Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 8,269
- 25,310
Monalisa Perez mwenye umri wa miaka 19 aliwekwa alipandishwa katika Mahakama moja mjini humo baada ya kumpiga risasi Pedro Ruiz ambaye ni mpenzi wake baada ya kutaniana kwa kuweka kitabu katika kifua cha mpenzi wake huyo akidhani kitazuia risasi hiyo kuingia.
Wawili hao wana mtoto wa miaka mitatu na takribani watu 30 walikuwa wakiangalia video hiyo ya YouTube alipompiga risasi mpenziwe. Shangazie Ruiz anasema kuwa walifanya kitendo hicho ili kuongeza marafiki katika mitandao ya kijamii.
Claudia Ruiz aliambia runinga ya WDAY-TV kwamba binamu yake alimwambia kwamba alitaka kufanya kitendo hicho '' kwa sababu walihitaji kupata wafuasi zaidi''. ''tunataka kuwa maarufu''.
''Aliniambia kuhusu wazo hilo na nikamwambia'',''Wasifanye jambo hilo ''.
''Kwanini utumie bunduki? Kwa nini?'', Claudia Ruiz aliambia chombo hicho cha habari.
Chanzo: BBC