Ana mimba na Condom imetumika kwa usahihi

Derimto

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
1,307
306
Leo nimekutana na mkasa tata sana nimeshindwa kuamua kesi hii iliyonichukulia zaidi ya masaa matano.

Kuna rafiki mmoja anatembea na dada moja aliyeolewa kwa ndoa na ana watoto wawili ila ANA MATATIZO MAKUBWA NA MUMEWE NA SUALA LA MALAVIDAVI KWAO NI KIKAO KIKAE na mpaka mkasa huu unatokea ni kwamba hajapewa na mumewe kwa muda wa miezi 5 sasa.

Kwa kuzingatia hilo mwanamke akamtafuta jamaa ambaye anaona kuwa anampenda kutokana kwamba alifuatilia kwa siku nyingi sana zaidi ya miaka kumi bila mafanikio mpaka wakati huu ambapo dada aliona ndiyo kipindi cha faraja kwao na kumpa mavituziiii.

Na wameanza mahusiano ya kimapenzi zaidi ya miezi miwili na wamefanyana mara mbili tu mwezi uliopita na wiki iliyopita na hawa watu wanaonekana kuaminiana na kupendana hasa ukiwaangalia tu.

Lakini leo mchana Dogo kanipigia cm.akanisihi sana nimfuate mojawapo ya hospitali za binafsi iliyotulia sana kwenda kuamua kesi yao kwamba yeye ametembea na huyo mwanamke mara mbili tu tena kwa tahadhari kubwa na suala la ngono salama yaani matumizi ya Condom yalizingatiwa sawasawa na mwanamke alikuwa wa kwanza kukiri hilo na alilihakikisha alilisimamia zoezi hilo na walipomaliza hakuona Condom kama imepasuka. Lakini baada ya kama wiki tatu aligundua kuwa siku zake zimepitiliza na hivyo alikwenda kumwona Dr. Na majibu yalivyoka yalionyesha kuwa mwanamke ni mjamzito akajihisi kuchanganyikiwa akampandia jamaa hewani na kusababisha kikao hiki ambacho nimeshindwa kukiamua maana MWANAMKE ANADAI HAJAFANYA NA MUMEWE MIEZI 5 SASA KUTOKANA NA MIGOGORO YAO NA DOGO ANA MKE NA WATOTO WATATU AMECHANGANYIKIWA HAJUI LA KUFANYA MAANA HAJUI MIMBA HIYO IMEPATIKANAJE.

Suala la kutoa mimba kwao halipo wanadhani yatakuwa makosa mara mbili hasa kulingana na imani zao na mwanamke anaona kutoa mimba litakuwa kosa mara mbili tena la kuua ambapo hataweza kujisamehe hata yeye mwenyewe na tayari dogo anaonyesha kukubaliana naye anatamani kuondoka anawaza watoto wake hawezi kuwaacha watateseka sana maana huyo Mumewe tayari alishawahi kukiri kuzaa na House Girl wao ambaye wanatoka kijiji kimoja na huyo dada miaka michache iliyopita.

Zaidi sana jamaa ni mbabe hata kutoa matumizi ya kawaida kama chakula kwa watoto ni tatizo ni mwanamke ajibane kazini kwake afuge kuku na vi miradi vidogovidogo ndipo aendeshe familia mwanaume ni mkali kwenye hela kiasi kwamba akimpa pesa ya matumizi hata 5000 anaweza kumsimanga hata mbele za watu na inajulikana kwa wanafamilia wa pande mbili kuwa mwanume ana jimama la kiswahili na aliahidi kujirekebisha lakini haikufanyika hivyo.

Dogo anawaza kutorosha pamoja na watoto wake ampangishie nyumba mbali mji wanaoishi mwanamke anaogopa maana hakuondoka pale walipokuwa na ugomvi mkubwa leo huu wa kichinichini ukimwondoa anawaza wanafamilia yake hasa mama yake anaweza akachanganyikiwa na hata kuugua kulingana na imani yake.

Kuwabeba watoto wa huyo Bwana na kuondoka nao anaogopa kwa madai kwao ni washirikina yanaweza kumkuta makubwa na suala la kwenda kumhadaa na kufanya naye mapenzi ili waseme ni mimba ya nyumbani linakuwa gumu kulingana poor communications zilizoko humo ndani.

Naombeni wadau mbalimbali na wanajamii mnisaidie kuamua hii kesi nimewambia tuonane kesho jioni ila ki ukweli sina jibu la kitaalamu kuwapa hawa watu na wanapendana kufa ila dogo amechanganyikiwa.

Nawasilisha kwenu naombeni mchango wa mawazo tafadhali tuokoe hili jahazi hasa madaktari walioko humu.
 
Labda mdada ni muumini mzuri wa kugawa,,so inawezekana dogo anasingiziwa tu!akome
 
Shughuli nzito hii, labda condom ilivuja au mama hajawa mkweli labda kuna sehemu nyingine alipita. Condom isiaminike 100% maana yanaweza kabisa kutokea yasiyotarajiwa kutokea hata kama condom imetumika.
 
eidha huyo demu kachakaliwa na mtu mwingine au kondom ilikua bomu maana kondom nazo si za kuziamini!halafu huyo demu hajatulia yani miezi 5 tuu kashindwa vumilia katoka nje ya ndoa mhhh!
 
mkuu hiyo kesi ngumu, ila condom sio 100% sure protection kwa mimba, na vile vile huwezi kujua demu kagawa wapi na wapi... kwani kama kaweza kumpa huyo mshkaji kuna uhakika gani hajagawa kwingine nyama kwa nyama?

hata mi nimebaki njia panda:whoo:
 
Labda mdada ni muumini mzuri wa kugawa,,so inawezekana dogo anasingiziwa tu!akome

Ukiacha huyu dogo tunayefahamina zaidi ya 20 fulani vile huyu dada namfahamu kama 13 iliyotulia na ninawafahamu na historia yao ndiyo maana walikubalinana kuniita huyu kama ni kupima tabia za mtu kwa macho namkatalia na yeye analalamika kuwa kizazi chake kiko karibu sana jamani niko njia panda naogopa kutoa ushauri mbovu kwao
 
NO. The case may be true! And favors the lady. Scientifically the per-year pregnancy rate for all time consistent, proper and effective condom users is 2%. The figure may actually jump to 20% depending on a specific population. So in summary the case is in favor of the lady.....but regarding the moral aspect of it, yaani kumtia mimba mke wa mtu, I reserve my comments 4 now
 
kama kondom ilitumika na bidada hajagawa nje.....basi walitumia kifutio kimoja......huu ni msala.......na kama hajakutana na mumewe miezi mitano hilo ni janga la taifa.....duh sasa huyu sijui tunamshaurije......mi naona suluhu ni moja tu....nitarudi baadae
 
Kitaalamu, ili fertilization itokee huwa kunahitajika milions of sperms kwa ajili ya kuyeyusha ukuta wa yai la mwanamke na baada ya hayo mapambano ya kuyeyusha yai, ni sperm moja tu huwa inafanikiwa na ndipo ule ukuta unazuia uwezekano wa sperm nyingine kuingia. Kama umetumia kondom kwa usahihi, hata kama kuna kitakachopita, bado kinaweza kisitoshe kusababisha mimba. Labda kama wakati wa uvuaji wa hiyo kondom ilitokea bahati mbaya zikamwagikia. Lakini katik hali ya kawaida kama matumizi yalikuwa sahihi, hakuna kitu kama hicho. Aulizwe vizuri huyo dada alipita wapi kwingine. La sivyo basi walishirikiana kifaa cha kufutia or kingine chochote.
Suluhu pekee ni dada kuomba talaka kwa mmewe kwa kuwa tayari ana migogoro naye, halafu dogo atunze mtoto kwa kuwa tayari ana mke. Akiona vema na kwa kuwa umesema wanapendana basi amuoe, awe mke wa pili.
 
NO. The case may be true! And favors the lady. Scientifically the per-year pregnancy rate for all time consistent, proper and effective condom users is 2%. The figure may actually jump to 20% depending on a specific population. So in summary the case is in favor of the lady.....but regarding the moral aspect of it, yaani kumtia mimba mke wa mtu, I reserve my comments 4 now

Thnx. Losikoki kwa kuonyesha sehemu ya uzoefu wako hili ni kosa tena kubwa katika jamii na ni aibu ila wameshakiri suala ni kwamba wanatokaje ntakesha humu kukusanya majibu ya kuwaridhisha
 
NO. The case may be true! And favors the lady. Scientifically the per-year pregnancy rate for all time consistent, proper and effective condom users is 2%. The figure may actually jump to 20% depending on a specific population. So in summary the case is in favor of the lady.....but regarding the moral aspect of it, yaani kumtia mimba mke wa mtu, I reserve my comments 4 now

Nafikiri hizi unaongelea probability za VVU. sidhani kama % probability ni moja. Kwani HIV ni mdogo zaidi ya mara mia moja ya sperm. Kwa hiyo sitarajii kuwa na percentage inayofanana. Otherwise kuwe kuna uzembe wa wazi unaofanywa na wahusika.
 
Ukiacha huyu dogo tunayefahamina zaidi ya 20 fulani vile huyu dada namfahamu kama 13 iliyotulia na ninawafahamu na historia yao ndiyo maana walikubalinana kuniita huyu kama ni kupima tabia za mtu kwa macho namkatalia na yeye analalamika kuwa kizazi chake kiko karibu sana jamani niko njia panda naogopa kutoa ushauri mbovu kwao

Derimto kwa nini ulipojua kuwa wanacheat hukuwashauri kuacha???haya yote yasingetokea!
 
Nafikiri hizi unaongelea probability za VVU. sidhani kama % probability ni moja. Kwani HIV ni mdogo zaidi ya mara mia moja ya sperm. Kwa hiyo sitarajii kuwa na percentage inayofanana. Otherwise kuwe kuna uzembe wa wazi unaofanywa na wahusika.

Lukolo nimemuuliza dr.1 nimejibiwa kitu kama kinachofanana na hiki na zaidi akasema unaweza kupata maambikizi ya ukimwi hata kama condom imetumika lakini suala la mimba anatatizika kama mimi na wewe hana maelezo ya kuridhisha suala la mke pili ni ndoto kwa dogo kulingana na kwao wlivyo
 
Mkuu, hii n ishu complex.
For sure, hapa kuna mtu ataharibiwa dental formula kama si kushikishwa ukuta.
Derimto, usitumie vpmo vya macho kwa mwanamke, ile maneno yao HAISOMI MITA ATI. Mimi nahisi huyo mwanamke si mwaminifu, na amekuwa anatafuta penzi la kumtosheleza kila atakpoweza. halafu ktk hali za wizi na haraka2 umakini unapungua sn, hvyo yeye anamjua kbsa aliempa hiyo mimba, awaambieni bana, asiisumbue MAHAKAMA bure!
 
Ndo tatizo la mapenzi ya siku hizi baada ya kuangalia tatizo ni nini katika ndoa yako mlisuruhishe ,matokeo yake mnaona njia muhimu ya kutatua tatizo hilo ni kutafuta mwanamke au mwanaume mwingine nje baada ya kukaa na kujadili nini tatizo ili mlitatue.
Plz mlio na ndoa,wachumba sio lazima mpate msada toka kwa watu wa marekani ' vunja ukimya zungumza na mwezako'
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom