Anakatazwa kutoka ndani!!

Huyo jamaa pumbavu sana,ushauri wa mwisho ninampa ni huu. Ahamie hotel 1 week azime simu, aombe likizo ofisini yeye awe wa kula kulala hotelini tu. baada ya hiyo wiki moja arudi nyumbani. Kama huyo mwanamke hajaacha hiyo tabia basi amrudishe kwa wazazi wake akafundwe upya, biashara huria akileta gozi gozi kuna watu wako tayari kuolewa bila misimamo ya kijinga kama yake.
 
Kuna kipindi jamaa huwa anafungiwa mlango analala sebuleni akichelewa....hii niliipata kwa hausigeli baada ya kumdadisi wanavyoishi.
Dah asee katavi endelea kudadisi huyo house geli, inawezekana kuna makubwa zaidi ya hayo anayofanyiwa na huyo mwanamke.
 
huyo jamaa vipi ... alishapewa go ahead na wazazi wake sasa anataka ushauri gani zaidi?? ... hapo anajitia pressure tu ... mfupa alioushindwa fisi binadamu utauweza?? mwambie awe mwanaume na sio wa kiume!!
Jamaa tukimwambia achukue maamuzi magumu anajitetea kuwa mtoto atapata taabu. Wamejaaliwa kupata mtoto mmoja.
 
Dah asee katavi endelea kudadisi huyo house geli, inawezekana kuna makubwa zaidi ya hayo anayofanyiwa na huyo mwanamke.
Kuna siku aliibuka ofisini kwa jamaa, akamkosa ofisini kwake kumbe alikuwa nje anaongea na sekretari mambo ya kiofisi. Ilikuwa ni ugomvi, jamaa kajitahidi kumueleza kuwa yule ni mfanyakazi mwenzake lakini mama hataki kuelewa. Nikaitwa kwenda kusuluhisha, ndio siku niliyopigwa marufuku kukanyaga pale eti mimi ndio namtafutia jamaa wanawake na nimemfundisha kiburi!
 
hapo tatizo naona ni huyo mama kutokuwa na la kufanya
kukaa nyumbani muda mwingi kunaboa mtu unaweza ukawa depressed
ukiachilia ana house gal ndo kabisaa ina mana ya kwamba kazi nyingi anafanya haus gal..sasa yeye afanye nini?ndo hapo linakuja swala la kumchokonoa mumewe ye akidhani anajenga kumbe anabomoa.na atakuja kujuta huyo mama kwa nayoyafanya kama hatoacha.

kuna jirani yangu alimfanyia mumewe hivyohivyo alianza hataki marafiki mara hataki atoke nje mara akamroga kabisa mume akaacha kazi akawa kama zembe tu home..mume akaja kufariki ndo tukajua ukweli yule mama akawa analia kwa kuongea maushenzi aliyomfanyia mumewe mpaka akawa zoba..

Katavi mshauri rafiki yako sidhani kama anataka kuend up like that.achukue hatua angali mapema..hapo alipo tu keshakuwa zoba sasa akiendelea na kazi ataacha..duuh huruma.pole zake
 
Huyo mke wa jamaa ana matatizo sana maana hata majirani haivi nao vizuri.
 
Afrodenzi umesema
ikizingatia ni mama wa house atakula jeuri yake

Uhuru kwenye ndoa ni haki ya kila mtu
is so sad when people take advantage of that
sasa hapo ile trust ndo inapotea jumla..

And trust is like a virginity u can only
break it once
 
hapo tatizo naona ni huyo mama kutokuwa na la kufanya
kukaa nyumbani muda mwingi kunaboa mtu unaweza ukawa depressed
ukiachilia ana house gal ndo kabisaa ina mana ya kwamba kazi nyingi anafanya haus gal..sasa yeye afanye nini?ndo hapo linakuja swala la kumchokonoa mumewe ye akidhani anajenga kumbe anabomoa.na atakuja kujuta huyo mama kwa nayoyafanya kama hatoacha.

kuna jirani yangu alimfanyia mumewe hivyohivyo alianza hataki marafiki mara hataki atoke nje mara akamroga kabisa mume akaacha kazi akawa kama zembe tu home..mume akaja kufariki ndo tukajua ukweli yule mama akawa analia kwa kuongea maushenzi aliyomfanyia mumewe mpaka akawa zoba..

Katavi mshauri rafiki yako sidhani kama anataka kuend up like that.achukue hatua angali mapema..hapo alipo tu keshakuwa zoba sasa akiendelea na kazi ataacha..duuh huruma.pole zake
Huu ndio ushauri tuliompa mwanzo kuwa amtafutie shughuli ya kufanya, lakini kama walivyosema wazazi wa binti siku ya harusi yule mwanamke hataki kufanya kazi ni mvivu sana.
 
asikurupuke kumhukumu mke, yawezekana huyo mama ana shida ya kisaikolojia inayoenda miaka mingi nyuma na bado inaendelea kumsumbua. nadhani ajaribu kutafuta watalaam wa ushauri wakae naye na kujua ni kwenye point ipi mambo yalienda kinyume huyu mama, asipofanya hivi na kudhani ni maigizo basi siku moja atamshudia huyu mama akiwa na sifa zote za kupelekwa Mirembe Hosp.
 
Huu ndio ushauri tuliompa mwanzo kuwa amtafutie shughuli ya kufanya, lakini kama walivyosema wazazi wa binti siku ya harusi yule mwanamke hataki kufanya kazi ni mvivu sana.

Mwanamke mvivu, jeuri, hapatani na majirani, mgomvi, ukiwa mvivu lazima uwe mchafu sasa huyo mwanamke wa kazi gani
ushauri wa mwisho apewe talaka akajifunzi upya
 
Duuuh

Hivi huyu mshikaji hajawahi kuwa mkorofi hata utotoni???
Nahisi hata ikitokea mkewe anatongozwa na njemba nyingine jamaa ata-mute tu kwa sababu ya upole wake. Na hata akiongea atatulizwa na waif wakee tu. Udhaifu mkubwa huu kwa mwanaume

Mkuu Katavi
Mwambie jamaa kwamba kuwa mpole too much ni udhaifu mkubwa sana ktk maisha
Kiongozi yeyote hata wa makazini wanalazimika kuwa wakali ili kazi zifanyike, na nidhamu ichukue mkondo wake
Ni sawa kwenda kusema kwa wakubwa lakin kama yeye hawezi kujitambua kama kiongozi wa nyumba na familia basi ataendelea kupelekeshwa aisha yake yote.
Mwambie pia hakuna mapenzi ya namna hiyo bali anaburuzwa.
Abadilike na aanze kuwa Baba wa kweli, kuwa na familia sio lelemama.
Jamaa anachoogopa ni pale akiwa mkorofi huenda wataachana na mtoto eti atapata shida.
 
Huyo mwanamke ana inferiority kama anaweza amtafutie hata cha kusoma awe busy, na kama ni mjeuri wa asili basi mume amtolee uvivu amuonyeshe yeye sio zoba. Na kwa kuwa bazazi banajua tabia ya binti yao basi awaeleze. Pole yake sana.
 
Back
Top Bottom