Amnyonga Mkewe kwa shati

Babuji

Senior Member
Nov 27, 2008
197
3
MWANAMKE mmoja ameuawa baada ya kunyongwa na mumewe kwa sababu za wivu wa kimapenzi.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Khamisi Bhai, alisema tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Lushamba katika kata ya Kazunzu Wilayani Sengerema ambako Amina Ibrahimu [22] alinyongwa na mumewe Dotto Fidelis[27] kwa kutumia shati lake.

Alisema baada ya kumnyonga mkewe aliandika ujumbe ukieleza kuwa amemuua Amina kwa sababu ya wivu wa kimapenzi.

Kamanda huyo alisema baadaye Dotto alitoroka na siku iliyofuata alikutwa amejinyonga kwenye shamba la mkazi wa kisiwa cha Nyamango Wilayani Sengerema ambaye mwenye shamba jina lake hakufahamika.

Source: NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
 
Back
Top Bottom