  Trophy Points: 280
  [h=3]Anamuomba mume wangu jioni na usiku tu![/h]

  [​IMG] SWALI
  Hapa kwa jirani yangu kuna mwanamke mrembo sana ambaye ameachwa na mume wake na kubaki mwenyewe kwenye hiyo nyumba.
  Kitu cha ajabu ni kwamba kila mara kukiwa na tatizo la kuhitaji msaada wa kutengenezwa kitu nyumbani kwake (kama kuweka bulbu nk ) basi huja kumuomba mume wangu akasaidie.
  Nimeanza kuwa na wasiwasi na mume wangu kuwa na uhusiano usio wa kawaida na huyo mwanamke kwani kila akiitwa anaenda bila kuniuliza au kukataa hata kama alikuwa anafanya kitu cha msingi hapa nyumbani, mbaya zaidi huyu dada figure yake si utani ameumbika na kikubwa zaidi matatizo yake ya kutengenezewa vitu hutokea jioni na usiku tu na si mchana.

  Najisikia wivu sana.
  Je, nifanyeje ili kuondokana na hii hali na ikiwezekana mume wangu kuachana kabisa na kutoa msaada wa aina hii kwa mwanamke huyu?

  MAJIBU
  Kiukweli hata ningekuwa mimi kwa kweli ningejisikia wivu kama unavyojisikia wewe na una haki ya kujisikia wivu kwani inaonesha huyo mwanamke jirani yako anatumia advantage ya wema na huruma za mume wako kutimiza mahitaji yake na pia namna anafanya inaleta maswali ambayo mwanamke yeyote ambaye anampenda mume wake na kumlinda lazima ajisikie wivu.

  Huyo mwanamke ameshafahamu kwamba mume wako ni mtu rahisi na mtu wa watu na kwamba anakuwa tayari kusaidia muda wowote (Pleaser) na kutokana na huo wema wake huyo mwanamke anaamini (anafahamu anachokifanya) kiasi cha kumvuta na mwishowe kutimiza malengo yake.
  Ingawa hatuna ushahidi kwamba kitendo cha mume wako kuwa mkarimu kwa huyo dada kina maanisha uhusiano usio wa kawaida, bado unatakiwa kuwa makini kulinda kilicho chako kabla ya mambo kuharibika, nimefurahi kwa uwezo wako wa kugundua kwamba huo uhusiano unaweza kuleta shida kwani ni vizuri kuwa mtu wa kabla ya tukio kuliko kuwa mtu wa baada ya tukio.

  Jambo la msingi ni wewe kuwa na mpango kamili (kumpa darasa mume wako kwa upendo na heshimu) ambao utasaidia mume wako kujisikia vile wewe unajisikia kwani huyo mwanamke inaonekana amewasha moto na dawa ya moto wakati mwingine ni moto, hivyo na wewe mwambie mumeo wazi na bayana vile unajisikia kwa kumpa mfano kama ifuatavyo.

  Muulize yeye mumeo atajisikiaje ikitokea kuna mwanaume hapo mtaani ambaye ameachana na mke wake na akawa anakuja hapo kwenu kukuomba wewe mwanamke kwenda kumsaidia kuonja chakula alichopika kama kimeiva au ukamsaidie kumwelekeza kama sabuni anayotumia kufua nguo inaweza kutakatisha nguo au la huko nyumbani kwake saa za jioni na usiku.

  Mpe hiyo picha na muulize atajisikiaje.
  Ndipo umwambie ndivyo wewe unajisikia kwa kile anaanya na yule mwanamke jirai yenu, hii ndiyo njia pekee ya kumsaidia mume wako asiwe handyman hadi chumbani kwa huyo mwanamke.

  Vinginevyo, tafuta simu ya fundi (handyman) yeyote unayemjua au tafuta fundi na nenda naye moja kwa moja kwa huyo mwanamke na ukifika mwambie “Nimeona hapa nyumbani kwako unahitaji fundi mara kwa mara na nimeamua kukutafutia fundi wa kudumu ambaye muda wowote, siku yoyote ukitaka msaada atakusaidia na unaweza kupanga naye ni namna gani awe anakuja kukusaidia kwani mimi na mume wangu tunahitaji muda pamoja kushughulia masuala ya familia”
  Mwache fundi hapo na wewe nenda nyumbani na mwambie mumeo tukio zima.

  Kama huyo mwanamke ana mishipa ya fahamu basi atafahamu umempa ujumbe gani.
  Lazima umuoneshe mume wako na huyo mwanamke kwamba na wewe una backbone.

  Be strong!

   
 2. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  mambo ya kizungu! Waswahili tutayaweza wapi?
  Even my anko alikua anaitwa na Mama esta akamfungie mapazia ilihali mumewe yupo.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,433
  Likes Received: 5,688
  Trophy Points: 280
  Yaaaaaaaaaaaaallllllllllaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaahhhh
   
 4. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #4
  Jul 17, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,232
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Ilishawahi kuletwa hapa hii thread tukaijadili!
   
 5. wende

  wende JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2011
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 715
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  apo kazi ipo,but watch out Pdidy mmeo ndo kashatekwa apo! wivu ni mhimu sana kwenye mali zako!
   
 6. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  mkuu pdidy tunashindwa kuchangia, hebu zipe interval threads zako kaka, zipo poa bt utatufanya tusichangia vizuri kama ilivyopaswa!
   
 7. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mume anauma haswa anapofanya mambo akajitia mpofu kama vile hakuoni kama unakereka.
   
Loading...