Elections 2010 Anafaa kuwa rais kwa kisasi hiki?

ZLATAN

Senior Member
Oct 5, 2010
150
18
Ndugu zangu wa-tz, sitochoka kutoa duku duku langu juu ya kiongozi huyu mumtakae nyinyi.

Najua wengi mtachukizwa, lakini hii ni haki yangu ya msingi ya kikatiba, hivi kiongozi mwenye visasi kama huyu wa nini? Au taarifa hii mmeifumbia macho na masikio kwa makusudi?

Huyu slaa mnaedhani atakuwa rais, ndiye aliyemchimbia mkwara ndugu mwakipesile.

Kama ndoto zake za kuingia ikulu zilivyomtuma, akaamua kumchimbia mkwara kwa kuona ni kikwazo kwake.

Nna mashaka si mwkipesile tu atakayetafuta pa kupita, watanzania lukuki watakiona kwa ufedhuli atakaoufanya.

Mpaka walom-support katika jf watajuta ila itakuwa too-late.

Lakini wadau wa jf msiogope, kaka/baba mdogo/mjomba 'enu hatoingia ikulu.

Kikwete ndio chaguo la wa-tz wengi.

Chagua ccm, chagua kikwete.
 
IHIV WANAOIPENDA NA KUSHABIKIA CCM NA KIKWETE NI WATANZANIA?
KUIPENDA ccm na kikwete inatakiwa uwe na moyo km wa mwenda wazimu.
 
Mimi niko tofauti sana na wana jf wengi.............hakuna mahali ambapo nimewahi kuandika jk nikimaanisha kikwete kwani naona sio kumtendea haki jk nyerere........hafanani hata kidogo na wala hawezi kukaribia kufanana na jk nyerere nashauri muitenei jm kwa kifupi au kikwete kwa kirefu.......
 
Lakini kama kweli Slaa ana visasi, naamini havitakuwa tofauti na vile vya Kikwete dhidi ya Babu Seya na watoto wake, vya Mangula, Stephen Mashishanga na wengine wengi ambao hawakuwa kwenye mtandao wake wakati wa kampeni za mwaka 2005. Ukitaka, tutaorodhesha hapa ni visasi kiasi gani amevifanya Kikwete. Kikwete ni mnafiki usipime, anakuua huku anakutabasamia, lakini Slaa amesema moja kwa moja bila kuficha. Na huo ndo uongozi tunaoutaka Tanzania, tuachane na sura za tabasamu huku unawamaliza wananchi.
 
Wewe vipi unataka rais awe msanii kama huyu wa sasa?umetumwa?peleka salamu!
 
You have a point:

Julius Kambarage Nyerere (JKN)
Jakaya Mrisho Kikwete (JMK)

Kama tunafupisha kwa kuangalia majina mawili ya kwanza itakuwa:

Julius Kambarage (JK)
Jakaya Mrisho (JM)

Lakini kama tunafupisha kwa kuacha jina la katikati itakuwa:

Julius Nyerere (JN)
Jakaya Kikwete (JK)
 
angalia mda si mrefu na wewe itapanda kichwani kama ndugu yako MS!! ohoooo...haya!
 
Kama huyo mgonjwa wenu anakubalika na wengi mnapata tabu ya nini kumnadi kwa mabango nchi nzima? Sasa wewe mjahidina wewe umesahau zile enzi zenu za JINO KWA JINO? Dr wa ukweli akisema atawashughulika wakorofi mnamuona ana kisasi, Mbona huyo kifaulongo wenu kamfunga babu seya kwa wasi wasi wa kupigiwa ngoma yake? Wacheni hizo, safari hii mume kalia msumari wa moto
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom