An-Anuur - Hauna imani na Barzla la Mitihani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

An-Anuur - Hauna imani na Barzla la Mitihani

Discussion in 'Jamii Photos' started by Candid Scope, May 26, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Tuwasaidieje hawa ndugu zetu, watanzania wenzetu na ndugu zetu kuhusu ukweli wa kufanya vizuri katika mitihani yao?
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Na waha waislamu waliosoma na kufaulu kwa kutumia majina yao halisi walipitaje pitaje kwenye system hiyo wanayoipiga vita? Ukiona mtu analeta sababu sababu kama hizi jua hana la kusema na kusema ameshazoea...hawa ndio wanaotaka kubomoa nchi. Serikali isikae kimya maana ifike mahala sasa tuhuma kama hizi ziwe zinaletwa na uthibitisho na sio maneno maneno tu.
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ukishajua an-nur linamilikiwa na na nani hutapata shida,,,,,nimeshaeleza kwenye thread ilotoka blog ya mjengwa
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  hahahahaaaaaaa,,,,hapo ndipo napojiuliza,,,binafsi huwa nawaambia ukweli tu waislam wenzangu,hata tuwapo miskitini huwa nawaambia ukweli,,,,TUSIWAHADAE WATOTO KUWA WANAONEWA,,,,,,WATASHINDWA KUSOMA,,,,TUJENGE MISINGI YA KUWAFANYA WAPENDE KUSOMA NA WAJUE KWANIN WANASOMA,HAPO TUTAFANIKIWA
   
 5. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Wananikera sana hawa ndugu zetu wenye kuamini hivyo, ni dhana potofu sana na yenye kuwavunja watu moyo. Mtoto kwa kiislamu ambaye yuko darasa la tatu leo hakika hawezi kuendelea kusoma.
   
 6. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hatuhitaji Msaada wowote kutoka kwenu, ni sisi wenyewe Waislam tuanze mchakato wa kujikwamua kutoka kwa Mafisadi wa Bakwata. Ufikie muda wa sisi wenyewe waislamu tuamue kuwa tunahitaji viongozi wenye muelewo wa mambo, wasomi na wenye nia ya kuleta Maendeleo kwa waislam na Taifa kwa Ujumla.

  Kwa sasa hatuhitaji Msaada wowote kutoka sehemu yoyote zaidi ya kuanza mchakato wa kuwatimua hawa Wazee Mafisadi wa Bakwata waliokalia Unafiki na Majungu ya kudidimiza Uislam kwa manufaa yao kama Ndugu zao CCM.

  Siamini kama tunafeli kwa ajili ya Uislam, bali tunafelishwa na system ya Bakwata iliyojaa Mafisadi kwa kisingizio cha Waislam tunaonewa wakati tatizo lipo kwa Viongozi zimejaa Ufisadi Kama Kampuni ya CCM.


   
 7. Edoedward1

  Edoedward1 JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 799
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 60
  za kidini me simooo,.
   
 8. k

  kihami Member

  #8
  May 26, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shauri yenu kama hamuweki bidi kusoma. Mutabaki kuwa boko haramu
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ndugu zangu na watanzania wenzangu tujaribu kuangalia tatizo la kufaulu au kushindwa wanafunzi katika shule na walimu pamoja na mfumo wa maisha ya wanafunzi wawapo shuleni kama unaakisi ufundishiki au ushiriki tu shuleni waliko. Wanaoleta mada hiyo wajaribu kuwasiliana na waumini wa dini hiyo walio wasomi nadhani watasaidia zaidi kutoa mwanga wa kutatua tatizo katika shule zenyewe badala ya kumnyooshea kidole fulani wakati walimu, taasisi ya elimu, watunzi wa mitihani na wasahihishaji wa mitihani ni mfumo shirikishi wa Watanzania wote.
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Je, mkazo wa ufundishaji shule ni masomo yakufaulisha wanafunzi au ni mchanganyiko wa mambo mengi na huenda kuna yenye mkazo zaidi kuliko yale ya kufaulisha. Hapa kinachaotakiwa ni balance ya kufundisha wanafunzi darasani, nidhamu ya masomo yote darasani husaidia hata nidhamu ya maisha ya kawaida ni kiroho.
   
 11. Bufa

  Bufa JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 4,168
  Likes Received: 3,375
  Trophy Points: 280
  Sasa naona udini unataja kuingia Tz, ni viongozi wangapi waislaam? kuanzia raisi hadi mawaziri wengi ni waislaam wao walifikaje huko? kama watu wanafeli ni kwamba hawana akili au hawakufanya jitihada sio kusema system imejaa waislaamu. wazanzibar wao wamekataa elimu sasa watasaidiwaje hata kama baraza zima litakua ni la waislaamu wazenji hawabebeki, mnataka watu wapewe vyeti hata kama wameurunda.
   
 12. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,062
  Trophy Points: 280


  .........................
  Ukweli umekuweka huru..........!!  .......


  Endelea hivyohivyo.....
   
 13. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hivi watu wengine mnajua mnachokiandika?
  kuna binadamu ambaye hana akili?
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tunahitaji kuchangia maoni kuwasaidia watanzania wenzetu, na papo ni ndugu zetu kwani kazi ya kupata maana kamili ya kuelewa nini kinaendelea mashuleni na matokeo ya mitihani ni sisi wenyewe na wala si kulinyooshea kidole Barala la Mitihani.

  Mfumo wa elimu ni wizara ya Elimu ambayo imeoa uhuru kwa baadhi ya mashirika na watu binafsi kuwa na shule, vyuo na wakufunzi ambao wanatambulika kwa vigezo vilivyowekwa. Lakini kama tutaweka wakufunzi ambao ni ridhio la moyo badala ya stahiki kwa taaluma inayotakiwa malalamiko haya hayataisha kwani tunatazama matokeo bila kuangalia kiini.

  Ningewashauri wahariri wa gazeti hilo wajaribu kwenda kwenye shule ambazo wanaona zimeonewa katika matokeo ya mitihani wafanye utafiri wa mazingira ya wanafuzi, wakufunzi na mkazo wa elimu katika shule hizo, bila shaka wataridhia kutoa jibu tofauti na walichokiandika gazetini.
   
Loading...