Amuua mkewe kwa kumkata sikio na kumnyonga akihoji fedha za mauzo ya Mbuzi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia Boshu Kulwa (60) kwa tuhuma za kumuua mke wake, Magdalena Lunguya (45) baada ya kumhoji kuhusu fedha za mauzo ya mbuzi.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Debora Magiligimba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema kuwa amemuagiza mkuu wa polisi wilaya ya kipolisi Msalala, kufuatilia suala hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi baada ya upelelezi kukamilika.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Nyamingu, Masesa Manyanda alisema tukio lililokea Saa 9:00 alfajiri Novemba 5, 2020 katika kijiji cha Nyamingu, kata ya Busangi wilayani hapa.

Alisema siku ya tukio alifuatwa na watoto watatu wakidai baba yao amempiga na kumuua mama yao.

“Nilipofika nyumbani kwao nilikuta amelazwa chumbani akiwa na majeraha mwilini, sikio la kushoto likiwa limekatwa na kitu chenye ncha kali na shingo imenyongwa,” alisema.

Mwananchi
 
Umasikini tu.

Serikali itengeneze mazingira ya kuweza kuondoa umasikini kirahisi.

Kuanzia na mfumo mbovu wa elimu.
 
Back
Top Bottom