Amiri Jeshi Mkuu Kikwete - Pana ukweli hapa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amiri Jeshi Mkuu Kikwete - Pana ukweli hapa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Sep 21, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  [​IMG] Amepeleka majeshi Pemba tokea mwanzo wa Ramadhani hadi leo ,wakitesa ,wakiwapiga watu mabomu ,kumbe Kikwete nae anamuogopa Mwenyezi Mungu ? Basi ajue madhila waliyopatishwa WaPemba na jeshi lake ni kosa ambalo linalomuhusu katika kutimiza ibada zake, nadhani anafahamu maana ya kuwa kiongozi muadilifu na haswa anapofikia kumkabili Mwenyezi Mungu ni laana kubwa ikiwa vitendo na ibada ni tofauti ,hivyo ajisahihishe huyo anae Muabudu hapo kwenye picha anayajua yote ya siri na ya dhahiri ,kuvaa koti kubwa na ukanzu wa kiarabu hakutamfanya yeye awe bora au mswafi mbele ya Mwenyezi Mungu wakati alipeleka jeshi na mapema ,akijua fika kuwa huu ni mwezi wa ibada ,kama angesimamia daftari la kura na kuhakikisha wananchi wote wanaandikishwa ,leo hapo alipo si angelikuwa mtu wa maana mbele ya Mwenyezi Mungu. Lakini wapi wanaongozwa na shetani wawepo kwenye uongozi na husahau kama kuna aliewaumba na iko siku marudio ni kwake na ndio hapo kama tuonavyo.
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Msomeeni فتوى (fatwa)!!
   
 3. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2009
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kaka pana ukwelihapo?
   
 4. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mwiba
  Tatizo la Mungu na ubaya ni maswahiba. Ndio maana wabaya bado wanadunda. Na hawa jamaa wameshagundua hakuna mungu kwa hiyo wanakandamiza kwa kwenda mbele. Hizo sala geresha tu, namna ya kuwapata wapigakura. Maskini wa Tanzania ndio bado wanaamini kuna mungu
   
 5. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe Mwiba,

  Kupiga watu wanaojiandikisha kwako wewe RUKSA siyo?? Kuchoma nyumba za watu kwa kuwa wanajiandikisha wewe waona raha kabisa au vipi??? Acha unafiki wa kumjua Mungu huku unashabikia maovu ya kuwaonea wasio na hatia. Ulitaka uendelee kuwachomea watu nyumba na sasa jeshi limekudhibiti unaanza kulalama, mwone. Usijifanye muislam kumbe pagani na kafir namba moja wewe. Jeshi na liendelee na kazi ya kulinda amani tu Pemba, kama unaona soo basi kimbilia tena Mombasa na usirejee Pemba asilani. Tena usiendelee na agenda hii maana tumechoka na chokochoko zenu wapemba safari hii mkizidisha huo unyambilisi wenu mtakiona cha moto xlkjuyyxzvf mkubwa we.
   
 6. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mwiba,

  Nakuunga mkono ila kuna wakati nadhani tusiingize religion sana kwenye politics ama leadership.Jeshi lilipaswa kuwepo ku-maintain law and order.Sidhani kama hata kama daftari la wapiga kura lilikuwa na tatizo kiasi cha kwamba wananchi wa Pemba walete vurugu zote zile kama siyo uchochezi wa hali ya juu wa CUF na uzembe na kutokuwajibika kwa baadhi ya Wajumbe wa ZEC.

  Law and order was necessary ili kulinda baadhi ya wale ambao wangeumizwa kwa vitendo vya wenzao!
   
Loading...