An open letter to President Magufuli

An open letter to President Magufuli

Mkuu Blacksniper

katika nchi nyingi duniani, magari yenye CC kubwa yanatozwa kodi zaidi zikiwa barabarani. Ndio maana nikaandika serikali inaweza baadae kupata kodi zaidi kwa kuwatoza road/city tax na pollution sticker (road worthy tax). Kwa mfano, Japan gari si ghali jipya, lakini nalipa $1600 kila mwaka kama kodi ya barabara na ya kupima gari halitoi uchafu zaidi ya kipimo kilichoruhusiwa. Mpaka sasa, serikali imeshaingiza karibu $10,000 kwa kodi tu.

Kutoza ushuri na kodi kubwa kwa mwananchi wa nchi masikini ni kupunguza kasi ya maendeleo na kuzidisha hali ya kuomba/kutoa rushwa.

Kuhusu wahalifu, wapo katika kila nchi, masikini na tajiri. Thailand na Indonesia, wauza unga wengi wanakamatwa wakitokea China na Taiwan. Indonesia, hao pia wanawatapeli watu katika mtandao. Lakini raia wao wote wanaingia nchi hizo bila ya kizuizi. Wachina na WaTaiwan pia wanapewa viza uwanja wa ndege wa Narita, Japan. Wauza unga wawili walionyongwa juzi juzi huko Indonesia walitokea Australia.

Kama tunataka kukuza utalii, lazima turuhusu wageni wa nchi nyingine waingie kirahisi. Hatuna ubalozi nchi nyingi kwa vyovote. Tanzania ina mbuga 16, Bahari ya Hindi na Mlima Kilimanjaro, lakini haipati kata watalii milioni mbili kwa mwaka. Bali, kisiwa cha Indonesia, ni sawa tu na Zanzibar, na kinapata watalii milioni 10.

Kuhusu money laundering, wahalifu wakubwa ni raia wa nchi zilizoendelea. Benki za Uswisi, kwa mfano, zimepigwa faini zaidi ya $2 billioni na serikali ya Marekani kwa kuficha pesa za matajiri wao kuepuka kodi. Kuna wengine mpaka wanaukana uraia wao ili waepuke jela.
 
Naona matumaini ya watanzania yakianza kukua taratibu. Muda wa mabadiliko hakika umefika.
 
dear mr. President,

like most tanzanians, i applaud you for going after the tax evaders and corrupted government officials. It's about time.

However, to make tanzanians more tax compliant and to reduce corruption, serious economic and political reforms must be implemented immediately.

I propose the following to your administration:

1. Reduce vat to 10%.
This will stimulate the economy by making goods and services affordable to low income earners.

2. Eliminate income tax for income below 1 million shillings a month for salaried workers and 4 million for traders.
This will increase spending power for poor consumers and help them afford to pay their bills. It will also make small traders more willing to pay taxes without reducing their capital. They can also be able to invest more in their businesses if they have extra income.

3. Reduce income tax for businesses. High taxes, without fine-tuning the rates in times of economic slowdow/crisis is one of the reasons why 99% of businesses cheat the government of tax revenue. Economic hardship encourage civil servants to take bribes to pay for the high cost of living. It also encourage businesspeople to give bribe to make their products more competitive.

4. Introduce civil service reforms. Productive civil servants should be paid more and promoted accordingly. Incompetent ones should be fired and corrupt ones should serve long prison sentences. The civil servants should not expect "life employment" if they are not competent. Competitive wages to the civil servants will also discourage corruption.

5. Increase the minimum wage to at least 500,000 a month. Most tanzanians cannot eat 3 meals a day, let alone send their children to a good school with the current wages. This wage should also cover domestic workers. They have long suffered from minimum wage exclusion.

6. Reform the court sysyem.
Too many poor tanzanians are spending years behind prison for petty crimes. Please set people free if they have served over 3 years waiting for their cases to be heard. The judges should send them to clean government buildings, clear trash in the city or do something more productive instead. It will also reduce prison congestion. Prison facilities should also be improved. It is a real shame, in this day and age, not to provide enough toilets to prisoners.

Judges should be not allowed to take a leave of absence for whatever reason other than health. Cases must be heard and judgement given in a reasonable time. It should not take 5 years to conclude a simple case.

The judiciary must be, at all times, feel, look and function independent of government pressure/interference. Even though our constitution stipulates that independence, in reality, the government often ignores it if the courts makes decisions not in her favour. Tanzanians would like to see the government respect court decisions. This will show the world our maturity as a democratic nation.

Before you introduce special courts to deal with corrupted civil servants and tax evaders, reform the current system first. It is impossible at the moment to seek justice in the court of law. It is not only time consuming but the system is heavily corrupted. Not only do average citizens are denied justice, it also discourages investors' confidence. It takes too long to settle business disputes.

7. Let more foreign nationals get visas on arrival. This will encourage more tourists to come to tanzania hassle free.

8. Introduce a special visa for rich retirees. This will increase foreign revenue, employment and taxes.

9. Allow highly educated foreigners to work/immigrate to tanzania for a fee. They will bring in much needed skills which are in short supply and capital. They will ask create employment.

10. Legalize dual citizenship.

11. Direct the postal service administrators not to tax packaged goods meant for personal use (under 300, 000 value).
Impose lower taxes for imports through the postal services to encourage internet businesses to flourish. This will make it possible for small traders to afford starting a business with little capital. They can import without filling a container.

12. Encourage domestic manufacturers to invest with confidence by introducing competitive tax rates and by reducing red tape. They should be able to get all the necessary permits and licenses faster and cheaper under one roof.

13. Discourage luxurious imports by imposing higher taxes on them.

14. Since transportation network is still poor, many people depend on their cars for transportation. Currently, unrealistic tax rates just encourage corruption to take place. I suggest lowering car import tax to 25% for brand new cars regardless of engine capacity and 35% for used cars under 10 years old. This will let more tanzanians afford to import more cars. You can then charge them more for road tax and make them pay for road worthy sticker as well. You can easily get 200,000 -1,000,000 per car, per year, depending on the engine size, for the duration of the car's usage.

15. Allow the people of zanzabar and tanganyika to choose their future destiny. I believe majority of tanzanians believe in the union. However, we were not consulted. I believe the people are now mature enough to decide on their fate through a referendum. It is the right way, the democratic way to seek our consent.

Mr. President, i hope my suggestions will be of some use to your administration. I am sure other jf contributors will come forward and give you more suggestion and proposals. All we want, is a strong, stable and prosperous country.

My very best wishes to your administration.

Sincerely,
tokyo40


**********************************************************************************************************



barua ya wazi kwa mheshimiwa raisi magufuli

ndugu mheshimiwa raisi magufuli,


kama watanzania wengi, nakupongeza kwa kazi yako ya kuwafuata na kuwashughulikia ipasavyo wakwepaji kodi na wala rushwa serikalini.

hata hivyo, ili kuwafanya watanzania walipe kodi kwa hiari na kupunguza rushwa, inabidi mageuzi makubwa ya kiuchumi na ya kisiasa yafanyike na kutekelezwa haraka iwezakanavyo.

napendekeza yafuatayo kwa serikali yako:

1. Punguza vat iwe asilimia 10
upunguzaji wa vat utasaidia na kuchochea uchumi kwa kufanya bei ya vitu rahisi kwa wananchi wenye uwezo mdogo.

2. ondoa kodi ya mapato kwa wafanyazazi wenye mshahara wa chini ya milioni moja kwa mwezi na kwa wafanyabiashara wanaopata faida chini ya milioni nne kwa mwezi. Hii itawasaidia wananchi wa hali ya chini kuzidisha matumizi na kuwasaidia kulipa gharama kubwa ya maisha. Hii pia itawafanya wafanyabiashara wadogo kulipa kodi kitiifu zaidi bila ya kuumiza mitaji yao ya biashara, na pesa inayobaki wanaweza kuzidishia katika uwekezaji wao.

3. punguza kodi kwa wafanyabiashara. Kodi kubwa bila ya kufanywa marekebisho kulingama ma hali ya uchumi wa nchi, ni sababu kubwa ya zaidi ya asilimia 99 ya wafanyabiashara kukwepa kodi. Hali ngumu ya maisha pia inawafanya wafanyakazi wa serikali kuomba rushwa ili walipe gharama za maisha. Kodi kubwa pia inawahamasisha wafanyabiashara kutoa rushwa ili kupunguza gharama za bidhaa zao, hasa wakati mgumu wa kibiashara.

4. anzisha mageuzi katika sekta ya wafanyakazi wa serikali. Wachapa kazi walipwe zaidi na kupandishwa chea haraka. Wavivu wa kazi wafukuzwe kazi, wala rushwa wapelekwe mahakamani na kuadhibiwa kwa kifungo kirefu. Mishahara mikubwa kwa wafanyakazi wa serikali pia itasaidia kupunguza rushwa kwa kuwa watakuwa na uwezo wa kukabiliana na hali ngumu ya maisha.

5. zidisha kiwango cha mshahara wa chini kifike 500,000 kwa mwezi. Watanzania wengi kwa sasa wanashindwa hata kula milo mitatu kwa siku, sembuse kulipa ada za shule na kodi ya nyumba kwa mshahara wa sasa. Kiwango hiki cha chini pia kiwe mshahara wa wafanyakazi wa nyumbani, ambao kwa miaka mingi wananyanyaswa kwa kutopewa mshahara wa kima cha chini.

6. fanya mageuzi katika mfumo wa mahakama
kuna vibaka wengi wapo jela zaidi ya miaka mitatu wanasubiri hukumu zao. Hawa ni watanzania wasio na uwezo wa kutoa rushwa wala dhamana. Naomba uwatoe jela kwa kuwa makosa yao ni madogo madogo na wameshaadhibiwa vya kutosha jela. Kama adhabu, vibaka wapewe adhabu ya kusafisha nyumba na ofisi za serikali, kuokota taka mjini au wapewe adhabu nyingine. Pia, jela zimejaa wafungwa na nafasi ni ndogo mno. Wakipewa adhabu ya nje, itapunguza idadi kubwa ya wafungwa. Pia, wajengee vyoo vya kutosha. Ni aibu kwa taifa, kutofanya hivyo.

mahakimu wasiruhusiwe kuhairisha kesi bila sababu maalumu. Kesi lazima zisikilizwe haraka ipasavyo na hukumu zitolewe haraka ili kukinga haki za wananchi. Mara nyingi kesi ndogo zinachukua hata miaka mitano.

pia, tunaomba serikali iiheshimu na kufuata hukumu za mahakama na isiingilie kazi zake kama inavyosema katiba ya nchi. Mara nyingi serikali za awamu za nyuma zilidharau hukumu za mahakama. Hii inaipa sura mbaya nchi, siyo tabia ya kidemokrasia na haionyeshi kuwa nchi imekomaa kidemokrasia.

kabla ya kuleta mahakama maalum za kuwahukumu wawekpa kodi, wala rushwa na mafisadi wengine, fanya mageusi kwanza. Ni tabu mno kwa mwananchi wa kawaida kupata haki yake mahakamani. Hukumu zinachukua mna mwingi kupita kiasi na mahakama zetu zinanuka rushwa. Siyo tu, mwananchi wa kawaida ananyimwa haki yake, pia, hali hii inawakata tamaa wawekezaji. Ni hasara kwa mfanyabiashara, kusubiri hukumu kwa muda usiojulikana kama kuna ugomvi wa kibiashara. Pesa za mtaji zinakwenda kutafuta haki, mwishowe watu wanafukuzwa kazi kupunguza gharama. Hasara hapa siyo ya mfanyabiashara peke yake, bali ya serikali kukosa kodi na ya mfanyakazi kukosa ajira.

7. ruhusu wageni / watalii wa nchi nyingi zaidi waingie tanzania kwa viza ya uwanja wa ndege. Hii itasaidia kuleta wageni zaidi bila ya kuomba viza katika ubalozi wetu. Serikali itapata fedha za kigeni zaidi na kuzalisha ajira zaidi.

8. anzisha viza maalum kwa ajili ya wastaafu wa kitajiri. Wataleta pato la kigeni, ajira na kodi.

9. ruhusu raia wa kigeni wenye kisomo cha juu kufanya kazi na kuishi tanzania. Watoze ada. Hii italeta wasomi wenye elimu ambayo ipo pungufu au hamna kabisa tanzania. Pia, italeta ajira na fedha za kigeni nchini.

10. Ruhusu uraia pacha.

11. waelekeze maofisa wa posta wasitutoze kozi tukipokea mizigo kwa njia ya posta kama ni kwa ajili ya matumizi binafsi. (chini ya thamani ya laki tatu). Toza ushuru mdogo kwa watumiaji wa posta ili wafanyabiashara wadogo wenye mtaji mdogo waweze kuagiza mali kutoka nje na kuuza kwa faida. Hii itaikuza biashara ya mitandao, itatoa ajira na kodi kwa serikali. Pia, wafanyabiashara wadogo hawatalazimika kutumia makontena ya gharama kubwa.

12. wape moyo wazalishaji wa ndani kwa kuwatoza ushuru usioumiza biashara na faida na kwa kupunguza aina mbalimbali ya leseni na vibali na kodi tofauti tofauti. Warahisishie kazi kwa kuwapatia huduma zote sehemu moja, kama wanavyofanyiwa wawekezaji wa nje. Kodi isiwe ya kukomoana bali ya kujenga taifa na biashara za nyumbani.

13. weka kodi kubwa kwa vitu visivyo na haja kubwa kwa jamii ili kukuza uchumi wa nyumbani na kusalimisha fedha za kigeni kutumiwa nje. Pia, vitu kama matunda ya afrika kusini au juisi, hatuvihitaji. Weka ushuru mkubwa ili wakulima wao waje kulima kwetu au watanzania wale matunda ya nyumbani zaidi kusaidia wakulima wetu.

14. kwa kuwa usafiri ni bado matatizo, watanzania wengi wanategemea magari kwa usafiri. Kwa sasa, ushuru mkubwa unaotozwa na serikali unasaidia kuzidisha rushwa nchini. Ningependekeza ushuru wa gari uwe asilimia 25 kwa gari jipya na asilimia 35 kwa gari lililotumika sio zaidi ya miaka 10, kwa ukubwa wowote ya injini ya gari. Hii itawasaidia watanzania wa hali ya kati wenye uwezo wa kununua gari kupata usafiri wa maana na serikali itaweza kuwatoza kodi ya barabara na ya usalama/ukaguzi wa gari kila mwaka.hapa unaweza kutoza kodi kutokana na ukubwa wa injini na kuingiza kodi kati ya laki mbili mpaka milioni moja kwa kila gari, kila mwaka.

15. ruhusu wananchi wa zanzibar na tanganyika wapige kura ya maoni ili wafanye maamuzi ya kutaka au kupinga umoja wetu. Nadhani wananchi wengi wanaupenda umoja na kura ya kutaka umoja itashinda. Lakini, hapa watakuwa wameombwa rasmi maoni yao kuhusu huu umoja. Tukirihusiw akupiga kura ya maoni, itaonyesha dunia kuwa tumekomaa kidemokrasia na tumetaka au tumekataa huu umoja wetu.


mheshimiwa raisi, nategemea mapendekezo yangu yatasaidia kidogo serikali yako. Nina uhakika watakuja wachangiaji wengine wa jf na kukupa mapendekezo yao pia. Tunachotaka sisi wananchi ni nchi iliyo na uchumi mzuri, imara, yenye nguvu na amani.

nakutakia kila la kheri katika serikali yako.

Wako mtiifu,

tokyo40

jamani kasharekebisha kiswahili naombeni msome tena mtaona vyema marekebisho... Comorade umeongea mambo ya msingi sana tunaamini habari zitamfikia mhe. Rais magufuli ... Tanzania nchi yangu naipenda na jf i love you.. ...
 
Ni hoja ya mwaka kudos. Ila uruhusu pia mbinu za kidicteta zitumike maana utatikisa nchi na wenye nchi sisi wananchi ndilo tunaliombea
 
NAni ambaye hajui kiingereza? Hicho kiingereza hata aliyefika form 4 anaelewa sembuse mwenye PHD? Ushindwe na ulegee Fisadi we!

Yeye anayejua kiingereza mbona amecomment kwa kiswahili???
 
Ni ushauri mzuri sana. Big up tokyo40. Naomba washauri wa mh. Jpm ambao wanapitia humu mpelekee huu waraka tafadhali.
 
Mkuu Pasco,

Ahsante kwa maoni yako.

Naamini kuwa Watanzania watanufaika na kodi ndogo ya VAT ya 10% zaidi kuliko ya sasa ya 18%. Hii pesa itazunguka katika uchumi kununua ardhi, kukodi nyumba, kulipa ada za shule, kutoa ajira na kadhalika. Ina multiplying effect.

Kwanza, tusijali EAC, lazima tutafute maslahi ya wananchi wa Tanzania kwanza. Kama hawezi kupunguza VAT, inabidi awasaidie vingine kama kuwajengea nyumba kwa bei nafuu au kutowatoza kodi kubwa katika mishahara yao na kuongeza mishahara yao ya kima cha chini. They deserve it!

Serikali zote za nyuma zimeonyesha kutumia pesa ya walipa kodi hovyo. Watanzania wanataka mabadiliko katika maisha yao. Kodi wanayotozwa na serikali ni kubwa mno, na huko vijijini watu wanashindwa maisha kabisa huku wabunge wanapokea mishahara na posho za ajabu ajabu.

Ingekuwa kama pesa inatumiwa vizuri, nadhani wananchi wengi wangeridhika na kujifunga mikanda. Lakini mpaka Raisi Magufuli anaingia Ikulu, wagomjwa bado wanalala sakafuni, dawa hamna wala kitanda. hapo hapo, waziri anakwenda ubalozi wa Japan na Land Cruiser VX na kuomba gari la wagonjwa! Haingii kwenye akili!

Juzi nilikuwa naongea na meneja wa kampuni ya Kijapani. Alikwenda kwenye maonyesho ya sabasaba na alishangaa sana, jinsi vitu vilivyokuwa ghali Tanzania. Na kumbuke, yeye ni Mjapani. Nilipokuwa naishi Tanzania, gharama ya umeme na maisha yalikuwa makubwa kuliko ya hapa Japan. Fikiri wananchi wa hali ya chini wanavyoishi.
 
Ahsante kwa maoni yako, Mkuu FJM.

Nimekuelewa kabisa kuhusu informal sector. Ni muhimu sana serikali ijue hapo. Wasomi wetu sijui wanasubiri nini. Kuna software nyingi tu zinatumika katika wizara za fedha ulimwenguni kupata haya majibu haraka (computer simulations for income tax management).

Kuhusu EAC, tunaweza kubadilisha makubaliano, kama hayana maslahi kwa taifa.

Kuhusu watalii, siyo wote wana uwezo wa kulipa 5 star hotel. Na siyo wote wanataka kuja DSM. Nina imani kuwa kama kutaongezaka watalii, mahoteli yatajengwa na Watanzania na wageni. Hata wananchi wanaweza kukodisha vyumba vyao kwa kutumia mitandao kutafuta wateja. Tatizo ni kuwa hamna mawasiliano baina ya serikali na wafanyabiashara mbalimbali kama unavyosema.

Nakubaliana na wewe kuhusu usalama wa nchi, lakini hatuwezi kusubiri bila ya kufanya kitu. Mahoteli India na Indonesia wanapeleka majina ya wageni polisi kila siku. Mgeni anapigwa picha na kutoa fingerprint. Nadhani hapa itasaidia kuanza kazi huku security database inatengenezwa na kuboreshwa. Pia, nadhani, tusifikirie sana kuwa watalii WOTE wana malengo mabaya. Intelligence cooperation is the key.

Kuhusu mstaafu ninayotaka akaribishwe, ni yule mwenye pensheni yake isoyopungua $2000 kwa mwezi. Hahitaji gharama yoyote kutoka kwa mlipa kodi. Ananunua nyumba yake au anakodisha, anatoa ajira, ananunua vitu madukani na kukuza uchumi. Akiumwa anajilipia mwenyewe. siku hizi insurance zipo za kujitibu nchi yoyote duniani. Wapo laki mbili Asia, watu kama hawa.

Kuhusu wasomi wa nje, naamini watasaidia sana Watanzania kufungua macho. Tunahitaji exposure zaidi. Naongelea wasomi wenye fani za biashara za kimataifa, lugha za kigeni, tiba n.k. Hatuwezi kuwapangia muda wa kukaa, kameleta pesa, wamelipa ada ya viza ya kuishi, waruhusiwe kuishi. Mbona Watanzania wanakaribishwa kuishi Australia, Kanada, Marekani na nchi nyingine? Mbona Kanada na Marekani ina vyuo vingi, lakini bado inakaribisha wasomi? hii ni biashara kubwa nchi nyingi sana duniani.

Kuhusu uraia pacha, naamini in the long run, its inevitable. Tutakataa leo, lakini kesho itakubalika. Its a matter of time. sikubaliani na wewe kuhusu brain-power. Madaktari wengi na manesi wanakimbilia Botswana kufanya kazi. Kama tungekuwa na wasomi wa fani nyingi, ungeona viwanda vya kila aina vimejengwa na hali ya afya ya Mtanzania imeboreshwa, etc.

Thanks.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hili kwanza kabisa aachane na sera ya chama chake ya serikali Mbili-hili halitadumu kwa namna yoyote.

Hivyo basi akae na Wazanzibar wakubali Mfumo wa Serikali Mmoja!. Namna Bora ya kuwezesha hili wachukue sera ya CDM ya Majimbo.Na amini hili litaendelea kulinda masilahi na hadhi ya wazanzibar kama walivyo sasa na liingizwe kwenye Katiba.



15. Ruhusu wananchi wa Zanzibar na Tanganyika wapige kura ya maoni ili wafanye maamuzi ya kutaka au kupinga umoja wetu. Nadhani wananchi wengi wanaupenda umoja na kura ya kutaka umoja itashinda. Lakini, hapa watakuwa wameombwa rasmi maoni yao kuhusu huu umoja. Tukirihusiw akupiga kura ya maoni, itaonyesha dunia kuwa tumekomaa kidemokrasia na tumetaka au tumekataa huu umoja wetu.



Hili nimelipenda kuliko maelezo!
Tena hata kabla hajafikisha mwaka wa Pili zoezi hili angehakikisha linaanza kufanikiwa.
Kuna Taasisi ambazo kusema kweli ajira zake zilifaa ziwe za Miakataba max-2yrs. Mfano.TPA,TRA yako mashirika mengi hakuna haja ya ajira ya kudumu-na mbaya zaidi zingine ni Executive agency na zinajipangia namna ya kulipana.



4. Anzisha mageuzi katika sekta ya wafanyakazi wa serikali. Wachapa kazi walipwe zaidi na kupandishwa chea haraka. Wavivu wa kazi wafukuzwe kazi, wala rushwa wapelekwe mahakamani na kuadhibiwa kwa kifungo kirefu. Mishahara mikubwa kwa wafanyakazi wa serikali pia itasaidia kupunguza rushwa kwa kuwa watakuwa na uwezo wa kukabiliana na hali ngumu ya maisha.
 
It is among very few constructive debates moving in Jf nowadays. I beg to differ with you in no 10. For the moment dual citizenship will cause more problems. Thank you for your critca remarks.
 
LMAO!!!!

Mkuu Movado, umenikumbusha mbali na ile ganja ya Arusha! Ujana Bana!
 
Last edited by a moderator:
Thank you Mkuu Hwasha.

I respect your point of view.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mp Kalix2

Thanks for your views.

Hata mimi nashangaa serikali haina wafanyakazi wa contract fupi kupunguza gharama. Kwenye sekta binafsi, contract ya mwaka mmoja mmoja ndiyo ipo zaidi.

Kwa kweli, mageuzi ya kufanywa ni mengi sana mpaka hii nchi ikae vizuri kiuchumi na kisiasa.
 
Last edited by a moderator:
Jamani JPM Mpelekee barua in shorthand .as ha sema yeye si mtu wa maongezi kazi tuuu
 
mkuu umenigusa kidogo kwenye chakula cha halal. sijawahi fika huko asia lakini ulaya na marekani halal food sio ishu tena siku hizi. ila sikujua kama huko japan kuna hilo tatizo hata hivyo. lakini hata hivyo kadiri siko zinavyozidi kusonga halal food itakuwa sio ishu tena popote pale duniani kwa sehemu kubwa.

Mkuu Abunuas,

Siyo raia wote wanaweza kupata visa uwanja wa ndege. Miaka mingi tunawabagua kwa mfano raia wa Afrika na kuwapendepea raia wa ulaya. Hatuangalii nani ni tajiri au masikini. Tuwe kama Malaysia. Hawajali umetoka wapi, ili mradi una fedha za kutosha, raia wa zaidi ya nchi 160 wanapewa visa uwanja wa ndege. Mwaka huu, Indonesia imefuata. Japan mwaka jana, kwa mara ya kwanza, imeruhuhusu raia wa nchi za kimasikini za Asia kupata visa uwanja wa ndege. Leo maduka yao yamejaa watalii wa China. Leo naweza kula chakula cha HALAL mjini Tokyo, nashukuru watalii wa Indonesia na Malaysia, waliolazimisha huduma hii.
 
Back
Top Bottom