Amkimbia mume wake kisa kachoka kumuuguza, amuachia mtoto 'alilazimisha talaka'

sio kwa mke hata ndugu pia ,nilipataga mtihani mkubwa lilikuwa jaribu kubwa sana,mama yangu mzazi akanikataa akawa ananikimbiza kwa buraza,mke wa buraza akawa ananilinda sana hanisimangi,ila nikienda kwa maza kejeli mateso tatizo linakuwa kubwa zaidi,nikawa sina uelekeo wowote mademu wakawa wananipenda pamoja na tatizo langu mama akawa anawaambia huyu hamna kitu ,ila madem walikomaa wakataka kuolewa na mimi tu,walikatishwa tamaa wakaolewa pengine hata dingi alikimbia,mungu si athuman akaingilia kati serikali ikanitibu bule nikapona.nikawa naishia kuosha vyombo kwa br kabla ya hapo nilikuwa na miliki aset ya viwanja 4 ,nilichofanya nikauza kimoja .nikapata kianzio ,haija pita mwaka ni kapata kazi,kwa fb wao wenyewe wanashangaa wakati nilikuwa mtu kutengwa ndani,nilipata kazi kupitia fb kwani kitaaluma ni phamasia, sasaivi mama ananiona mtoto natamani kumunasa vibao.weken akiba ya aset kwa maisha yenu yaabadae kwani inafikia ukipata majalibu makubwa hata ndugu wanakukimbia.NB kupitia jalibu yangu nimejifunza me
Ni hivi Mzee Huwa anasema wanawake wote ni Washenzi awe mama,Mke,dada sijui nani wote ni wapuuzi ishi nao Kwa tahadhari,kitu pekee wanachojali kwao ni Mali.
 
Kweli Duniani hakuna fomula. Mm nimeshuhudia mke akipambana na mume aliyeparalyse miaka 7 huku ndugu wakituma salamu tu za vipi leo kaamkaje?

Yule baba ni kichwa tu ndo kilikuwa kinafanya kazi, kuanzia kunya mpaka kula ni yule mke alisimama naye mpaka kifo chake.
Tumia lugha ya Staha
 
Mwanaume hakikisha unawekeza Nguvu zako kwenye Kutafuta Pesa Sio kwa Mwanamke.

Uwe na pesa ya Familia na pesa Yako pembeni maana Kuna Siku yaja huyo mwanamke unaejifanya kumpenda na kumjali kuliko unavyojijali wewe na ndugu zako atakuja kukutelekeza baada ya kufulia.

Binafsi sijawahi muamini mtu anaitwa mwanamke,ona huyu sio tuu amemtelekeza mume wake Bali kamuachia na mtoto huku akijua ni mgonjwa.
---

AMKIMBIA MUME WAKE KISA KACHOKA KUMUUGUZA, AMUACHIA MTOTO 'ALILAZIMISHA TALAKA'

Sadiki Mohamed Mkazi wa Buguruni kwa Mnyamani jijini Dar es Salaam ambaye yupo Kitandani kwa miaka nane sasa kwa tatizo la kupooza mwili, amejikuta katika mazingira magumu zaidi baada ya kumuacha mke wake kwa talaka ya mdomo kwa kulazimishwa na mke huyo kwa madai ya kuwa amechoka kumuuguza.

Sadiki ambaye mwaka jana (2022) kupitia mahojiano maalum na Mwandishi wetu @hamisimguta Sadiki alisema alipata tatizo hilo ghafla akiwa nyumbani kwake Majohe, jijini Dar es Salaam alipokuwa akiishi kabla ya kuuza nyumba yake kwa ajili ya matibabu, amesema hadi sasa hajapata mwarobaini wa tatizo lake kwakuwa misaada inayomfikia inaishia kutibu vidonda vilivyotokana na kulala kwa muda mrefu, na kugharamia chakula.

"Mkewangu aliniambia live kabisa kwamba amenihudumia anaona siponi, anajitesa na yeye bado ni msichana anataka akatafute mtu mwingine wa kuishi naye, alikuja na Mama yake mdogo ikabidi nimpe talaka," amesema Sadiki.

Wasafi Media
FACT
 
Hiyo inaitwa nguvu ya maamuzi, yanaweza kuwa na matokeo mabaya au mazuri, na hili linagonga pande za zote, mipango ya kila mtu iwe katika msingi wa Mungu ili hata maamuzi mabaya yakija Mungu akulinde nayo.
 
Kwamba baada ya kukaa naye miaka 8 akae naye milele? Pumbavu kabisa, hana ndugu wakusaidia, ukute wakati akiwa na kazi alikuwa tia Maji matumizi!

Hivi mnafikiri hawa single Mama mnaowasimanga kila siku walipewa mimba na kina Dada? Ni sisi sisi wanaume, ila kelele na lawama kwao.

Miaka 8 ni mingi, na kama kachoka, kachoka tu, hakuna la kumlaumu, kafikia mwisho, kaona bado ni mdogo na ana maisha ya kuishi, miaka 8 sio mchezo, kafanya sehemu yake vizuri.
So, you would do the same if it's were you ,
 
I am not a woman, I do not know how to be a woman, but I support that.
Hio scenario inaweza kumkuta mtu yeyote kwasababu ni ugonjwa hauchagui jinsia.

Nilichomaanisha ikiwa mkeo amekutwa na hio hali je na wewe utafanya kama alivyofanya yeye ,kwa Sababu ulizozitaja
-kumuuguza kwa muda mrefu
-kuchoka,
-kutafuta mtu mwingine wa kuendelea nae maisha.
 
....
Angeongeza wake 3 zaidi wamuuguze kwa hela ya chipsi kuku si dini yake inamruhusu? Analalamika mke mmoja kumtelekeza wakati angempa talaka na kuoa wake 4? Kama yote yameshindikana aache tu kulalamika sababu Allah kasema NO kwa hiyo imebaki akae mkao wa kuaga dunia.
Umeandika pumba....rudia kusoma..!!
 
Idadi ya wanaume wanaowatelekeza wake zao wanapougua ni kubwa zaidi. Hapa umetumia ubinafsi. Kama wewe ni mfuatiaji wa vyombo vya habari utakuwa umeshakutana na wanaume wengi waliowatelekeza wake zao kwa sababu ya wake kuugua au kuzaa mtoto mlemavu. BTW hili ni tatizo la uongozi wa nchi zaidi kuliko tatizo la huyo mwanamke. Watu wanaweza wasione uhusiano wa uongozi bora na tatizo la huyo mgonjwa lakini nchi yenye kila aina ya raslimali ilitakiwa iwe na uwezo wa kuwatunza wagonjwa kama hawa kwa kuwapa allowance kila mwezi.
Point yako ya mwisho hapo well said 👏 👍
 
Kweli Duniani hakuna fomula. Mm nimeshuhudia mke akipambana na mume aliyeparalyse miaka 7 huku ndugu wakituma salamu tu za vipi leo kaamkaje?

Yule baba ni kichwa tu ndo kilikuwa kinafanya kazi, kuanzia haja kubwa mpaka kula ni yule mke alisimama naye mpaka kifo chake.
Wanawake huwa wanapambana sana aisee. Hata huyu kajitahidi sana, miaka 7+ sio kazi ndogo.
 
Back
Top Bottom