An open letter to President Magufuli

An open letter to President Magufuli

Tokyo40, Mr president has good will with our nation, the Greatest obstacles his ruling party. Before doing those mentioned he must bring back Warioba constitution

Wewe umepunjwa nini na katiba iliyopo?
 
BARUA YA WAZI KWA MHESHIMIWA RAISI MAGUFULI

Ndugu Mheshimiwa Raisi Magufuli,


Kama Watanzania wengi, nakupongeza kwa kazi yako ya kuwafuata na kuwashughulikia ipasavyo wakwepaji kodi na wala rushwa serikalini.

Hata hivyo, ili kuwafanya Watanzania walipe kodi kwa hiari na kupunguza rushwa, inabidi mageuzi makubwa ya kiuchumi na YA kisiasa yafanyike na kutekelezwa haraka iwezakanavyo.

Napendekeza yafuatayo kwa serikali yako:

1. Punguza VAT iwe ASILIMIA 10
Upunguzaji wa VAT utasaidia na kuchochea uchumi kwa kufanya bei ya vitu rahisi kwa wananchi wenye uwezo mdogo.

2. Ondoa kodi ya mapato kwa wafanyazazi wenye mshahara wa chini ya milioni moja kwa mwezi na kwa wafanyabiashara wanaopata faida chini ya milioni nne kwa mwezi. Hii itawasaidia wananchi wa hali ya chini kuzidisha matumizi na kuwasaidia kulipa gharama kubwa ya maisha. Hii pia itawafanya wafanyabiashara wadogo kulipa kodi kitiifu zaidi bila ya kuumiza mitaji yao ya biashara, na pesa inayobaki wanaweza kuzidishia katika uwekezaji wao.

3. Punguza kodi kwa wafanyabiashara. Kodi kubwa bila ya kufanywa marekebisho kulingama ma hali ya uchumi wa nchi, ni sababu kubwa ya zaidi ya asilimia 99 ya wafanyabiashara kukwepa kodi. Hali ngumu ya maisha pia inawafanya wafanyakazi wa serikali kuomba rushwa ili walipe gharama za maisha. Kodi kubwa pia inawahamasisha wafanyabiashara kutoa rushwa ili kupunguza gharama za bidhaa zao, hasa wakati mgumu wa kibiashara.

4. Anzisha mageuzi katika sekta ya wafanyakazi wa serikali. Wachapa kazi walipwe zaidi na kupandishwa chea haraka. Wavivu wa kazi wafukuzwe kazi, wala rushwa wapelekwe mahakamani na kuadhibiwa kwa kifungo kirefu. Mishahara mikubwa kwa wafanyakazi wa serikali pia itasaidia kupunguza rushwa kwa kuwa watakuwa na uwezo wa kukabiliana na hali ngumu ya maisha.

5. Zidisha kiwango cha mshahara wa chini kifike 500,000 kwa mwezi. Watanzania wengi kwa sasa wanashindwa hata kula milo mitatu kwa siku, sembuse kulipa ada za shule na kodi ya nyumba kwa mshahara wa sasa. Kiwango hiki cha chini pia kiwe mshahara wa wafanyakazi wa nyumbani, ambao kwa miaka mingi wananyanyaswa kwa kutopewa mshahara wa kima cha chini.

6. Fanya mageuzi katika mfumo wa mahakama
Kuna vibaka wengi wapo jela zaidi ya miaka mitatu wanasubiri hukumu zao. Hawa ni Watanzania wasio na uwezo wa kutoa rushwa wala dhamana. Naomba uwatoe jela kwa kuwa makosa yao ni madogo madogo na wameshaadhibiwa vya kutosha jela. Kama adhabu, vibaka wapewe adhabu ya kusafisha nyumba na ofisi za serikali, kuokota taka mjini au wapewe adhabu nyingine. Pia, jela zimejaa wafungwa na nafasi ni ndogo mno. Wakipewa adhabu ya nje, itapunguza idadi kubwa ya wafungwa. Pia, wajengee vyoo vya kutosha. Ni aibu kwa taifa, kutofanya hivyo.

Mahakimu wasiruhusiwe kuhairisha kesi bila sababu maalumu. Kesi lazima zisikilizwe haraka ipasavyo na hukumu zitolewe haraka ili kukinga haki za wananchi. Mara nyingi kesi ndogo zinachukua hata miaka mitano.

Pia, tunaomba serikali iiheshimu na kufuata hukumu za mahakama na isiingilie kazi zake kama inavyosema katiba ya nchi. Mara nyingi serikali za awamu za nyuma zilidharau hukumu za mahakama. Hii inaipa sura mbaya nchi, siyo tabia ya kidemokrasia na haionyeshi kuwa nchi imekomaa kidemokrasia.

Kabla ya kuleta mahakama maalum za kuwahukumu wawekpa kodi, wala rushwa na mafisadi wengine, fanya mageusi kwanza. Ni tabu mno kwa mwananchi wa kawaida kupata haki yake mahakamani. Hukumu zinachukua mna mwingi kupita kiasi na mahakama zetu zinanuka rushwa. Siyo tu, mwananchi wa kawaida ananyimwa haki yake, pia, hali hii inawakata tamaa wawekezaji. Ni hasara kwa mfanyabiashara, kusubiri hukumu kwa muda usiojulikana kama kuna ugomvi wa kibiashara. Pesa za mtaji zinakwenda kutafuta haki, mwishowe watu wanafukuzwa kazi kupunguza gharama. Hasara hapa siyo ya mfanyabiashara peke yake, bali ya serikali kukosa kodi na ya mfanyakazi kukosa ajira.

7. Ruhusu wageni / watalii wa nchi nyingi zaidi waingie Tanzania kwa viza ya uwanja wa ndege. Hii itasaidia kuleta wageni zaidi bila ya kuomba viza katika ubalozi wetu. Serikali itapata fedha za kigeni zaidi na kuzalisha ajira zaidi.

8. Anzisha viza maalum kwa ajili ya wastaafu wa kitajiri. Wataleta pato la kigeni, ajira na kodi.

9. Ruhusu raia wa kigeni wenye kisomo cha juu kufanya kazi na kuishi Tanzania. Watoze ada. Hii italeta wasomi wenye elimu ambayo ipo pungufu au hamna kabisa Tanzania. Pia, italeta ajira na fedha za kigeni nchini.

10. Ruhusu uraia pacha.

11. Waelekeze maofisa wa posta wasitutoze kozi tukipokea mizigo kwa njia ya posta kama ni kwa ajili ya matumizi binafsi. (Chini ya thamani ya laki tatu). Toza ushuru mdogo kwa watumiaji wa posta ili wafanyabiashara wadogo wenye mtaji mdogo waweze kuagiza mali kutoka nje na kuuza kwa faida. Hii itaikuza biashara ya mitandao, itatoa ajira na kodi kwa serikali. Pia, wafanyabiashara wadogo hawatalazimika kutumia makontena ya gharama kubwa.

12. Wape moyo wazalishaji wa ndani kwa kuwatoza ushuru usioumiza biashara na faida na kwa kupunguza aina mbalimbali ya leseni na vibali na kodi tofauti tofauti. Warahisishie kazi kwa kuwapatia huduma zote sehemu moja, kama wanavyofanyiwa wawekezaji wa nje. Kodi isiwe ya kukomoana bali ya kujenga taifa na biashara za nyumbani.

13. Weka kodi kubwa kwa vitu visivyo na haja kubwa kwa jamii ili kukuza uchumi wa nyumbani na kusalimisha fedha za kigeni kutumiwa nje. Pia, vitu kama matunda ya Afrika Kusini au juisi, hatuvihitaji. Weka ushuru mkubwa ili wakulima wao waje kulima kwetu au Watanzania wale matunda ya nyumbani zaidi kusaidia wakulima wetu.

14. Kwa kuwa usafiri ni bado matatizo, Watanzania wengi wanategemea magari kwa usafiri. Kwa sasa, ushuru mkubwa unaotozwa na serikali unasaidia kuzidisha rushwa nchini. Ningependekeza ushuru wa gari uwe asilimia 25 kwa gari jipya na asilimia 35 kwa gari lililotumika sio zaidi ya miaka 10, kwa ukubwa wowote ya injini ya gari. Hii itawasaidia Watanzania wa hali ya kati wenye uwezo wa kununua gari kupata usafiri wa maana na serikali itaweza kuwatoza kodi ya barabara na ya usalama/ukaguzi wa gari kila mwaka.Hapa unaweza kutoza kodi kutokana na ukubwa wa injini na kuingiza kodi kati ya laki mbili mpaka milioni moja kwa kila gari, kila mwaka.

15. Ruhusu wananchi wa Zanzibar na Tanganyika wapige kura ya maoni ili wafanye maamuzi ya kutaka au kupinga umoja wetu. Nadhani wananchi wengi wanaupenda umoja na kura ya kutaka umoja itashinda. Lakini, hapa watakuwa wameombwa rasmi maoni yao kuhusu huu umoja. Tukirihusiw akupiga kura ya maoni, itaonyesha dunia kuwa tumekomaa kidemokrasia na tumetaka au tumekataa huu umoja wetu.


Mheshimiwa Raisi, nategemea mapendekezo yangu yatasaidia kidogo serikali yako. Nina uhakika watakuja wachangiaji wengine wa JF na kukupa mapendekezo yao pia. Tunachotaka sisi wananchi ni nchi iliyo na uchumi mzuri, imara, yenye nguvu na amani.

Nakutakia kila la kheri katika serikali yako.

Wako Mtiifu,

Tokyo40
Asante kwa kutafsiri, ila ndugu Tokyo40, na hii page uliyoitafsiri iweke kwenye hiyo page one, yaani iwe ktk page moja na hiyo ya kizungu, la sivyo hii page zikiwa nyingi itapotea!
 
Last edited by a moderator:
Yaani Kingereza chako ni kichanga saana, una point ila hujui kingereza sijui kwa nini hukuandika tuu kiswahili. Ni nani alikudanganya kuwa unafahamu kingereza? sijawahi kuona kingereza kibovu hivi duniani, umejaribu ila huna vocablary za kutosha kitu ambacho kimekufanya uafnye direct translations.
Wewe Bongani ni janga la taifa haswa!
 
Last edited by a moderator:
Comrade TOKYO40 congratulations for your good and well analysed "open letter".
I wish our Excellent Honourable President JPM and his staff will take it into consideration.
Thanx Comrade MTK and other members who have got a very +ve comments...let's pray for our fellow who deny each and everything.
My addition is on item # 2; especially for the civil servants who earn salary of 1m and above; I suggest to pay lower PAYE in contrast to the recent one.At least 5 to 6 % is enough.
 
How could he reform courts while it is the corrupt judge (Mr Lubuva) who brought him in power!!!

I wonder why some pro-ukawa dudes consciously choose to be ignorant? I still have no clue!
By the way, Lubuva is no longer an active judge!
 
Comrade TOKYO40 congratulations for your good and well analysed "open letter".
I wish our Excellent Honourable President JPM and his staff will take it into consideration.
Thanx Comrade MTK and other members who have got a very +ve comments...let's pray for our fellow who deny each and everything.
My addition is on item # 2; especially for the civil servants who earn salary of 1m and above; I suggest to pay lower PAYE in contrast to the recent one.At least 5 to 6 % is enough.
 
Safi sana naafiki mengi ila kuongeza tu hilo kuhusu magari naona wanaonunua magari yanayozidi cc 2000 yangetozwa zaidi, Leo dunia nzima inapigana kuwa na hewa safi.
Kuhusu suala la Visa nchi ambazo zina walakin kwa kuingiza madawa ya kulevya money laundering na uhalifu au kuvuruga amani ni lazima waombe visa toka ubalozi uliopo kwao.
Mungu ibariki Tanzania
 
Yaani Kingereza chako ni kichanga saana, una point ila hujui kingereza sijui kwa nini hukuandika tuu kiswahili. Ni nani alikudanganya kuwa unafahamu kingereza? sijawahi kuona kingereza kibovu hivi duniani, umejaribu ila huna vocablary za kutosha kitu ambacho kimekufanya uafnye direct translations.
Swala sio vocabulary hapo swala ni ujumbe you arrogant!, tunahitaji watu wenye udhubutu na kuchangia kwenye nchi yao. Respect kwako kamanda Tokyo40.
 
hajui kiingereza sasa si umepoteza muda wako kuandikagazeti

NAni ambaye hajui kiingereza? Hicho kiingereza hata aliyefika form 4 anaelewa sembuse mwenye PHD? Ushindwe na ulegee Fisadi we!
 
Dear Mr. President,

Like most Tanzanians, I applaud you for going after the tax evaders and corrupted government officials. It's about time.

However, to make Tanzanians more tax compliant and to reduce corruption, serious economic and political reforms must be implemented immediately.

I propose the following to your administration:

1. Reduce VAT to 10%.
This will stimulate the economy by making goods and services affordable to low income earners.

Mr. President, I hope my suggestions will be of some use to your administration. I am sure other JF contributors will come forward and give you more suggestion and proposals. All we want, is a strong, stable and prosperous country.

My very best wishes to your administration.

Sincerely,
Tokyo40
Mkuu asante kwa hii kitu, imetulia, ila kwenye hili la VAT iwe 10% itakuwa ngumu!, nadhani 10% itakuwa ni ndogo sana, kutosheleza kuendesha nchi, hata kama target ni volumes of collection vs per unit value, kwamba tukishusha watu wengi zaidi watalipa, hivyo serikali itakusanya zaidi kiliko hali ilivyo sasa, wengi wakijitahidi kukwepa!, ila bado sina uhakika kama kuna nchi yoyote duniani inatoza kiwango kidogo hivi cha kodi, ukiondoa nchi za petrodollars!, unless wachumi wamthibitishie Magufuli kuwa uchumi wa gesi has that capacity, mimi ningeshauri VAT iwe 15% , kwa sasa VAT kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ni 18% kwa nchi zote isipokuwa Kenya wao ni 16%.

Pasco
 
1. Punguza VAT iwe ASILIMIA 10

2. Ondoa kodi ya mapato kwa wafanyazazi wenye mshahara wa chini ya milioni moja kwa mwezi na kwa wafanyabiashara wanaopata faida chini ya milioni nne kwa mwezi.

3. Punguza kodi kwa wafanyabiashara. Kodi kubwa bila ya kufanywa marekebisho kulingama ma hali ya uchumi wa nchi, ni sababu kubwa ya zaidi ya asilimia 99 ya wafanyabiashara kukwepa kodi.

4. Anzisha mageuzi katika sekta ya wafanyakazi wa serikali. Wachapa kazi walipwe zaidi na kupandishwa cheo haraka. Wavivu wa kazi wafukuzwe kazi, wala rushwa wapelekwe mahakamani na kuadhibiwa kwa kifungo kirefu.

5. Zidisha kiwango cha mshahara wa chini kifike 500,000 kwa mwezi.

6. Fanya mageuzi katika mfumo wa mahakama
Kama adhabu, vibaka wapewe adhabu ya kusafisha nyumba na ofisi za serikali, kuokota taka mjini au wapewe adhabu nyingine.

Mahakimu wasiruhusiwe kuhairisha kesi bila sababu maalumu.

7. Ruhusu wageni / watalii wa nchi nyingi zaidi waingie Tanzania kwa viza ya uwanja wa ndege.
8. Anzisha viza maalum kwa ajili ya wastaafu wa kitajiri. Wataleta pato la kigeni, ajira na kodi.

9. Ruhusu raia wa kigeni wenye kisomo cha juu kufanya kazi na kuishi Tanzania. Watoze ada.

10. Ruhusu uraia pacha.

12. Wape moyo wazalishaji wa ndani kwa kuwatoza ushuru usioumiza biashara na faida na kwa kupunguza aina mbalimbali ya leseni na vibali na kodi tofauti tofauti. Warahisishie kazi kwa kuwapatia huduma zote sehemu moja, kama wanavyofanyiwa wawekezaji wa nje.

14. Kwa kuwa usafiri ni bado matatizo, Watanzania wengi wanategemea magari kwa usafiri. Kwa sasa, ushuru mkubwa unaotozwa na serikali unasaidia kuzidisha rushwa nchini. Ningependekeza ushuru wa gari uwe asilimia 25 kwa gari jipya na asilimia 3


Tokyo40, nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani, na naomba nichangie kwenye maeneo kadhaa.

No 1, Kiwango cha VAT kama sikosei ni sehemu ya makubaliano ya East African Community. So I don't think Tanzania can change that unilaterally.

No 2 & 3, Kabla ya kupunguza kodi (income tax & corporate tax), ningeshauru Serikali ifanye survey ill kujua kwa uhakika uwezo wa ulipaji kodi na namna (mechanism) bora ya kukusanya kodi. Tukumbuke Watanzania wengi wako kwenye 'informal sector' na wengi wao hawajaingizwa kwenye mfumo wa ukusanyaji kodi. Serikali inatakiwa kuwa na information (data) za uhakika kuhusu makundi yote ya watu wanaotakiwa kulipa kodi, ili kuweka kiwango kinachoendana na hali halisi kwa pande zote (serikali na mlipaji kodi).

No 4, nakubaliana na wewe.

No 5, nakubaliana na hoja ya kuongeza mishahara (sio kima cha chini tu), lakini naona hili linaendana na items No 2 & 3. Uwezo wa serikali kuengeza mishahara utategemea revenue collection, na ndio sababu ni muhimu sana kufanya survey ya taxation system yote.

No 6, I am with you 100%. Our justice system inahitaji reform, na wakati umefika sasa wa kuangalia alternative ways za kutumikia adhabu. Community services i.e. kufagia barabara, soko, etc.

No 7 & 8, ni kuhusu kuongeza watalii. Labda niseme hivi, kabla ya kuongeza watalii, serikali inatakiwa ijue (kwa uhakika) ina uwezo wa kuhudumia watalii wangapi? 1m, 2m, 3m or what? Hivi kwa mfano tukapata watalii 300,000 kwa mara moja na wote ni wanahitaji 5star hotel service, tuna uwezo huo? Nadhani serikali kwa kushirikiana na wadau wa utalii wakae chini na kuwa na mpango wa pamoja unaotekelezeka.

Na kuhusu utoaji viza airport nadhani bado ni busara lisiwe kwa kila nchi. Kuna nchi nyingine ni vyema mtu akapa visa huko huko kwa sababu za kiusalama. Tanzania tuna tatizo kubwa la border control, na hata ndani ya nchi bado vyombo vyetu ni weak kufuatilia makosa mengo. Bila ya kuwa mfumo imara kama ilivyo mfano
Malaysia, ni rahisi sana akaja mtu mhalifu kwa mgongo wa utalii na akatoka bila ya vyombo vyetu vya usalama kushtuka. Na hili limetokea mara nyingi sana tunasikia watuhumiwa wa ugaidi kwenye nchi nyingine kuwa waliwahi kuja Tanzania.

Pia umegusia special viza za wazee matajiri, again, hao wazee matajiri wako kwenye hali gani, nikimaanisha wanahitaji special care, na kama wanahitaji tumejipangaje? Tuna data zinazo-support hii proposal ya wazee matajiri?


No 9, Kabla ya kualika 'educated foreigners' ni vema kujua, kama Taifa tuna mapungufu wapi, fani gani, na kwa kiasi gani? Lakini pia hao 'educated foreigners' watakuja kwa utaratibu gani mfano, watatakiwa kufundisha Watanzania ili baada ya muda fulani Watanzania wawe na uwezo wa kufanya hizo kazi? Bado ninaamini solution ya matatizo ya Tanzania yapo ndani ya Tanzania hivyo tusijikite sana kwenye idea ya ku-import solutions.

No 10, uraia pacha. Ni maoni yangu kwamba kwa sasa Tanzania isijishughulishe na uraia pacha ila kuwepo na utaratibu wa kisheria wa kuwasaidia watu wenye asili ya Tanzania washiriki kwenye shughuli mbalimbali i.e. investment etc. Kuna sababu kadhaa, kwanza, with the exception ya Pemba, Tanzania haina tatizo la 'brain-drain'. Nchi kama Rwanda, kwa mfano, wana tatizo la wananchi wake wengi kuwa nje ya Rwanda kwa sababu migogoro ya ndani iliyowafanya kuwa wakimbizi kwenye nchi nyingine. Tanzania hatuna hiyo historia, watu wengi bado wako hapa hapa nchini. (Pemba ndiyo sehemu pekee yenye tatizo la watu hasa wataalam kukimbia Pemba).

Pili, mpaka sasa hakuna data zozote zinazoonesha kuwa Tanzania itapata kiasi gani au inakosa kiasi gani kwa sababu hakuna dual citizenship. Kumekuwepo na maongezi ya jumla kuwa nchi itafaidika i.e. investment, lakini hakuna specific data!

No 12, Nakubaliana na wewe kabisa. Mazingira ya biashara na hawa wafanyabiashara wadogo yanahitaji maboresho makubwa. It is unacceptable katika mazingira ya teknolojia kwa mtu kuanza kuzurura barabarani akifanya usajili wa kampuni, kulipa kodi au kutafuta leseni. Wakati umefika sasa kuwepo na dirisha moja tu ambapo mtu ukienda unapata majibu yote kuanzia TIN, Leseni, Penshen (i.e. NSSF, PPF, PSPF etc).

No 14, serikali isimamie uanzishwaji wa Mamlaka za usafiri kwenye miji na majiji. (Transport Authority). Sasa hivi mambo yanafanyika on ad-hoc basis.

Tujadiliane.


 
Mkuu YEHODAYA,

Ahsante kwa maoni yako.

Niya yangu siyo kumwonea Raisi Magufuli. Nadhani kama Raisi anafahamu matatizo ya wananchi, inakuwa rahisi kwake, kuomba bunge kubadilisha sheria. Wabunge wetu hawana historia kubwa ya kuleta mabadiliko haraka. Mabadiliko yanatoka kutoka serikalini na wao ni kupitisha au kupinga (kutoa shilingi). Nina imani kuwa Raisi akiwasomesha, watasomesheka. Ni kweli ulivyosema kuwa wabunge wengi hawafanyi kazi zao vizuri, ndiyo maana kazi ya mabadiliko lazima itoke IKULU.

Kuhusu kutoruhusu wananchi wa nchi za kimasikini ni kupoteza biashara kijinga. Kuna raia wengi wa nchi za Kiafriaka kama Nigeria ambao ni wafanyabiashara na ni "Middle Class". Utapeli na ujambazi sio tu unafanywa na raia wa nchi masikini. (soma Ponzi scheme ilipoanza na utapeli wa wall street wa kuuza junk bonds ). Naheshimu maoni yako, lakini kwangu ni ujinga kumrudisha mfanyabiashara au mtalii mwenye pesa za kutosha kufanya biashara au utalii eti tu kwa sababu ya wauza unga wa nchi yake. Kuna raia wengi Asia wa nchi za ulaya hasa Ujerumani na Uswisi, wanakamatwa kila siku Thailand na Cambodia wakiwashika kwa nguvu watoto wadogo (pedophiles). Kuan raia wa Australia wanakamatwa kila siku Indonesia wakiishi bila kibali. Hata leo ukienda Zanzibar utawakuta Waitaliano wanaishi bila kibali. Lakini hao raia wote wanaingia Tanzania bila shida yoyote lakini Mwafrika tajiri wa Nigeria anasumbuliwa. ni ujinga huu.

Kama unafikiri wasomi hawahitajiki Tanzania, kwa nini Kanada na Australia inapokea wasomi 200,000, Marekani wageni 1,000,000 kwa mwaka? Tanzania kuna vyuo vingi zaidi yao? Sijasema turuhusu kila msomi, ila msoni mwenye fani inayohitajika. Nisome vizuri. Pia, usiangalie fani peke yake, angalia kiasi cha fedha watazoingiza nchi. Kanada inaingiza US$2 bilioni kila mwaka kwa njia hii peke yake (YOUR ADDED VALUE), mbali ya kuwaruhusu wafanyabiashara matajiri. Karibu kila nchi zinazoona mbele wana program hii ya kuingiza pato kwa kutumia wasomi na matajiri. Zingine ukinunua nyumba ya $300,000 kama Panama, Spain, Greece, Bulgaria na Malta, unapewa viza ya kuishi mpaka kupata uraia ukipenda. Thailand ukiweka $25,000 benki, wanakupa visa ya kuishi., n.k.
 
Last edited by a moderator:
Kumlazimisha mzaliwa na Tanzania kuingia kwa viza kama mgeni ni ujinga.

Ningekuelewa kama Tanzania ni Norway au Japan ambapo raia haruhusiwi uraia wa nchi nyingine.

Kwa vyoyote, karibu Watanzania wote wanaoishi nje wamechukua uraia kwingine ile waweze kupata kazi nzuri, kusafiri bila kero la kuomba viza, kuomba scholarship, na maslahi mengine. Mpaka mwisho wa dunia, maslahi ya binadamu yanakuja mwanzo kuliko ya uzalendo. Binafsi sioni tatizo, mbingu hazitashuka majirani zetu waliporuhusu uraia pacha.
 
Mkuu Sungurampole,

Mimi kama mfanyabiashara, milioni nne kwa mwezi ni pato dogo kulilipia kodi. Badala ya kumpa serikali, ni bora liwekwe kwenye biashara kuzidisha mtaji wa biashara au kutumika katika mzunguko wa uchumi: kununua ardhi, gari, kulipa kodi ya shule na vitu madukani. Serikali itapata faida zaidi pesa hii ikizunguka kuliko kuikata kodi.

Kwa biashara ndodo ndogo, kutokana na kubanwa na TRA na red tape ya leseni chungumzima, wanalazimika kufanya hivyo ili waishi. Na makadirio katika biashara ni kitu cha kawaida wakati wa kulipa kodi. Wafanyabiashara wa kubanwa na kuangalia makadirio ya mapato yao ni wafanyabiashara wakubwa. Hii siyo Tanzania tu, bali nchi yoyote ile.
 
Last edited by a moderator:
Yaani Kingereza chako ni kichanga saana, una point ila hujui kingereza sijui kwa nini hukuandika tuu kiswahili. Ni nani alikudanganya kuwa unafahamu kingereza? sijawahi kuona kingereza kibovu hivi duniani, umejaribu ila huna vocablary za kutosha kitu ambacho kimekufanya uafnye direct translations.

Nigekua na mamlaka watu wa aina yako napiga risasi tu
 
Mkuu IROKOS,

Sidhani kama Mheshimiwa anapata muda mwingi wa kusoma email kwa sasa.

Lakini wanasiasa wengi wanapita JF, nina imani ujumbe utamfikia.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kwemanga2,

A country should ALWAYS follow policies that are in her best interest.

If financial computer simulations find it ideal that our economy will benefit from VAT reduction and/or other tax tariffs, then I say we should demand changes within the legal framework of the community. There are countries like the UK in the EU which refuse to follow some policies which are against their economic/political interests within the EU.
We can renegociate, if need be.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Betterhalfay,

Thank you for your kind support.

I am a firm believer in applying low tax brackets to salaried workers to a certain level. I think 5-6% should work for PAYE but maybe to a certain income bracket, let's say under 1.5 million a month. I think it is only fair that the more you make, the more you have to contribute to the country's development. We should always go for a progressive tax system.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom