Amnesty International: Kabendera ameonewa, hakustahili kununua uhuru wake

Amnesty International: Kabendera ameonewa, hakustahili kununua uhuru wake

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,560
Reaction score
3,955
Mara baada ya kuachiwa huru kutoka jela mwandishi wa habari za uchunguzi Eric Kabendera baada ya kulipa faini na fidia ya jumla ya Shs 273 milioni, Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Binadamu kimataifa (Amnesty International) ofisi ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika Deprose Muchena ameeleza masikitiko yake juu faini ya fedha kubwa kiasi hicho.

“Wakati habari za kuachiwa kwa Kabendera zimepokelewa kwa furaha baada ya kukaa jela karibuni miezi saba, inashitusha kuona kuwa amelazimishwa kulipa kiwango kikubwa cha faini ili kupata uhuru wake, baada ya kuwa aliwekwa mahabusu kwa uonevu kwa sababu alikuwa anatumia haki yake ya uhuru wa kujieleza.

“Mama yake Kabendera alikufa wakati yeye yuko mahabusu kipindi kifupi baada ya kutoa maombi yake kwa Rais John Magufuli kupitia kituo cha televisheni kwamba amwachie huru mtoto wake.

Taarifa ya Amnesty International inasema kuwa tayari Kabendera ameteseka kwa kiasi kikubwa kwa kutekeleza wajibu wake wa Kiuandishi na alistahili kuachiwa bila masharti yoyote.

"Hakuna haki kabisa katika kile kilichofikiwa mahakamani mjini Dar es Salaam hivi leo," amesema mkurugenzi huyo.

Ameongeza : “Tanzania lazima iache kutumia vibaya sheria zinazotumika kukiuka haki za watu katika kutumia uhuru wao, uhuru wa kujelezea na kupashwa habari, kukusanyika kwa amani na kujiunga na chama wanachotaka."

Shirika hilo limesisitiza kuwa :"Ni lazima nchi ichukue ahadi hadharani kwamba itamhakikishia kila mtu ana uhuru wa kutumia haki zao zote za kibinadamu na kuacha kutumia sababu zinazochochewa na siasa kuwabana wapinzani na waandishi kama Eric Kabendera.”

Chanzo: VOA Swahili
 
Mimi sitaki shobo kabisa...wakati unaanza choko choko wanakujaza upepo wewe.....ukiwekwa korokoroni wanandelea halafu baadae wanakutoa sadaka...mwishowe unatoka ndani ukiwa na kipilipili cha ndevu...dred...na ukitembea kizombi zombi...

Haya mambo ya artivist kwa tanzania bado...wala ctaki mbwembwe kabisa...wasaliti wapo wengi mnoo
 
Awamu hii kweli inanyoosha haswa.. hata hawa bado wanyumba yumba!!!.. yupo nyumbani kwake.. wamusaidie kulipa.. wanyamaze.. walitaka awe huru na ameachiliwa muda wao walikuwa wakitamani kumutumia ili kupiga ramli zao juu ya Tanzania.. kuichafua tu nchi yetu
 
Haya mashirika yalikuwa wapi yasipaze sauti kuwa wote..mpaka kabendera yanamkuta yote haya...kijana kaenda mzuri/HB kabisa katoka kama teja...utadhani alikuwa anakula ngada huko ndani...

Of this organisation decides to stay with you...iwe ni mwanzo mpaka mwisho...siyo kuzungumzia wakijisikia au wakipata paltform ya kujibaraguza...

Of this realy care wamlipie hiyo fine...is believe this have mpunga wa kutosha..
Ovaaaa
 
Awamu hii kweli inanyoosha haswa.. hata hawa bado wanyumba yumba!!!.. yupo nyumbani kwake.. wamusaidie kulipa.. wanyamaze.. walitaka awe huru na ameachiliwa muda wao walikuwa wakitamani kumutumia ili kupiga ramli zao juu ya Tanzania.. kuichafua tu nchi yetu
Naomba unisaidie kuelewa, ameichafuaje nchi? Kipi alisema ambacho kimeichafua nchi?
 
Egypt kuna Mwandishi wa Aljazeerah yupo ndani unaenda Mwaka wa nne bila ya kufunguliwa Mashtaka na wameufyata hao Waandishi

Kwny kila Habari ya Aljazeerah wanapitisha utepe wa habari hiyo kwa chini.

Kabendera amekiri Makosa na amepata Msamaha na huruma ya Rais kwa kulipa faini japo ni Waandishi hao hao walikuwa wanakejeli Sheria ya kukiri kosa kabla ya kupitishwa.

Waliomtuma na kum pump Kabendera walikaa Kando

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee umeanza vizuri ila ulivyochanganya lugha me nimeshindwa kuelewa kwanini usiandike kiswahili all the way ? OF THIS REALY, na IS BELIEVE THIS sio sawa kabisa mkuu


Sent from my iPhone using JamiiForums
Baharia tunawasilisha kwa huku shirika watendaje watu wengi wanaelewa zaidi kidhungu...
 
Ki
Duh "utadhani alikuwa anakula ngada"!
Kibongo bongo ukitoka ndani kwa hilo unayokuwa nayo tu inabidi familia ikupeleke kwe rehabilitaion centre...hebu mcheki anko ruge..sethi...wapo kama wamedata sasa hivi..

Jela ya bongo siyo ni sehemu hatari sana kuishi...
OVAAA
 
Kilicho tokea kwa huyu Eric hakika kitazidi kuitangaza nchi yetu huko kwa wenzetu wanao heshimu haki za binadamu.

In God we Trust
 
Hilo genge naona limeyeyuka tayari
Hilo shtaka la kuendesha genge la uhalifu wamelitoa wapi?Hilo genge ambalo alikuwa analiongoza liko wapi?Mambo ya kubambikiziana kesi haya!

In God we Trust
 
Baada ya kupiga ban Bashite asiingie kwao, sasa wanaandaa hati ya mashitaka ili genge lenu mkafikishwe icc ili mfundishwe jinsi ya kutawala
Awamu hii kweli inanyoosha haswa.. hata hawa bado wanyumba yumba!!!.. yupo nyumbani kwake.. wamusaidie kulipa.. wanyamaze.. walitaka awe huru na ameachiliwa muda wao walikuwa wakitamani kumutumia ili kupiga ramli zao juu ya Tanzania.. kuichafua tu nchi yetu

In God we Trust
 
Kijana naona unamkufuru mungu, jitahidi kuwa muoga kwa mungu maana jera haikujengwa kwa watu fulani tu maana hata wewe ni mfungwa mtarajiwa. KITAULO,

In God we Trust
 
Back
Top Bottom