Amitabh Bachchan ashinda tuzo ya Bollywood

explicity

JF-Expert Member
Oct 9, 2015
207
140
8f644d39136c2838b34aae173b0d72a5.jpg


Nyota wa filamu za Bollywood Amitabh Bachchan na Kangana Ranaut wameshinda mataji makuu katika tuzo za kitaifa za filamu nchini India.

Bachchan alishinda tuzo ya muigizaji bora kwa jukumu lake katika Piku huku Ranaut akiwa muigizaji bora upande wa wanawake kwa filamu ya Tanu Weds Manu Returns.

Tuzo ya filamu bora lilichukuliwa na Bahubali huku Sanjay Leela Bhansali akijishindia mwelekezaji bora wa filamu ya Bajirao Mastani.

Tuzo hizo hutolewa kila mwaka na serikali ya India.

Hiyo ni tuzo ya nne ya Bachchan.Alijishindia tuzo ya muigizaji bora mwaka 1990,2005 na 2009.
 
dah huyo mzee nuksi, lakini heshma anayoipata india haifikii ile anayoipata sharukh khan
 
Back
Top Bottom