Amwaga fedha kumpoza msichana wake wa kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amwaga fedha kumpoza msichana wake wa kazi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jul 25, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Amwaga fedha kumpoza msichana wake wa kazi[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #e1e1e1"]
  [TD]
  [​IMG]
  [/TD]
  [TD]Monday, July 04, 2011 10:59 AM
  BAADA kutoweka nyumbani kwake kwa takribani siku nne kukimbia dhahama aliyemsababishia msichana wake wa kazi imedaiwa bosi huyo amekwenda kumuangukia dada wa msichana wake na kumwagia fedha ili waweze kuyamaliza kimnya kimnya.

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Mwanamdke huyo aliyetambulika kwa jina la Mama Mudy alimsababisha kubakwa kwa msichana wake wa kazi za ndani aitwae Grace [17] baada ya kumfukuza usiku kwa sababu ya kuchelewa kurudi katika ajira yake hiyo

  Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo alitoroka usiku huo kwa kuogopa mahojiano kati yake na polisi na kutoweka nyumbani kwake hapo kwa takribani siku nne mfululizo

  Hata hivyo imedaiwa kuwa mwanamke huyo alitinga nyumbani kwa dada huyo kwa lengo la kutaka kuyamaliza kiundugu na kukiri kosa hilo na kuahidi kumsaidia msichana huyo na kumtaka dada huyo kutaja kiasi cha fedha anachokihitaji ili aweze kuyamaliza

  Hata hivyo imediwa kuwa dada binti huyo hakuhitaji fedha hizo na kuhofia afya ya mdogo wake huyo na bosi huyo kukiri kuwasaidia endapo atagundulika endapo atagundulika kama atakuwa na ujauzito

  Imedaiwa kuwa dada wa binti huyo alitaka kwanza kujua hatma ya afya ya mdogo wake ili mengine yafate baada na kudaiwa alikubali kupokea kwanza kiasi cha shilingi laki tano na kuahidiwa kiasi kingine kama hicho leo ili aweze kufuta kesi hiyo

  Chanzo cha habari kilidai kuwa, dada huyo anatarajiwa kupatiwa kiasi hicho leo mbali na hicho alichopewa na haijafahamika kama anamtega bosi huyo ama la

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Matatani kwa kusababisha ubakaji wa housegirl[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #e1e1e1"]
  [TD]
  [​IMG]
  [/TD]
  [TD]Monday, June 27, 2011 10:54 AM
  MWANAMKE mmoja anayetambulika kwa jina la Mama Mudy ameingia matatani baada ya kusababisha ubakwaji wa mfanyakazi wake wa kazi za ndani huko maeneo ya Uwanja wa Ndege jijini Dar es salaam.

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Mwanamke huyo imedaiwa kuwa, juzi majira ya saa 4 usiku, alimfukuza msichana huyo aliyetambulika kwa jina la Grace [17] nyumbani kwake baada ya kukerwa na kuchelewa kurudi nyumbani kwa msichana huyo baada ya kwenda kumtembelea ndugu yake maeneo ya Kinyerezi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam

  Imedaiwa kuwa msichana huyo juzi asubuhi aliomba ruhusa kwa bosi wake huyo kwenda kumtembelea dada yake binamu anayeishi maeneno ya Kinyerezi na alitakiwa kurudi nyumbani hapo isizidi saa 12

  Hata hivyo imedaiwa kuwa msichana huyo aliweza kurejea nyumbani hapo majira ya saa 4 usiku kwa kuchelewa kwa sababu ambayo haikufahamika mara moja

  Imedaiwa mwanamke huyo kwa kukerwa na uchelewaji wa msichana huyo, alimuamuru msichana huyo arudi alipotoka na msichana huyo alijaribu kumuomba bosiw ake huyo amruhusu aingie ndani lakini ilishindikana

  Hivyo imedaiwa kuwa msichana huyo aliweza kuripoti tukio hilo kwa baadhi ya majirani na aliweza kurudi kwa dawa yake alikotoka na aliondoka nyumbani hapo saa 5 kasorobo usiku kuelekea kwa daa yake

  Imedaiwa msichana huyo kabla hajafika kwa dada yake njiani alikutana na vijana wawili walimrubuni kumpa lifti ya pikipiki kumpeleka alikokuwa akienda na msichana huyo aliweza kudanganyika na kukubali lifti hiyo

  Imedaiwa vijana hao hawakuweza kutimiza lengo la binti huyo na walimpeleka katika chumba walikokuwa wakiishi vijana hao ‘maskani' na walianza kumbaka msichana huyo kwa kupokezana kisha ilipofika majira ya saa 7 usiku walimpeleka msichana huyo karibu na nyumba anakoishi dada yake huyo na kumuacha hapo

  Kwa mujibu wa maelezo ya binti huyo alifika kwa dada yake huyo majira ya saa 7:10usiku na dada yake alishangazwa kwa kumuona na alipomueleza yaliyomtokea dada huyo alimuamuru kurudi kwa bosi wake huyo

  Hata hivyo imedaiwa dada huyo aliweza kurudi nyumbani hapo na kumueleza yaliyomtokea msichana huyo na dada huyo kumfahamisha kuwa anakwenda kuripoti tukio hilo kituo cha polisi kutokana na kusababisha hatari kwa binti huyo

  Ilidaiwa ilikuwa majira ya saa 9 usiku walipofika nyumbani hapo na mwanamke huyo kumuomba dada wa binti huyo kuyamaliza wenyewe na asiripoti tukio hilo kituoni hata hivyo dada huyo hakuweza kubadili msomamo wake

  Imedaiwa mwanamke huyo usiku huo baada ya kuondoka kwa dada huyo mwanamke huyo aliwasha gari na kuondoka na hadi jana jioni ilikuwa haijafahamika alitorokea wapi


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  hizo ni habari tofauti lakini mnabaisho mmoja lazima tuulize hawa watu wana siri gani jamani
  nyumba nyingi zinaumia sasa kama azijachomwa moto na awa wah
   
Loading...