Anaandika Ballon Ngetti kada wa CCM

Omary Ndama

JF-Expert Member
Apr 16, 2017
3,367
4,056
BLACK DAY TANZANIA 2019

NINAANDIKA posti hii kwa uchungu mwingi. Ni miongoni mwa maandiko machache niliyowahi kuandika huku machozi yakinilenga sawa na mtu aliyehukumiwa kunyongwa. Naililia mama yangu, nchi yangu takatifu Tanzania. Ninajiuliza nitapata wapi Tanzania nyingine hii ikitoweka maana kutoweka ni hakika!

Ninaandika posti hii nikiwa nimejitoa kuitwa "mchochezi" kwa ajili yenu wajoli wa nchi hii ya Mwalimu Nyerere na Mzee Karume pamoja na kina Kassim Hanga nakadhalika.

Ndugu zangu Taifa letu teule linapitishwa kwenye miiba na makorongo ambayo usalama unazidi kuwa shakani siku hadi siku.

Ninaomba kwa heshima na ridhaa yenu mniruhusu kutambulisha kwenu siku nyeusi kwa Tanzania ambayo itakuwa ni tarehe 5/5/2019(Jumapili) Nakuombeni siku hii iwe muhimu kwa kila Mtanzania anayeipenda nchi kwa moyo wa dhati bila kujali tofauti yoyote katika jamii.

Ndugu zangu naomba siku hii iwe maalumu kwa ajili ya kukumbuka ndugu zetu waliopoteza maisha yao kwa namna yoyote ile lakini vifo vyao kwa namna moja au nyingine vimehusishwa na siasa za toka 2015!

Sio tu waliopoteza maisha lakini pia walioteswa kimwili, kiakili au hata kiuchumi kwa kulilia demokrasia na uhuru kamili wa kikatiba. Wapo watu waliotekwa na kupotea hadi leo haijulikani Wako wapi na kama waliuawa ni kwa njia gani? Je, walipigwa risasi kama Lissu, je walipigwa shoka vichwani, je walichinjwa au kupigwa mawe?

Wapo watu waliokamatwa kwa tuhuma za uchochezi na "kuhifadhiwa" na polisi kwa siku zisizo za kisheria (nikiwemo), wapo watu waliotekwa na kuteswa na kupokonywa mali zao (Mbowe), wapo wanaoendelea kusota mahabusu. Hatujui kesho ni zamu ya nani maana sie miti mibichi tulifanyiwa hivyo itakuwaje enyi miti mikavu?

Ndugu zangu katika utawala huu zipo ndoa zilizosambaratika kwa Sababu za siasa. Katika zamu hii usalama wa watu umekuwa shakani kiasi kwamba hata viongozi wa dini wamefyata mikia yao. Ni Enzi za hatari kuwahi kutokea katika historia ya nchi hii!

Ndugu zangu orodha ni ndefu kila mmoja anaweza kutaja.

Tarehe 5/5 tufanye nini? Naam, kwa kuwa ni siku nyeusi nakuomba kila mtu alipo kwa nafasi yake kuwasha mshumaa mmoja hata kwa dakika 10 na kuwaombea wahanga wote walioumia toka 2015 bila kusahau matukio ya kihistoria! Katika hizo dakika 10 sema na Mungu Wako kwa lugha yako ili Mungu aiponye Taifa na mambo haya! Kama ni familia basi kila mmoja awashe mshumaa baada ya mkuu wa kaya kutoa maelezo mafupi kwa nini tunafanya hivyo. Kwa wale waliokaribu na makaburi ya watu kama Mawazo fikeni kaburini na mishumaa yenu kutoa sala zenu. Hakika Mungu ni mwema atabadilisha mioyo ya watesi wetu. Shetani hajawahi kushinda vita!

Watakaokutwa baa washeni mishumaa na kusimama kwa dakika mbili kuwakumbuka kina Ben Saa8 na Azory Gwanda! Walisimama katika zamu yao sasa ni zamu yako!

Cha msingi picha zipigwe na ku-share na watu mitandaoni ili ku-share spirit na wapendwa wetu. Tuwakumbuke walio magerezani maana si wote wana makosa! Mungu atawakumbuka!

Kama kuna ubunifu wowote unaweza kufanyika basi ufanyike kwa nia njema. Haya yatakuwa ni kuifikishia ujumbe watawala kuwa hatufurahishwi na baadhi ya mambo yao! Hashtag itakayotumika ni #BlackDayTanzania2019.

Kwa wale watakaoweza kuandika makala juu ya matukio mbalimbali yaliyotokea wafanye hivyo lakini kwa kuzingatia sheria za nchi. Tushikamane katika hili kui-alert umma!

Ujumbe huu ufike kila mahali kutoka mijini hadi mashambani na milimani. Hatuwezi kuandamana tutapigwa hadi tuchakae lakini hata kwa kuwanunia watawala dunia itatusikia. Rangi ya siku hiyo ni nyeusi. Nakaribisha mchango wa kuboresha zaidi!
#AchaWoga2020
0763 014452
 
Mleta uzi umewasahau waliokufa kibiti,rufiji na mkuranga nao wanahitaji kuombewa
 
Sasa hv hata kuandika Mungu Ibariki Tanzania unajihis ww ni mnafiki nambari 1..

Anywýs Mungu Ibariki Afrika!
 
BIGUP JF.
Bahati mbaya mawazo kama haya yamebaki kuandikwa kwenye social media kama jf ila kwingine ni ngumu sana, hata page yako ya facebook unawaza mara mbili.

Bigup ndugu mtanzania, but siku moja aridhi ya mama Tanzania itakuja kutulilia siku moja kwa kutoitendea hali.
 
Back
Top Bottom