Anahitajika mpishi ambaye anajua kupika

AbduliG

New Member
Nov 15, 2019
3
20
Habari zenu wana JF,

Anahitajika mpishi ambae anajua kupika (mwenye uzoefu na iyo kazi atapewa kipaombele) pamoja na kuwa na uwezo wa kupima sahani za chakula kwa ajili ya mgahawa.

Pia anahitajika mpishi mwengine kwenye chipsi na nyama choma, watakuwepo wawili na mmoja ameshapatikana bado mmoja. Kuhusu malipo ni suala la maongezi.

Uaminifu, usafi na kujituma kwenye kazi ni muhimu. Eneo la biashara ni Dar es salaam Mjini karibu na chuo cha DIT na/au CITY MALL, kazi inategemewa kuanza jumatatu ya kesho kutwa 28 Disemba 2020.

Nitangulize shukrani.

NB: Namshukuru mungu watu wote wameshapatikana.
Nikutakieni heri ya mwaka mpya, mungu ajaalie uwe mwaka wa mafanikio katika kutafuta riziki na mengine yalokuwa mema na atuepushe na janga linaloikabili dunia. Asanteni.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom