Anaandika Juma Aweso, Waziri wa Maji

Anaandika Juma Aweso, Waziri wa Maji

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,169
Reaction score
898
Tunawaomba wananchi kutumia maeneo rasmi ya huduma ya maji kuepusha Taharuki.

"Nimefatilia zaidi swala la upatikanaji wa Maji Kijiji cha Iponda baada ya taarifa zilizowekwa mtandaoni kwa kutuma timu ya wataalamu wafike haraka na kunipa taarifa sahihi; lengo kuu ni kujiridhisha na kuwa na taarifa sahihi na kama kweli hali ni mbaya basi kupata suluhu ya haraka na kutoa mrejesho.

Baada ya timu kufika ukweli ni kwamba Kijiji Cha iponda kilichoko Kata ya ilembula, Wanging'ombe kwa sasa kinapata maji kwa kutumia chanzo Cha maji cha Mbukwa; wakati huohuo tunaendelea kukamilisha mradi mkubwa wa Maji wa miji 28 katika mji wa Wanging'ombe wa Bil.43.7 ukitegemewa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu ambapo kijiji Cha iponda ni mojawapo kitakachonufaika na mradi huu hivyo tutaongeza maji zaidi.

Pamoja na haya yote ukweli ni kwamba wananchi wanapata Maji kwasasa, maeneo yote muhimu kuanzia majumbani, mashuleni, vituo vya afya na sehemu zote za kijiji zina huduma ya Maji,
Kilichotokea ni kwamba wale walioonekana wananchi wakichimba mchanga ni wananchi wanaofyatua matofali pamoja na wanajishughulisha na mambo mengine na sio maji ya matumizi ya binadamu ama majumbani.!

Lengo la ujumbe huu sio kukanusha taarifa ama kufafanua kwani sio vibaya kupashana habari na sio kweli kwamba tumekwisha maliza vijiji vyote ama maeneo yote kupata Maji; bali kutoa wito kwa wananchi kwanza kuthamini jitihada za huduma za serikali yao na pia kuepuka upotoshaji unaoweza kuleta taharuki na migongano na kuwa wakweli ili kushikamana kutoharibu taswira ya nchi yetu.

Wito mwingine ni kuwaomba wananchi kutumia maeneo rasmi ya huduma ya maji na sio maji mengine yasio salama ambayo wakionekana wanafanya hivyo inaleta ukakasi na hofu kana kwamba eneo hilo halina huduma ya Maji safi,hili halina sheria ya kumbana mwananchi bali ni utashi na ustaarabu binafsi na tutaendelea kutoa elimu zaidi na pia wahandisi wa Maji waendelee kutambua maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma kabisa ama karibu tupeleke maji karibu ili wananchi wasipate shida kama hii.

Mwisho nchi yetu ni kubwa sana, tunaendelea na kazi ya kuijenga, changamoto za Maji hazijaisha lakini mapambano yanaendelea; pia kuna hatua tumepiga tuendelee kujipa moyo na zaidi kazi hii inahitaji tushirikiane na kuifanya kwa pamoja."




 
Back
Top Bottom