Ana Miaka 40, Hana Mtoto Wala Hana Mwanaume

Ana Miaka 40, Hana Mtoto Wala Hana Mwanaume

Yupo mwanamke mmoja anayejitambulisha kwa jina moja la Nekesa ambaye amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana akilalamika kwamba ana umri wa miaka 40 na bado hajapata mume wala mtoto.

Kwa mujibu wa video zake kwenye Tiktok, hafurahishwi na upweke unaomuandama kwa muda mrefu na kubainisha kuwa maisha yake hayaendi ipasavyo na anaelekea kukata tamaa.

Katika moja ya video hizo, Nekesa anaonekana akiwa amezama kwenye lindi la mawazo na kudai hana watoto ila anatumai kuwa ataolewa siku moja.

Nekesa anasema anamuomba mno Mwenyezi Mungu siku moja amjaalie mwanaume mmoja ambaye atampa huba lake lote.

“Miaka 40 sasa, sina watoto, mume au kuwa kwenye uhusiano wowote. Mungu wangu nisaidie,” Nekesa anaomba akionesha masikitiko yake.

Maelezo ya Nekesa yamewagusa wengi huku wakionesha kumpa matumaini kwamba siku moja atapata mume atakayempenda na kumpatia watoto.
Mpe namba yangu
 
We need to Know the negative side of her.Huyo lazima Ana mapungufu fulani ambayo yamemsababishia upweke alionao Sasa.She needs to be transparent enough.
 
Hapo ndio penye. Siku hizi vijana hawatongozi sijui wamepatwa na nini? Yaani hata zile psssst mtaa wa Kongo hawapati.
Wanaogopa mizinga wengi wanaingia na gia ya kuomba urafiki, baada ya hapo wanakulana kimasihala then mwana anatambaa
 
Wanaogopa mizinga wengi wanaingia na gia ya kuomba urafiki, baada ya hapo wanakulana kimasihala then mwana anatambaa
Sasa uliona wapi mtu unatongoza eti nikuoe, huo wazimu. Hata ukipika uji lazima uonje sukari we vipi
 
Alijifanya Asali,,, Vijana wakamuacha ajilambe...

Na siku hizi feminist wakileta kelele wanashonwa ndoige,,, akili inakaa sawa...


 
Back
Top Bottom