Amvulia nguo obama, awa bilionea

Amvulia nguo obama, awa bilionea

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,955


Juan James Rodriguez baada ya kukamatwa na polisi wakati akitangaza tovuti ya bilionea Alki David .
​
<center style="margin: 0px; padding: 0px; border: 0px; outline: 0px; vertical-align: baseline; background-color: transparent; font-size: 16px; background-position: initial initial; background-repeat: initial initial;"></center>
MWANAUME ambaye alijitokeza mbele ya rais wa Marekani, Barack Obama akiwa uchi wa mnyama huku akiwa na maandishi ya kutangaza tovuti ya bilionea Alki David, amejishindia zawadi ya dola milioni 1 toka kwa bilionea huyo.


Juan James Rodriguez, 24, alitiwa mbaroni na polisi baada ya kujitokeza mbele ya rais wa Marekani, Barack Obama akiwa uchi wa mnyama huku akiwa na maandishi makubwa kifuani na tumboni ya kutangaza tovuti ya bilionea Alki David.

Rais Obama alikuwa Philadelphia akikipigia kampeni chama chake wakati Juan alipojitokeza mbele yake ghafla akiwa uchi wa mnyama.
Bilionea Alki, Mgiriki aliyezaliwa Lagos, Nigeria alitangaza zawadi ya dola milioni moja kwa mtu yoyote atakayejitokeza uchi wa mnyama mbele ya rais Obama huku akiwa na maandishi ya kutangaza tovuti ya bilionea huyo inayoitwa “BATTLECAM”.

Akiongea na waandishi wa habari, bilionea huyo alisema kuwa atatimiza ahadi yake kwa kumzawadia dola milioni 1, Juan ingawa kwa sasa wanaangalia video za tukio hilo ili kujua kama masharti yote ya zawadi hiyo yalifuatwa.

Sharti la kushinda kitita hicho kinono lilikuwa ni kujitokeza mbele ya rais Obama na kuhakikisha Obama amekuona na pia kutamka kwa sauti kubwa “Battlecam.com” mara sita.
Ingawa Juan huenda akashinda dola hizo milioni 1, alikamatwa polisi na kufunguliwa mashtka ya kujianika hadharani kinyume cha maadili ya jamii.


Rodriguez akitangaza tovuti ya bilionea Alki David ya “BATTLECAM”


AMA KWELI PESA NI SHETANI MKUBWA DUNIANI AHHHH JAMAA AMAWAGA RAZI MBELE YA RAIS OBAMA.?
​
 
Money is not the source of evils but it is a great motivator of evils.
 
mm kazi kwelikweli kujifanya hayawani.
 
Masharti mengine bana, sijui ndevu za panya, mara mabega ya nyoka. Hela hii......?
 
Ingetangazwa bongo, umati woote wa waliokwenda kwenye eneo husika wange saula ili wapata US$ 1M ambazo ni sawa na TShs. 1.6Bn. Cheza na kifo lakini Usicheze na njaa!
 
Aisee na huku bongo si walete hiyo ..tufanye mbele ya MUKULU............
 
Back
Top Bottom