Ana Miaka 40, Hana Mtoto Wala Hana Mwanaume

Ana Miaka 40, Hana Mtoto Wala Hana Mwanaume

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,664
Reaction score
8,282
Yupo mwanamke mmoja anayejitambulisha kwa jina moja la Nekesa ambaye amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana akilalamika kwamba ana umri wa miaka 40 na bado hajapata mume wala mtoto.

Kwa mujibu wa video zake kwenye Tiktok, hafurahishwi na upweke unaomuandama kwa muda mrefu na kubainisha kuwa maisha yake hayaendi ipasavyo na anaelekea kukata tamaa.

Katika moja ya video hizo, Nekesa anaonekana akiwa amezama kwenye lindi la mawazo na kudai hana watoto ila anatumai kuwa ataolewa siku moja.

Nekesa anasema anamuomba mno Mwenyezi Mungu siku moja amjaalie mwanaume mmoja ambaye atampa huba lake lote.

“Miaka 40 sasa, sina watoto, mume au kuwa kwenye uhusiano wowote. Mungu wangu nisaidie,” Nekesa anaomba akionesha masikitiko yake.

Maelezo ya Nekesa yamewagusa wengi huku wakionesha kumpa matumaini kwamba siku moja atapata mume atakayempenda na kumpatia watoto.
 
Kizazi hiki wanawake tumekuwa wengi mnooo halafu wanaume wanaringa ile mbaya,
Inatuhuzunisha sana
Walio oa wanataka uwe mchepuko, single boy wanataka eat and run. Ndoa zimekuwa taflani usipo kaa mguu sawa unakuwa used kwa muda mfupi sana
 
Back
Top Bottom