Amnyonga mkewe kisha kukimbia na 300k

Amnyonga mkewe kisha kukimbia na 300k

Inasikitisha kuona maisha yakipotea kizembe kwa namna hii. Ikiwa taarifa hizi zitathibitishwa na vyombo vya uchunguzi, ni muhimu sheria ichukue mkondo wake na haki itendeke. Pole kwa familia, watoto na wote walioguswa na msiba huu. Tuache mamlaka husika zikamilishe uchunguzi ili ukweli wote ujulikane.
mm namuombea huyo jamaa akamatwe naye anyongwe tu
 
mm namuombea huyo jamaa akamatwe naye anyongwe tu
Mkuu najua una maumivu makali lakini kumbuka kwamba adhabu ya kunyongwa au hatia ya mtuhumiwa huamuliwa na mahakama (japo tuna mahakama maagizo kutoka juu)baada ya mchakato wa haki kukamilika. Ni vyema kuepuka kutoa hukumu kabla ya uchunguzi na kesi kukamilika.
 
Mwanamke asiye mwaminifu ndani ya ndoa, anakisogelea kifo
 
Nimeitoa FB

============================================================================

R.I.P uyo mwanamke ndiye marehemu na huyo wapembeni ndiye alikua akiishi nae kama mume hivyo alichukua jukumu la kumuua mke wake mchana waleo akiwa shambani hivyo alipo fanya tukio alichukua simu ya marehemu na kutuma sms kwa watoto wake ambao wao walikua nyumbani "sms ikisema (BABA ENU MDOGO AKIJA MPATIENI LAKI TATU)

Hivyo jama alipofka nyumbani akawaambia watoto mmeona sms ya mama yenu watoto walisema ndiyo, kisha wakampatia hela huyo baba kiasi cha tsh 300,000/= uyo baba wa kambo akaondoka,

lkn muda ulizidi kwenda, Mama yao wakaona haludi nyumbani, wakapatwa na mashaka walichukua jukumu la kwenda kumtafuta shambani maeneo YALUGONGA na kukuta Uyo mama kauwawa kwa kunyongwa lkn huyo jamaa yeye alichukua boda na kuelekea BAHI akiwa tayari amechukua mizigo yake,

TUKIO ILI LIMETOKEA SAA NANE MCHANA LEO TAREHE 20~07~2026, MKOA WA DODOMA WILAYA YA BAHI,

mpaka sasa saa 20:39 mwili upo shambani wanasubiliwa polic
============================================================================
View attachment 3634206
AISEE NIMEONA FB NIMEUMIA YAAN KILA TUKIAMKA KUNA MATENDO YA KUJIUA AMA KUUWANA

KHA

ALLAH UTUEPUSHE NA VIFO VISIVYO NA ULAZIMA
 
Hao ndugu wa@mpwayunguvillage sasa wamezidi wiki hizi chache.Mara baba amtwae/aoe mke wa kijana wake.Hatujakaa sawa, couple w
inauana kwa gharama ya chupa moja ya wanzuki aina ya "Hennessy"!
 
Mimi sio muumini wa ile dini ya 'usiolewe na mwanaume maskini' ila watu hawa nawaelewa na nawaunga mkono because wtf is this? Mtu anatoa mwenzie uhai kwa laki tatu!
 
The other gender katika ubora wao na bado kuna wapuuzi wanamtetea, hivi hata kama ukijificha unakua unajisikiaje kua umedhulumu uhai kiumbe ambacho hukukitia wewe uhai, hata kama umesalitiwa jiue wewe mbona easy tu.
 
Nimeitoa FB

============================================================================

R.I.P uyo mwanamke ndiye marehemu na huyo wapembeni ndiye alikua akiishi nae kama mume hivyo alichukua jukumu la kumuua mke wake mchana waleo akiwa shambani hivyo alipo fanya tukio alichukua simu ya marehemu na kutuma sms kwa watoto wake ambao wao walikua nyumbani "sms ikisema (BABA ENU MDOGO AKIJA MPATIENI LAKI TATU)

Hivyo jama alipofka nyumbani akawaambia watoto mmeona sms ya mama yenu watoto walisema ndiyo, kisha wakampatia hela huyo baba kiasi cha tsh 300,000/= uyo baba wa kambo akaondoka,

lkn muda ulizidi kwenda, Mama yao wakaona haludi nyumbani, wakapatwa na mashaka walichukua jukumu la kwenda kumtafuta shambani maeneo YALUGONGA na kukuta Uyo mama kauwawa kwa kunyongwa lkn huyo jamaa yeye alichukua boda na kuelekea BAHI akiwa tayari amechukua mizigo yake,

TUKIO ILI LIMETOKEA SAA NANE MCHANA LEO TAREHE 20~07~2026, MKOA WA DODOMA WILAYA YA BAHI,

mpaka sasa saa 20:39 mwili upo shambani wanasubiliwa polic
============================================================================
View attachment 3634206

Mwanaume wa hovyo atakuja kujuta sana; unaua sababu ya hako katundu hapo chini, unaacha watoto wanateseka bila Mama yao???? Mbuzi kabisa huyu, atashikwa haraka sana
 
Ikithibitika yeye ndie muuaji atahimili kweli mitikasi ya jela kweli
 
Back
Top Bottom