Amos Makala karibu Mbeya

mambawengi

Member
Jan 23, 2015
26
6
Kwanza hongera kwa kuwemo katika awamu hii ya tano, lakini kumbuka unaingia mkoa uliowashinda wengi akiwemo kandoro Ila naomba katika kazi zako usisahau kumulika wilaya ya mbeya vijijni bonde la songwe kitongoji cha kaloleni.

Mh,tunaporwa ardhi na mkuu wa wilaya akishirikiana na watendaji wa ardhi,
kumbuka sisi ndio tuliopisha kiwanda cha cement kwa manufaa ya umma, tena tukapisha kiwanda cha mbeyatex kwa manufaa ya umma, tena tukapisha uwanja wa ndege kwa manufaa ya umma,

Lakini leo tunaporwa ili wawauzie wenye fedha wakitumia dalali anaeitwa amboni. Tunajua jambo hili utilifuatilia na kulitendea haki...salaaam.
 
Huyu jamaa mliyeletewa si ndiye aliyefuta likizo kwa Walimu kule alikotoka?
 
Kwanza hongera kwa kuwemo katika awamu hii ya tano,
lakini kumbuka unaingia mkoa uliowashinda wengi akiwemo kandoro
Ila naomba katika kazi zako usisahau kumulika wilaya ya mbeya vijijni
bonde la songwe kitongoji cha kaloleni.
Mh,tunaporwa ardhi na mkuu wa wilaya akishirikiana na watendaji wa ardhi,
kumbuka sisi ndio tuliopisha kiwanda cha cement kwa manufaa ya umma,
tena tukapisha kiwanda cha mbeyatex kwa manufaa ya umma,
tena tukapisha uwanja wa ndege kwa manufaa ya umma,
Lakini leo tunaporwa ili wawauzie wenye fedha wakitumia dalali anaeitwa amboni
Tunajua jambo hili utilifuatilia na kulitendea haki...salaaam.
Duu umenikumbusha nilienda kutafuta shamba nikaambiwa huwezi pata bila kumuona wakala wa mkuu wa wilaya Mr Ambani sikuamini ila leo unaanza kunipa mwanga. Naamini Rc atapata ujumbe huu liwe jipu lake la kwanza kulitumbua, ama akikaa kimya tutajua naye kaingia kwenye biashara
 
Kuna haja tufundishwe roles za Mbunge ni na za Meya na hawa mnawaita wakuu wa Wilaya maana kuna hatari tukampa mkuu wa mkoa kazi zisizomhusu
 
Kuna haja tufundishwe roles za Mbunge ni na za Meya na hawa mnawaita wakuu wa Wilaya maana kuna hatari tukampa mkuu wa mkoa kazi zisizomhusu
Kuna baadhi ya wakuu Wa wilaya ni majipu,kuingilia kazi za watendaji kwa maslahi binafsi ndiyo maana migogolo mingi ya ardhi imehusisha wakuu Wa wilaya kwa zaidi ya 60%.Nadhani hao wakuu Wa wilaya ndiyo Wa kupewa semina ya utendaji kazi
 
Back
Top Bottom