Anakatazwa kutoka ndani!!

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,983
12,702
Heshima wakuu...

Kuna jamaa yangu ambaye tumekuwa pamoja nikiwa na maana michezo ya utotoni na shule ya msingi pia tumesoma darasa moja kule kijijini kwetu. Amekuwa kama ndugu maana ndiye alinipokea hapa mjini kabla sijaanza kujitegemea.

Matatizo yalianza alipooa, baada ya miezi kama sita hivi nilipigwa marufuku na mkewe nisiwe na mazoea na huyu jamaa eti namtafutia wanawake, pindi tunapotoka pamoja hasa siku za wikendi. Kuepusha mgogoro nikaacha kwenda nyumbani kwa jamaa na kama kuna shida ya muhimu namuibukia ofisini kwake. Si mimi tu, bali marafiki wote wa karibu wa jamaa walipigwa mkwara kama mimi.

Ishu ni juzi huyu jamaa kaja kuniomba ushauri amfanye nini mkewe maana kero zimezidi, akichelewa kurudi kazini ni zogo, na akirudi haruhusiwi kutoka labda atoe sababu za msingi kwa nini anatoka na ikiwezekana wanatoka wote. Kifupi jamaa hana sauti mbele ya mkewe.

Nilimshauri jamaa hii ishu aifikishe kwa wazee akianza na mshenga, kabla ya kuchukua uamuzi. Mke wa jamaa ni mama wa nyumbani.

Nimeileta hapa ili tupate uzoefu kutoka kwa wataalamu wa mahusiano na mapenzi huenda tukapata uzoefu kwa waliowahi kupata mkasa kama huu.

Nawasilisha...
 
Huyo Mama anamatatizo anafikiri kwa umri huo huyo jamaa anashindwa kutongoza mpaka akusubiri wewe uje umtongozee akili finyu sana hii.

Huyo rafiki yako nae huyo mwanamke toka wako wachumba alikuwa halioni hilo la kuwa controled na mwanamke akalizuia mapema??

Namuonea huruma huyo mwanaume maana navyojua mimi mwanamke akipata nafasi mwanaume atajuta ni mara 1000000000000 ya mwanaume kuwa hivyo.

Msaidie mwenzio mpe mwongozo kabisa hata umsindikize kwa mshenga maana inaweza kuwa hata huko anakatazwa kwenda.
 
Yaani huyu jamaa hadi namuonea huruma, maana sio muongeaji. Huyo mwanamke inaonekana alificha makucha yake wakati wa uchumba, lakini cha kushangaza siku ya harusi wazazi wa mwanamke walimtahadharisha jamaa na wakamwambia kuwa mkewe ni jeuri hivyo asisite kumshikisha adabu pale atakapokuwa mkorofi, tulidhani ni utani bwana, baada ya miezi sita yale yaliyosemwa yakaanza kujionyesha..
 
Msaidie mwenzio mpe mwongozo kabisa hata umsindikize kwa mshenga maana inaweza kuwa hata huko anakatazwa kwenda.
Hili liko wazi kabisa anakatazwa kutoka, nilipomwambia ushauri huo akaanza kuwa na wasiwasi eti ataendaje??
 
ila kwawanaume wa sasa naona hiyo inafaa zaidi!!

ila we mwanamke naongea na ww, heshimu marafiki za mumeo bila marafiki unafikiri kesho na kesho kutwa mnapata taabu itakuaje???

naongea na ww mwanamke, "niwako akiwa kwako akiwa nje si wako" utakufa bure na pressure lol!!!

au lbd mwenzetu umepata mume mwenye mtarimbo wa dhahabu??? Ama kweli kungwi wako aliyekufunda kala hasara!!!!
 
dah! Kazi kwei kwei ina maana hata yeye kuwa mke wa huyo jamaa yako kwani wewe ndiye uliyemtafutia? Huyo uwezo wake wa kufikiri ni mdogo mno.
 
Dah
Yaelekea huyo mwanamke
She is insecure kuhusu kitu fulani..
lakini nacho shauri huyo rafiki yako
anatakiwa amwonyeshe mkewe nani ni baba wanyumba
asiwe lelemama sana

Akaechini na mkewe na kumueleza anachofanya si vema..
ajaribu kumwambia mkewe je ni vipi kama yeye
Akikatazwa kwenda salon au kuonana na marafiki zake?

Amwambi e mkewe ndoa si jela wanatakiwa wafurahie maisha
ya wao kuwa wawili ..
na ndoa bila ndugu, jamaa na marafi ni ndoa ya upweke..
 
Hapo kweli hakufundwa na kungwi!
 
dah! Kazi kwei kwei ina maana hata yeye kuwa mke wa huyo jamaa yako kwani wewe ndiye uliyemtafutia? Huyo uwezo wake wa kufikiri ni mdogo mno.
Nadhani hajiamini labda kwa kuwa ni mama wa nyumbani!
 
Dah
Yaelekea huyo mwanamke
She is insecure kuhusu kitu fulani..
lakini nacho shauri huyo rafiki yako
anatakiwa amwonyeshe mkewe nani ni baba wanyumba
asiwe lelemama sana

Akaechini na mkewe na kumueleza anachofanya si vema..
ajaribu kumwambia mkewe je ni vipi kama yeye
Akikatazwa kwenda salon au kuonana na marafiki zake?

Amwambi e mkewe ndoa si jela wanatakiwa wafurahie maisha
ya wao kuwa wawili ..
na ndoa bila ndugu, jamaa na marafi ni ndoa ya upweke..
Hayo yote unayoshauri dada Afro yalishafanyika, ila mke kawa kichwa ngumu!
 
Yaani huyu jamaa hadi namuonea huruma, maana sio muongeaji. Huyo mwanamke inaonekana alificha makucha yake wakati wa uchumba, lakini cha kushangaza siku ya harusi wazazi wa mwanamke walimtahadharisha jamaa na wakamwambia kuwa mkewe ni jeuri hivyo asisite kumshikisha adabu pale atakapokuwa mkorofi, tulidhani ni utani bwana, baada ya miezi sita yale yaliyosemwa yakaanza kujionyesha..
Dah!! Kwahiyo huyu mwanamke ana tabia ya ujeuri kiasi kwamba hadi wazazi wanaimfahamu vizuri na walimtahadharisha jamaa
 
duuh mambo ya kufungiwa ndani haifai aisee,yani castle lite za nyumbani hazipandagi kabisa

hapo jamaa akomae nae mpaka mwisho mama akimwaga ugali nae amwage mchuzi tu maisha ya kulindana na kufungiana ndani mi ningepata depression bana:ballchain:
 
Dah!! Kwahiyo huyu mwanamke ana tabia ya ujeuri kiasi kwamba hadi wazazi wanaimfahamu vizuri na walimtahadharisha jamaa
Sisi wenyewe tulishangaa, tulidhani labda waliongea vile kwa sababu ya kilevi, si unaelewa mambo ya sherehe!! Halafu mbaya zaidi kauli hiyo ilisemwa na wazazi wote wawili, hasa mama wa binti ndie alitia msisitizo!
 
Kuna kipindi jamaa huwa anafungiwa mlango analala sebuleni akichelewa....hii niliipata kwa hausigeli baada ya kumdadisi wanavyoishi.
 
siku ya harusi wazazi wa mwanamke walimtahadharisha jamaa na wakamwambia kuwa mkewe ni jeuri hivyo asisite kumshikisha adabu pale atakapokuwa mkorofi ...

huyo jamaa vipi ... alishapewa go ahead na wazazi wake sasa anataka ushauri gani zaidi?? ... hapo anajitia pressure tu ... mfupa alioushindwa fisi binadamu utauweza?? mwambie awe mwanaume na sio wa kiume!!
 
Duuuh

Hivi huyu mshikaji hajawahi kuwa mkorofi hata utotoni???
Nahisi hata ikitokea mkewe anatongozwa na njemba nyingine jamaa ata-mute tu kwa sababu ya upole wake. Na hata akiongea atatulizwa na waif wakee tu. Udhaifu mkubwa huu kwa mwanaume

Mkuu Katavi
Mwambie jamaa kwamba kuwa mpole too much ni udhaifu mkubwa sana ktk maisha
Kiongozi yeyote hata wa makazini wanalazimika kuwa wakali ili kazi zifanyike, na nidhamu ichukue mkondo wake
Ni sawa kwenda kusema kwa wakubwa lakin kama yeye hawezi kujitambua kama kiongozi wa nyumba na familia basi ataendelea kupelekeshwa aisha yake yote.
Mwambie pia hakuna mapenzi ya namna hiyo bali anaburuzwa.
Abadilike na aanze kuwa Baba wa kweli, kuwa na familia sio lelemama.
 
Kuna kipindi jamaa huwa anafungiwa mlango analala sebuleni akichelewa....hii niliipata kwa hausigeli baada ya kumdadisi wanavyoishi.

aaaaaaaaaah hii mbaya sasa mkuu.. hamna mapenzi tena hapo bali visa na mikasa kama vip ampe talaka yake kila mtu ashike sabini zake
 
huyo rafiki yako alikosea toka mwanzo
alipogundua kwamba amezuia marafiki zake kufika nyumbani alitakiwa kujua sababu na hapo ndipo alitakiwa kumwonyesha huyu mkewe kwamba yeye ndiye dume
na kumbuka alikwisha pewa onyo wakati wa harusi
hata hivyo hajachelewa aanze sasa kuchukua nafasi yake kama mume na mapema kabla mzizi haujakomaa
 
Hayo yote unayoshauri dada Afro yalishafanyika, ila mke kawa kichwa ngumu!

Kama ameamua kuwa jeuri kiasi hicho
Mwambie huyo rafiki yako achukue likizo
asafiri kwa wiki au mbili
Asiache matumzi wala nini..
labda hapo ataitambua thamani ya mumeo..
 
Back
Top Bottom