Amtetea Mike Tyson, Amuua Mgeni Wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amtetea Mike Tyson, Amuua Mgeni Wake

Discussion in 'Sports' started by kilimasera, Apr 18, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mwanaume mmoja toka Urusi ambaye alikuwa akibishana na wageni wake kuwa bingwa wa zamani wa ngumi za uzito wa juu Mike Tyson ni mkali zaidi kuliko wababe wa sasa duniani katika ngumi hizo ndugu wawili wa familia ya Klitscho toka Ukraine, ubishi huo umepelekea mwanaume huyo amuue rafiki yake.
  Ubishi uliozuka kwenye nyumba ya mwalimu Nikolai Makayev wa mji wa Tyumen nchini Urusi ulipelekea mwalimu huyo awacharange kwa kisu wageni wake wawili.

  Katika ubishi huo, Nikolai alikuwa akibishana na wageni wake juu ya nani mkali kati ya Mike Tyson na ndugu wawili toka Ukraine wa familia ya Klitschko ambao hivi sasa ndio wanaotamba duniani katika anga ya ngumi za uzito wa juu.

  Nikolai ambaye alikuwa akipata ulabu pamoja na wageni wake hao wawili, alitamba kuwa Tyson ndio mkali zaidi kuliko Vitali Klitschko na ndugu yake Wladimir Klitschko.

  Wageni wake walimshutumu Nikolai kuwa hana uzalendo kwa kumshabikia Tyson ambaye ni bondia wa Marekani na kuwaacha akina Klitchko ambao wao ni Warusi.

  Nikolai alikasirika kuambiwa hivyo na ghafla alichukua kisu na kuanza kumshambulia mgongoni mmoja wa wageni wake.

  Mgeni mwingine ambaye naye alikuwa ni rafiki wa karibu wa Nikolai, aliamua kukimbilia nyumbani kwake kunusuru maisha yake ingawa naye alikuwa tayari ameishajeruhiwa kwa kuchomwa na kisu na Nikolai.

  Polisi waliitwa lakini hadi wanafika tayari Nikolai alikuwa ameishamuua mmoja wa wageni wake.

  Vifo vinavyosababishwa na pombe vimekuwa vikiongezeka nchini Urusi ambapo watu 500,000 huuliwa au hufariki kutokana na ulevi.

  Hali hiyo imewaathiri zaidi wanaume nchini Urusi ambapo wanaume wengi wamekuwa wakifariki kutokana na ulevi au matatizo yanayotokana na pombe, hali hiyo imesababisha kuwe na idadi kubwa ya wanawake kuliko idadi ya wanaume nchini Urusi.
  tys.jpg
   
 2. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Ahsante sana kwa taarifa kiongozi, inaonyesha mzimu wa Tyson bado unawafwnya wazungu wanaweweseka.... ila huyo mlevi alikuwa sahihi ila sasa hapo kuuwa wenzie sasa ndio kamzidi hadi Tyson mwenyewe sababu ye Tyson aling'ata tu wala hakuua
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hawa jamaa ni wabaguzi sana hasa pande hizi za urrusi lazima wamfagilie wa kwao!hawapendi kabisa nyani
   
Loading...