Ana mimba na Condom imetumika kwa usahihi

Ndo tatizo la mapenzi ya siku hizi baada ya kuangalia tatizo ni nini katika ndoa yako mlisuruhishe ,matokeo yake mnaona njia muhimu ya kutatua tatizo hilo ni kutafuta mwanamke au mwanaume mwingine nje baada ya kukaa na kujadili nini tatizo ili mlitatue.
Plz mlio na ndoa,wachumba sio lazima mpate msada toka kwa watu wa marekani ' vunja ukimya zungumza na mwezako'

Nimekusoma mtu wangu
 
Mkuu, hii n ishu complex.
For sure, hapa kuna mtu ataharibiwa dental formula kama si kushikishwa ukuta.
Derimto, usitumie vpmo vya macho kwa mwanamke, ile maneno yao HAISOMI MITA ATI. Mimi nahisi huyo mwanamke si mwaminifu, na amekuwa anatafuta penzi la kumtosheleza kila atakpoweza. halafu ktk hali za wizi na haraka2 umakini unapungua sn, hvyo yeye anamjua kbsa aliempa hiyo mimba, awaambieni bana, asiisumbue MAHAKAMA bure![/QUOTE]

Unamaanisha Derimto asisumbuke eeh,,ha ha ha!ukweli ingawa wote walikuwa wanacheat lkn lazma kuna mahali mwanamke alicheza rafu zaidi ya cheater mwenzie.
 
kama kondom ilitumika na bidada hajagawa nje.....basi walitumia kifutio kimoja......huu ni msala.......na kama hajakutana na mumewe miezi mitano hilo ni janga la taifa.....duh sasa huyu sijui tunamshaurije......mi naona suluhu ni moja tu....nitarudi baadae

Hili la kifutio kimoja hili nalo neno kunaweza kuwepo uzembe wa namna hiyo
 
Derimto kwa nini ulipojua kuwa wanacheat hukuwashauri kuacha???haya yote yasingetokea!

Dogo aliufatilia huu mzigo muda mrefu sana bila mafanikio na mimi nilijua kuwa alishanyimwa ila nadhani maombi yake yalikubaliwa siku za karibuni na ndipo yakawakuta haya makubwa wasiyoyategemea
 
@ lukolo and demrito the percentage stated above ni kwa 'condom failure rate as a contraceptive' and not as a barrier against VVU.
 
ule mchuzi tu wa mwanzoni unatosha kumpa mimba,kama aligusisha kichwa na mchuzi ukitoka hapo hapo,walee mimba tu
 
Matumizi ya condom is all but personal assessment! Mtumiaji anajua kama alitumia au la!
 
Dogo aliufatilia huu mzigo muda mrefu sana bila mafanikio na mimi nilijua kuwa alishanyimwa ila nadhani maombi yake yalikubaliwa siku za karibuni na ndipo yakawakuta haya makubwa wasiyoyategemea

Bado sikuelewi,,,labda utakapojibu memo ya Preta,,,kwanini dogo aendelee kufatilia wakati alishaoa Derimto????halafu inaonekena ulikuwa mshenga,,haya hii mimba inakuwaje??mume halali atashikishwa?au mtaendeleza dhambi mkaitoe??mtihani huo
 
Ntataka kutafunia na makukuru,,,halafu huyu Derimto huyu!!naomba umpe memo ijumaa

Jamani majungu hayo mi.huwa nawachanganya sasa mkiwa na ushirikiano na Preta si mtaniumbua hebu katulieni huko nipate madaktari humu
 
Mkuu, hii n ishu complex.
For sure, hapa kuna mtu ataharibiwa dental formula kama si kushikishwa ukuta.
Derimto, usitumie vpmo vya macho kwa mwanamke, ile maneno yao HAISOMI MITA ATI. Mimi nahisi huyo mwanamke si mwaminifu, na amekuwa anatafuta penzi la kumtosheleza kila atakpoweza. halafu ktk hali za wizi na haraka2 umakini unapungua sn, hvyo yeye anamjua kbsa aliempa hiyo mimba, awaambieni bana, asiisumbue MAHAKAMA bure!

Nimekusoma mkuu ila nadhani mahakama hii ya jf itatoa hukumu ya kitaalamu zaidi ya mitizamo yangu binafsi nimeshawahi kusuluhisha vimeo vingi kwa ufundi mkubwa ila hapa nahisi kama nachemsha vile kulingana na tukio lenyewe
 
mwambie aende akapime DNA!!!!!
kuna harufu ka uchakachuaji hapo..:teeth:
what a shame,sijui wataficha wapi nyuso zao pindi wapenzi wao wakijua upuuzi wao...
wote ni vicheche,ila huyo mwanamke kazidi!!!usimtetee kwa vile unamjua...mtu ndoa iko matatani miezi mitano tu kaamua kugawa nje???!!!.. huyo ni kicheche...period!...utamwaminije mtu wa hivi kama hajachakachuliwa kwingine pia?
 
ule mchuzi tu wa mwanzoni unatosha kumpa mimba,kama aligusisha kichwa na mchuzi ukitoka hapo hapo,walee mimba tu

Nashukuru hii nayo ni point muhimu nayakusanya haya yote niangalie nitatoa ushauri wa aina gani
 
Kitaalamu, ili fertilization itokee huwa kunahitajika milions of sperms kwa ajili ya kuyeyusha ukuta wa yai la mwanamke na baada ya hayo mapambano ya kuyeyusha yai, ni sperm moja tu huwa inafanikiwa na ndipo ule ukuta unazuia uwezekano wa sperm nyingine kuingia. Kama umetumia kondom kwa usahihi, hata kama kuna kitakachopita, bado kinaweza kisitoshe kusababisha mimba. Labda kama wakati wa uvuaji wa hiyo kondom ilitokea bahati mbaya zikamwagikia. Lakini katik hali ya kawaida kama matumizi yalikuwa sahihi, hakuna kitu kama hicho. Aulizwe vizuri huyo dada alipita wapi kwingine. La sivyo basi walishirikiana kifaa cha kufutia or kingine chochote.
Suluhu pekee ni dada kuomba talaka kwa mmewe kwa kuwa tayari ana migogoro naye, halafu dogo atunze mtoto kwa kuwa tayari ana mke. Akiona vema na kwa kuwa umesema wanapendana basi amuoe, awe mke wa pili.

?????????????????:embarrassed:
 
Leo nimekutana na mkasa tata sana nimeshindwa kuamua kesi hii iliyonichukulia zaidi ya masaa matano.

Kuna rafiki mmoja anatembea na dada moja aliyeolewa kwa ndoa na ana watoto wawili ila ANA MATATIZO MAKUBWA NA MUMEWE NA SUALA LA MALAVIDAVI KWAO NI KIKAO KIKAE na mpaka mkasa huu unatokea ni kwamba hajapewa na mumewe kwa muda wa miezi 5 sasa.

Kwa kuzingatia hilo mwanamke akamtafuta jamaa ambaye anaona kuwa anampenda kutokana kwamba alifuatilia kwa siku nyingi sana zaidi ya miaka kumi bila mafanikio mpaka wakati huu ambapo dada aliona ndiyo kipindi cha faraja kwao na kumpa mavituziiii.

Na wameanza mahusiano ya kimapenzi zaidi ya miezi miwili na wamefanyana mara mbili tu mwezi uliopita na wiki iliyopita na hawa watu wanaonekana kuaminiana na kupendana hasa ukiwaangalia tu.

Lakini leo mchana Dogo kanipigia cm.akanisihi sana nimfuate mojawapo ya hospitali za binafsi iliyotulia sana kwenda kuamua kesi yao kwamba yeye ametembea na huyo mwanamke mara mbili tu tena kwa tahadhari kubwa na suala la ngono salama yaana matumizi ya Condom yalizingatiwa sawasawa na mwanamke alikuwa wa kwanza kukiri hilo na alilihakikisha zoezi hilo na walipomaliza hakuona Condom kama imepasuka. Lakini aligundua kuwa siku zake zimepita na hivyo alikwenda kumwona Dr. Na majibu yalivyoka yalionyesha kuwa mwanamke ni mjamzito akajihisi kuchanganyikiwa akampandia jamaa hewani na kusababisha kikao hiki ambacho nimeshindwa kukiamua maana MWANAMKE ANADAI HAJAFANYA NA MUMEWE MIEZI 5 SASA KUTOKANA NA MIGOGORO YAO NA DOGO ANA MKE NA WATOTO WATATU AMECHANGANYIKIWA HAJUI LA KUFANYA MAANA HAJUI MIMBA HIYO IMEPATIKANAJE na suala la kutoa mimba kwao halipo wanadhani yatakuwa makosa mara mbili hasa kulingana na imani zao naombeni wana jamii mnisaidie kuamua hii kesi nimewambia tuonane kesho jioni ila ki ukweli sina jibu la kitaalamu kuwapa hawa watu na wanapendana kufa ila dogo amechanganyikiwa.

Nawasilisha kwenu naombeni mchango wa mawazo tafadhali tuokoe hili jahazi hasa madaktari walioko humu.

Wakati wa kufanya uzinzi wao walitegemea nini hayo ndio majibu
 
Bado sikuelewi,,,labda utakapojibu memo ya Preta,,,kwanini dogo aendelee kufatilia wakati alishaoa Derimto????halafu inaonekena ulikuwa mshenga,,haya hii mimba inakuwaje??mume halali atashikishwa?au mtaendeleza dhambi mkaitoe??mtihani huo

Kama kuna ukweli wa kiasi fulani nilishawahi kuwanganisha kimazungumzo kama miaka 4 iliyopita na hapakuwa na mafanikio ila walivyokuja kuonjana hawakuniambia zaidi wameniambia baada ya kulikoroga na siwezi kuwatema kirahisi ni marafiki jamani
 
tusiamini amini condom sana,bt dis lady kama aliweza kutembea na mshkaj huyu,we cant rule out the posibility anaeza kawa katembea na mwingine kabla...cmshauri kuitoa,ila...duh kichwa kinauma.
 
mwambie aende akapime DNA!!!!!
kuna harufu ka uchakachuaji hapo..:teeth:
what a shame,sijui wataficha wapi nyuso zao pindi wapenzi wao wakijua upuuzi wao...
wote ni vicheche,ila huyo mwanamke kazidi!!!usimtetee kwa vile unamjua...mtu ndoa iko matatani miezi mitano tu kaamua kugawa nje???!!!.. huyo ni kicheche...period!...utamwaminije mtu wa hivi kama hajachakachuliwa kwingine pia?

Mwanamke ameolewa ana miaka 7 ya ndoa na ana watoto wawili tayari na huyo mume wake ila wameishi kwa mbinde sana na mume wake huyo na huyu wa kwetu ana mke na watoto watatu HIZI NI NDOA MBILI ZINATISHIA KUBOMOKA
 
Kama kuna ukweli wa kiasi fulani nilishawahi kuwanganisha kimazungumzo kama miaka 4 iliyopita na hapakuwa na mafanikio ila walivyokuja kuonjana hawakuniambia zaidi wameniambia baada ya kulikoroga na siwezi kuwatema kirahisi ni marafiki jamani

Hapo kinachotakiwa ni kujua what next,,maana mimba imeshaingia.Nahisi kitu,,:A S-alert1: ngoja nilale mie
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom