Ampendae kampiga kibuti: afanyeje ili kuvumilia maumivu ya 'heart break'? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ampendae kampiga kibuti: afanyeje ili kuvumilia maumivu ya 'heart break'?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pape, Feb 6, 2010.

 1. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Jana jioni nilipigwa na butwaa kumuona rafiki yangu akilia kuliko kawaida! Nilipomuuliza alishindwa hata kuongea! Basi nilianza kazi ya kubembeleza. Mwishowe nikaona hali yake inakuwa mbaya kwani alikuwa anaonekana anauchungu sana kiasi cha mwili wote kumtetemeka! Alikuwa hataki hata kunywa kitu chochote!

  Niliamua kumpigia simu mpenzi wake (girlfriend wake) kujua kama anataarifa yeyote! ndipo aliponiambia kwamba 'its over between them'...Niliamua kwenda kuongea na shem wangu ana kwa ana kwani hali ya jamaa ilikuwa ni mbaya sana (usipime)!

  Shem aliniambia kwamba siku za hivi karibuni alianza kupoteza mapenzi kwa jamaa (rafiki yangu) kwahiyo alikuwa hajisikii kitu chochote na ndio maana ameamua kusitisha uhusiano wao! Nikamuuliza tena sasa ndio itakuwaje? Akanipa jibu kwamba amepata 'mtu mwingine ambaye anahisi ndiye chaguo lake la moyo!

  Baada ya kurudi home kwangu nikajaribu kumuuliza mshikaji wangu nae akasema kwamba yeye (mpenzi wake ndiye ameamua) na kunipa sababu aliyopewa na shem (sababu ile ile shem aliyonipa mimi wakati naongea nae).

  Sasa nimeendelea kukaa na huyu jamaa lakini analia na kuniambia kwamba kuachwa na huyu mpenzi wake ni pengo kubwa sana! Jamaa yaani analia tu kula hali! Nimejaribu kumwekea movie aaangalie lakini wapi!

  Naleta kwenu jamani, hivi kuna njia gani ya kumfariji mtu aliyeachwa na mpenzi wake? Nifanyeje kumsaidia manake naogopa jinsi anavyoweweseka hapa! Je, nimwache alie tuuu au nifanyeje?
   
 2. A

  Artman Member

  #2
  Feb 6, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mapenzi ni watu wawili kupendana, sasa kama mtu mmoja hajisikii chochote kwa mwenzake, hata wakirudiana mapenzi hapo hamna. Ndo yale utasikia mke anakuwa na buzi lake nje. Huyo rafiki yako ajitahidi kuchukuliana na hali hiyo na aone kama haikuwa bahati yake. Tena ashukuru Mungu kwa kuwa hali hii imejitokeza wakati bado wako kwenye urafiki, ingetokea wakiwa kwenye ndoa ingekuwa balaa.

  Cha kumsaidia kwa sasa ili asiwaze sana juu ya hilo, wewe mtoe out, mahali kwenye mkusanyiko wa watu wengi ili aweze kubadili mazingira na mawazo. Mfano mnaweza kwenda beach, mnaweza kwenda kutembea kwenye masupermarket makubwa kama Mliman city n.k.

  Kazi kweli kweli.
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 38,087
  Likes Received: 9,747
  Trophy Points: 280
  The best way to get over a lover is to get a new and better lover.
   
 4. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Je, hiyo si inakuwa kama vile ni kukomoana?
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 38,087
  Likes Received: 9,747
  Trophy Points: 280
  Hapana, itakuwa kukomoana tu kama unataka kujionyesha. Ikiwa part ya ku-move on, ikiwa imefanywa kwa sababu ya kutaka kumridhisha aliyepigwa kibuti zaidi ya kutaka kumuonyesha aliyepiga kibuti, inaitwa "betterment".

  Ikiwa inafanywa kwa sababu ya kumuonyesha aliyepiga kibuti inaiwa "bitterment" na zaidi ya yote inaonyesha aliyepigwa kibuti hajaweza kusema "it is over".  Pussywhipped 26: 1 -2.
   
 6. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  well noted but what is that in red?
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,973
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 145
  Jamani vibuti ni kawaida kwa sisi wanaume kupigwa inategemea sera zako pamoja na jinsi gani unavyo hudumia mzigo.
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 38,087
  Likes Received: 9,747
  Trophy Points: 280
  Hiyo biblia ya mambo ya relationship, si unaona inakupa na aya kabisa.
   
 9. bht

  bht JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  hicho kitabu kipe jina lingine ikiwezekana basi....
   
 10. bht

  bht JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  ufafanuzi hapo nilipopigia mstari
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Feb 6, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,973
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 145
  Hahahaha yaani huduma anazitoa jamaa kwa huo mzigo mpaka ukaamua kumpiga kibuti yaelekea alikuwa hazami sana kwenye EPA ndo maana mzigo ukaamua kumpiga red card. Hujui mapenzi siku hizi bila EPA hayaendi?
   
 12. bht

  bht JF-Expert Member

  #12
  Feb 6, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  kwa hiyo mwanamke ndio mzigo wenyewe hapo???
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Feb 6, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,973
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 145
  Ndo maanake, upo sahihi kabisa. Ukisikia mtu anasema ule mzigo jamaa anaubeba manaake ni mwanamke.
   
 14. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #14
  Feb 6, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Pole sana na hilo lilokupata au yalompata rafiki yako..Katika mapenzi jamani ni hamna jinsi ya kumsaidia zaidi ya yeye kuanza kusahau kidogo kidogo,watu watatoa mengi fanya hivi fanya hivi jamani kibuti jamani kinauma,yakikupata ndo utajua nini maana ya kuachwa,sometimes to be player helps cuz utakutana na mengi ya kuachwa au kuacha,yameshanitokea hayo ndo maana naandika hivyo..Mkuu huyo rafiki yako kaa nae karibu tuu soon he will be okay and find another one to replace...daima lenye mwanzo mwisho unasubiri ingawa utachelewa..
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Feb 6, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 43,164
  Likes Received: 27,143
  Trophy Points: 280
  Pape ni msanii.
   
 16. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #16
  Feb 6, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,734
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 180
  ...mwambie ujasiri hupimwa kwa jinsi anavyoweza kukabiliana na mshtuko kama huo, ...asing'ang'anie kuangalia mlango ulofungwa akakosa kuona milango mipya inayofunguka mbele yake,

  Kama hataki kuelewa, mpe kalamu na karatasi aorodheshe mabaya ya huyo mpenzi wake kuanzia walipoanzana mpaka walipoachana, atafarijika tu.
   
 17. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #17
  Feb 6, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nitaipata wapi?
   
 18. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #18
  Feb 6, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Jamani EPA ndio kitu gani katika mapenzi?
   
 19. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #19
  Feb 6, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Msanii wa mapenzi?
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Feb 6, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 78,282
  Likes Received: 40,524
  Trophy Points: 280
  Rebound is not good. It's better to take a break and regroup before you jump into another relationship. And passage of time is the best healer of heartache.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...