Chief Kumbyambya
JF-Expert Member
- Jun 16, 2022
- 490
- 1,461
Wasalaam mazee,
Natumai muwazima wa afya tele kabisa na mambo yanakwenda sawa bin sawia.
Kipindi anapigana Muhammad Ali mimi sikuwepo lakini sababu ya mambo ya utandawazi uliopo sazi nimebahatika kuangalia mapambano mengi sana ya Muhammad Ali kama nikikuwepo vile na kiukweli jamaa alikuwa anajua na alizikonga nyoyo za mashabiki haswa.
Lakini pia nimebahatika kufuatilia mapambano mengi sana ya Mike Tyson ambayo sikuyaona lakini kwa msaada wa mtandao nimeyaona yote kama nilikuwepo vile wakati kwa umri wangu nimekuta Mike Tyson ndiyo anaishia ishia hivi lakini kupitia mitandao nimeyaangalia mapambano yake yote ya nyuma kama nilikuwepo vile.
Tuje Muhammad Ali Vs Iron Mike Tyson.
Wazee nafikiri Muhammad Ali anapewa heshima yake na kuangaliwa na wengi kama kivutio cha mchezo wa ngumi sababu yeye ndiye alisababisha mchezo huu kuanza kufuatiliwa na kuwa mchezo namba mbili wenye mashabiki wengi zaidi duniani ukitanguliwa na mpira wa miguu ambao ndio unashikilia nafasi ya kwanza.
Ila kuikweli Mike Tyson alikuwa anapiga ngumi mazee. Aisee ngumi za Mike Tyson zilikuwa zinasisimua mzee, yani mtu anakula kichapo mpaka unaeangalia kama una roho nyepesi unaweza kufunga macho usione mtu anavyokufa live.
Kwa upande wangu ukiwapambanisha hawa wawili kama wangekuwa katika era moja na kwa mapambano yao niliyoyaona wakipigana basi Muhammad Ali naamini angechakazwa vilivyo na Iron Mike Tyson. Tyson alikuwa na style yake hatari sana ya kupigana inayojulikana kama ”Peek A Boo.” Hii ni moja kati ya style ngumu inayowashinda mabondia wengi kuimaster hivyo ukimtoa aliemfundisha Tyson bwana D’Amanto hakuna bondia yeyote yule anayeiweza style hii zaidi ya Tyson mwenyewe.
Sijajua kama huu ni mtazamo wangu tu au kuna wengine wanaliona hili.
simshushi cheo Muhammad Ali, atabakia kuwa mtangulizi aliesababisha mchezo huu kupendwa na watu wengi zaidi ilaaaa narudia tena ilaaaaa Mike Tyson alikuwa anapiga ngumi bwana, wacha kabisa.