Pape
JF-Expert Member
- Dec 11, 2008
- 5,488
- 79
Jana jioni nilipigwa na butwaa kumuona rafiki yangu akilia kuliko kawaida! Nilipomuuliza alishindwa hata kuongea! Basi nilianza kazi ya kubembeleza. Mwishowe nikaona hali yake inakuwa mbaya kwani alikuwa anaonekana anauchungu sana kiasi cha mwili wote kumtetemeka! Alikuwa hataki hata kunywa kitu chochote!
Niliamua kumpigia simu mpenzi wake (girlfriend wake) kujua kama anataarifa yeyote! ndipo aliponiambia kwamba 'its over between them'...Niliamua kwenda kuongea na shem wangu ana kwa ana kwani hali ya jamaa ilikuwa ni mbaya sana (usipime)!
Shem aliniambia kwamba siku za hivi karibuni alianza kupoteza mapenzi kwa jamaa (rafiki yangu) kwahiyo alikuwa hajisikii kitu chochote na ndio maana ameamua kusitisha uhusiano wao! Nikamuuliza tena sasa ndio itakuwaje? Akanipa jibu kwamba amepata 'mtu mwingine ambaye anahisi ndiye chaguo lake la moyo!
Baada ya kurudi home kwangu nikajaribu kumuuliza mshikaji wangu nae akasema kwamba yeye (mpenzi wake ndiye ameamua) na kunipa sababu aliyopewa na shem (sababu ile ile shem aliyonipa mimi wakati naongea nae).
Sasa nimeendelea kukaa na huyu jamaa lakini analia na kuniambia kwamba kuachwa na huyu mpenzi wake ni pengo kubwa sana! Jamaa yaani analia tu kula hali! Nimejaribu kumwekea movie aaangalie lakini wapi!
Naleta kwenu jamani, hivi kuna njia gani ya kumfariji mtu aliyeachwa na mpenzi wake? Nifanyeje kumsaidia manake naogopa jinsi anavyoweweseka hapa! Je, nimwache alie tuuu au nifanyeje?