Amnesty International: Kabendera ameonewa, hakustahili kununua uhuru wake

Amnesty International: Kabendera ameonewa, hakustahili kununua uhuru wake

Tunamshukuru Mungu kwa hili swala la #Eric kabendera ,amefanikisha kumtoa kwenye mikono ya watesi .
siku zote Mungu ni mkuu kuliko tawala za kimabavu na kandamizi
Grory be to Our Greatest God.
 
Kumbe hii serikali ya wauaji?!
Pohamba,
Unajua haya mashirika yanaweza kumpump ili azidi kuichukia serikali then mwisho wa kabendera waweza kuwa kifo kwa sababu hatoishi maisha yake bali ya kuambiwa na watu na akifa washikaji zake watafurahi mno hao akina amnest maana watapata misaada kibao kwa kifo chake.

Nadhani Eric be careful, achana na wajinga wajinga hao, umepatikana na hatia, lipa hizo gharama, kaa tuijenge nchi, hao amnest kama wana uchungu wakamtoe tule mwandishi wa aljazeera au wamrudishe snowden US.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Awamu hii kweli inanyoosha haswa.. hata hawa bado wanyumba yumba!!!.. yupo nyumbani kwake.. wamusaidie kulipa.. wanyamaze.. walitaka awe huru na ameachiliwa muda wao walikuwa wakitamani kumutumia ili kupiga ramli zao juu ya Tanzania.. kuichafua tu nchi yetu
Kwani wewe unauchungu gani na Tanzania zaidi ya nchi yako Rwanda?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
The so called mwanahabari za kiuchunguzi, Erick Kabendera, hajawahi kuchunguza lolote lililofukunyua skendo lenye manufaa ya umma, kubwa wala dogo.

His name recognition is bigger than the profile of his work, if any.
 
Baada ya kupiga ban Bashite asiingie kwao, sasa wanaandaa hati ya mashitaka ili genge lenu mkafikishwe icc ili mfundishwe jinsi ya kutawala

In God we Trust

Sifahamu ni nani umemtaja..
 
Mara baada ya kuachiwa huru kutoka jela mwandishi wa habari za uchunguzi Eric Kabendera baada ya kulipa faini na fidia ya jumla ya Shs 273 milioni, Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Binadamu kimataifa (Amnesty International) ofisi ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika Deprose Muchena ameeleza masikitiko yake juu faini ya fedha kubwa kiasi hicho.

“Wakati habari za kuachiwa kwa Kabendera zimepokelewa kwa furaha baada ya kukaa jela karibuni miezi saba, inashitusha kuona kuwa amelazimishwa kulipa kiwango kikubwa cha faini ili kupata uhuru wake, baada ya kuwa aliwekwa mahabusu kwa uonevu kwa sababu alikuwa anatumia haki yake ya uhuru wa kujieleza.

“Mama yake Kabendera alikufa wakati yeye yuko mahabusu kipindi kifupi baada ya kutoa maombi yake kwa Rais John Magufuli kupitia kituo cha televisheni kwamba amwachie huru mtoto wake.

Taarifa ya Amnesty International inasema kuwa tayari Kabendera ameteseka kwa kiasi kikubwa kwa kutekeleza wajibu wake wa Kiuandishi na alistahili kuachiwa bila masharti yoyote.

"Hakuna haki kabisa katika kile kilichofikiwa mahakamani mjini Dar es Salaam hivi leo," amesema mkurugenzi huyo.

Ameongeza : “Tanzania lazima iache kutumia vibaya sheria zinazotumika kukiuka haki za watu katika kutumia uhuru wao, uhuru wa kujelezea na kupashwa habari, kukusanyika kwa amani na kujiunga na chama wanachotaka."

Shirika hilo limesisitiza kuwa :"Ni lazima nchi ichukue ahadi hadharani kwamba itamhakikishia kila mtu ana uhuru wa kutumia haki zao zote za kibinadamu na kuacha kutumia sababu zinazochochewa na siasa kuwabana wapinzani na waandishi kama Eric Kabendera.”

Chanzo: VOA Swahili
Hawa sijui amnesty international ni majuha na wajinga wakubwa...hovyo kabisa....huyo kabendera wao alikamatwa kwa kuandika habari au kwa makosa hayo aliyokutwa nayo na kukiri??!! Idiots
 
Hawa sijui amnesty international ni majuha na wajinga wakubwa...hovyo kabisa....huyo kabendera wao alikamatwa kwa kuandika habari au kwa makosa hayo aliyokutwa nayo na kukiri??!! Idiots
Wacha upumbavu wewe yaani ndiyo unajiona unajua kila kitu na kuwaona wenzako ni ma idiot?

In God we Trust
 
Back
Top Bottom