Anahujumiwa! Wafanyabiashara wakubwa wakutana kwa siri, waazimia kuficha fedha zao, kutoagiza bidhaa

Bado hatujajiuliza kwa mini watu wanakwepa kodi? Rais mwenyewe amewahi kusema kuwa kodi zetu sio rafiki na zimekaa kikukomoana jee nani Amelishughulikia hilo?
Kama MTU hawezi kukwepa kodi na iliyoko sio rafiki kwa mini afanye biashara ya hasara? Anaacha kwanza
 
KULIKO KUHALALISHA KUTOKULIPA USHURU NI BARA WASEPE TU.
YAANI KULIPA USHURU WANAONA KAMA DHAMBI!!
KWELI MAZOEA UGONJWA!!
ii
 
Hao walizoea kutikisa nchi enzi ya Mkwere ....watambue serikali ina masikio marefu ...hata ukinong'ona na mkeo kitandani serikali itasikia ....wafate sheria otherwise wataumia ....
 
Wewe unaandika kwa kuangalia upande mmoja tu ttambua kuwa nyuma ya hawa wafanya biashara kuna watanzania wengi wapo kwenye ajira ndani ya makampuni ya hao wafanya biashara hivyo elewa iwapo yatatokea hayo watakao athirika sana ni hao waajiliwa.

Mkuu wafanyabiashara wana nguvu ndio lakini ni lazima wafuate sheria za nchi. Sikio lina umuhimu mkubwa lakini halizidi kichwa!

Kumbuka vilevile walipokuwa wanakwepa kodi walioathirika ni hao hao wananchi unaowasikitikia. Wajifunze kulipa kodi!!
 
Dr Pombe aache kukurupuka kwa ajili ya kujitafutia sifa.
Sifa za nini wakati ameshakuwa rais?Anatafuta sifa ili zimsaidie nini?
Hivi hata kama kuna wafanyabiashara Hawakulipa kodi sawasawa,si angemalizana nao bila kuwataja hadharani?
Hivi mfano Dr.Pombe anajua madhara aliyopata Azam,Bakhressa kwa kutangazwa kuwa halipi kodi?
Kwani wananchi wanachotaka ni majina ya waliokwepa kodi au wanataka kila mtu alipe kodi stahiki?
amka wew mbona ulikuwa uchekelea vibaka na majambazi wanavyotajwa na kova na silaha walizo tumia na hawa si majambazi kama walivyo majambazi wengine
 
Wasicheze na Serikali, kwa hiyo walitaka wasilipe kodi? basi waende Marekani kuwekeza kama itawavumilia...

Serikali ina mbinu nyingi sana za kudeal na watu kama hawa, nawasihi sana waache Mara moja, watajuta, wakumbuke aliyepo Ikulu ni JPJM siyo JK.

Ukiwasihi watajiona kama wanabembelezwa, nawe una dhiki nao, waache wathubutu ili waone matokeo yake, wajifunze kwa vitendo sidhani kama hawatarudia tena, sana sana wataishia kulaumiana na hao wanao washauri,
 
Hao wafanya biashara matapeli ni vyema wakafunga biashara. Kwanza hawa ndio chanzo cha kuwafanya wa fanya biashara halali wasilipe kodi stahiki.
Hao matapeli wakiondoka au kufilisika, watabaki wale halali na wapya watakuja
 
Bro usimuingize bakhressa hapa hahusiki na lolote huyu ni miongoni mwa wafanyabishara wenye nidhamu ya hali ya huu sana

nidham ipi wakat alikua anawapitishia watu makontena yasiyolipwa kodi na yeye mwenyewe alikua anafanya biashara bila kulipa kodi!!! kwa usafi upi kama analipa wafanyakaz kwa bahasha mkononi kwa nini hawalipi kupitia benki na hawalipii nssf? ushamuona mtu mtaan anafanya kazi kwa bakhressa ana maisha mazur ana gari na nymba?
 
Ukiwasihi watajiona kama wanabembelezwa, nawe una dhiki nao, waache wathubutu ili waone matokeo yake, wajifunze kwa vitendo sidhani kama hawatarudia tena, sana sana wataishia kulaumiana na hao wanao washauri,
hao wanao washauri ndiyo watawazunguka na kuchukua idea za biashara zao na kufanya kazi huku wakilipa kodi na wenyewe wakiendelea kufilisika
 
nidham ipi wakat alikua anawapitishia watu makontena yasiyolipwa kodi na yeye mwenyewe alikua anafanya biashara bila kulipa kodi!!! kwa usafi upi kama analipa wafanyakaz kwa bahasha mkononi kwa nini hawalipi kupitia benki na hawalipii nssf? ushamuona mtu mtaan anafanya kazi kwa bakhressa ana maisha mazur ana gari na nymba?
wale wahindi
 
Nyie akina nani? Chifu Yemba, Anna Mghirwa, Hashim Rungwe, Lyimo au Dovutwa?
kumbe hii nchi haiwezwi kuongozwa na wapinzani. hatua za kitoto zilizochukuliwa na serikali, eti wafanyabiashara wanalalamika? tungeingia je, watu wangekufa kabisa. tungewabana mbavu hadi waonyeshe makaratasi.
 
Hii issue ina ukweli ndani yake kwani kwenye mzunguko dola hakuna kwani tangia juzi dola imepanda sana kwa sasa si chini ya 2200
 
Mkapa amejichafua kwa kubeba masanduku ya kura fake, wizi wa mali za umma katika kumalizia uraisi wake na uchakachuaji wa matokeo ya kura.

uovu hufunika kwa nguvu kuliko wema. Kaharibu historia na mema yake yote na kwa hiyo hakuna mtu anamwamini huku heshima yake ikipotea kama mshumaa kwenye upepo.

Anglikuwa yule mkapa wa zamani, bila shaka angeweka historia. Lakini sasa, yeye atulie aasubiri matokeo ya ufufuo wa taifa.

Na hiyo petroli fake maana yake nini? Inapoingia wataalamu wa viwango wako wapi? Acheni utani.

Wafanya biashara wanapogoma kuingiza bidhaa na kufischa fedha, wanareact kwenye maumivu yapi? Naomba muwe mnatoa ufafanuzi japo kwa muhtasari ili tuweze kujadili.

Asubuhi njema.

Waache wagome kama sababu ni kutakiwa kulipa kodi, hata kama kutakuwa na maumivu lkn ni ya muda na baadaye tutakaa sawa tu!
Asiyetaka kulipa kodi aondoke nchini aende kwningine ambako hawalipi kodi!
 
Wewe unaandika kwa kuangalia upande mmoja tu ttambua kuwa nyuma ya hawa wafanya biashara kuna watanzania wengi wapo kwenye ajira ndani ya makampuni ya hao wafanya biashara hivyo elewa iwapo yatatokea hayo watakao athirika sana ni hao waajiliwa.

Athari ndiyo itakuwepo lkn baada ya muda tutakaa sawa, na kujenga nchi yenye maendeleo ya kweli na siyo ya kubabaisha, tunataka tuwe na mabilionea ambao utajiri wao unaonekana na unajulikana na siyo kuwa na mabilionea ambayo hawalipi kodi na mishe mishe, tunasema HAPANA!
Kama hawalipi kodi basi wasepe!
 
Mkuu nilianzisha Uzi kuwa tusijisifu kwa kukusanya Trillion 1.4 kwa kutegemea biashara za uchuuzi wa bidhaa za nje na kusahau uzalishaji wa ndani watu hawakuelewa ona sasa.
Kuagiza bidhaa nje ni matakwa binafsi ya mfanyabiashara na sio lazima sasa wakigoma tutapata wapi hiyo trilioni? Waweke sawa mkakati wa kuwezesha uzalishaji wa ndani sio hii mbinu ya kukamua majipu kwa waleta bidhaa pekee. Kilimo cha tija wamesahau, uvuvi hakuna jipya, mifugo ni ugomvi tuu na viwanda vidogo kabla ya vikubwa hakuna umeme kila siku ni hadithi tuu.
Mkuu utegemezi wa kodi ya ushuru wa bidhaa ni shida na hauwezi kuendesha nchi ingawa wengi walipinga kwenye andiko lako. Au kutegemea kodi kupitia pombe pia si jambo la kujivunia tunapaswa kutafuta vyanzo vipya endelevu!
 
Back
Top Bottom