Amnest ya mafisadi yamshangaza Magufuli!

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
6,518
2,000
Katika kikao cha Dpp kilichoitishwa Ikulu leo ili kuwasilisha idadi ya maombi ya watuhumiwa walioandika barua ya 'marejesho' ili wajinasue imemshangaza rais!

Hii imetokana na mwitikio mkubwa wa watuhumiwa kuandika barua kwa Dpp za kuomba msamaha na kurejesha fedha walizotuhumiwa kukwapua.

Amesema hakutegemea kusikia idadi ya watuhumiwa 467 waliopokelewa maombi yao na wengine ambao barua zao zimechelewa kuwasilishwa kutokana na sababu mbalimbali, wote hao wamechangamkia hiyo fursa adhimu.

Kaeleza huo 'mchezo' hautaendelezwa baada ya siku ya leo, kuendelea mbele, watakao ucheza sasa wataibeba misalaba yao kupitia mahakama.

Hautatolewa tena msamaha 'kabila hiyo' na wote watakao bainika sasa watabanwa moja kwa moja na sheria za mafisadi na wahujumu uchumi zilizopo.

Kasema kuwa kama mtu anapotoshwa aidha na mawakili ili aendelee kukamuliwa pesa, shauri yake.
Nafasi hii ya kupitishwa kwenye tanuri la moto na kisha kutokea kwenye tundu la sindano ni moja na ni ya mwisho.

Kweli nchi hii ilikuwa na wapigaji jamani!
Hivi ukiwapanga foleni kuanzia posta, si watafika hadi station kabisa, Dah!

Tunawatakia msamaha mwema na wenye kuleta maridhiano.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
8,449
2,000
Hii miradi mikubwa imeanza kumchanganya mzee wangu

Maji yako shingoni! Pumzi inaelekea kukata. Alidhani ataimaliza kirahisi hiyo miradi yake kupitia dhuluma ya kutowapandisha watumishi wa umma madaraja yao na pia kugoma kuwaongezea mishahara na incriment zao za kila mwaka.
 

ujoka

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
2,360
2,000
Kama ulikwiba na deep down unajua ulikwapua au ulihujumu but unauhakika kabisa si jamuhuri wala awaye yote mwenye sensible and tangible evidence za kukutia kukutia hatiani so unaamua tu kukaza hata offer kama hii unaidindia tu japo moyo wako unakushudia kwamba wewe ni muharifu .

Hapo unakua unatenda dhambi ya pili na hii ni mbaya kuliko ile ya kwanza hii inaitwa sin against your self . .
Maana ninauhakika kabisa hapo hakuna alieko mjengoni kimakosa
 

Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
9,088
2,000
Na hata afanye nini, pesa kamwe hazitamtosha. Akubali miradi yake ya zima moto iende taratibu tu kama wenzake walivyoiendesha.
 

Levels baby

JF-Expert Member
Sep 26, 2019
831
1,000
Maji yako shingoni! Pumzi inaelekea kukata. Alidhani ataimaliza kirahisi hiyo miradi yake kupitia dhuluma ya kutowapandisha watumishi wa umma madaraja yao na pia kugoma kuwaongezea mishahara na incriment zao za kila mwaka.
Kuna mingine mkuu wa inchi inabidi atemane nayo mana itamtoa damu na hachelewi kusitisha mishahara ya watumishi baadhi ya miezi
 

Njemba Soro.

JF-Expert Member
Oct 5, 2013
1,619
2,000
Huyu boss anjitahidi tuwe sawa lakini watumishi wanamuangusha mno. Hii ni shida maana hata kelele za ndege ndege ndege naona zinazimika kimya kimya.
 

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,465
2,000
Asee nyie watu wa serikalini ndio mnamhujumu mh Rais.
Ninatamani watu kama nyie mshughulikiwe vilivyo.Wewe unafurahia nini miradi kuchukua muda mrefu kama siyo kutafuta fursa za kupiga dili?
Ninasikitishwa na sana na aina hii ya watu
Na hata afanye nini, pesa kamwe hazitamtosha. Akubali miradi yake ya zima moto iende taratibu tu kama wenzake walivyoiendesha.
 

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,370
2,000
Naimani kunawatu wakitoka mjengoni wanahamia kwa jirani because hawana iman na kilichotokea
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
8,449
2,000
Miradi yake ama miradi ya watz...

Hiyo ni miradi yake maana hata kwenye ilani ya chama chake ya mwaka 2015, haipo! Kwenye hiyo ilani kuna milioni 50 kwa kila kijiji, kuboresha maslahi ya wafanyakazi, nk. Yote hayo kapiga chenga!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom