Mzee Mkira,
Don't get me wrong. Hakuna ubaya kwa Serikali kuwasomesha watu wake nje. Hata hivyo, Serikali zinazoongozwa na watu waliostarabika kwa manufaa ya nchi, wanakuwa na utaratibu unaoeleweka na kuheshimiwa. Mfano, kumsomesha mtu katika fani ambayo nchi inaihitaji (siyo inaitaka, manake kuna needs and wants), na wakati huo huo hakuna chuo kinachoweza kutoa huo utaalam katika nchi husika.
Kifuta machozi kwako Mzee Mkira, ni ukweli kuwa mali ya dhuluma uenda kwa dhuluma. Mpango huu ulihusisha makundi matatu 1. Watoto wa masikini waliokuwa wajanja 2. Watoto wa matajiri walioweza kuhonga 3. Watoto wa matabaka ya watawala na viongozi wa mashirika ya Umma. Pia ili ufanikiwe, ilitakiwa uwe na vitu viwili. 1. Fedha ya kuhonga 2. Connection-mtu wa kukupigia kifua. Ni watoto wachache sana wa matabaka ya watawla na viongozi wa mashirika ya Umma walioweza kumaliza shule kwa fedha ya wizi na udanganyifu.
Mtoto wa Sumaye uliye mtaja (ingawa sipendelei majungu), anaangukia kwenye kundi la mali ya dhuluma. Habari za uhakika kutoka Marekani, zinasema kuwa huyu kijana alikuwa katika jimbo la Texas katika shule moja ya weusi inayoitwa Texas Southern University. Aliingia shule muhula mmoja, lakini hakumaliza pia. Miaka yote alikuwa anapiga mzigo na kuzulula mitaani. Ilipokuwa inafika wakati wa ubalozi kutuma fedha kwenda shuleni, alikuwa yuko mstari wa mbele kwenda shule na kudai apewe fedha hizo. Baba yake alikwenda kwenye ziara huko Marekani iliyokuwa inanungunikiwa kwa kutumia mamilioni ya fedha. Alitembelea Texas na kukutana na mwanae. Aligundua kuwa mtoto asomi shule. Mama yake alifunga tena safari nyingine na kumrudisha nyumbani, kabla ya kumpeleka India. Sasa sijuhi ni yuleyule wa India ndiye yuko BOT au ana wawili.
Story hii ni ya mtoto wa Sumaye, lakini inafanana na asilimia zaidi ya 80 ya watoto wa matabaka ya watawala na viongozi wa mshirika ya Umma. Afadhali mtoto wa Sumaye alirudishwa na wazazi. Wengine walikuwa jela na wengine walirudishwa kwa lazima. Bad news hapa ni kwamba fedha ya walipa kodi, au ya mikopo ambayo tunakuja baadae kulipa kwa riba kubwa ilikwisha potea na haikuzaa matunda.
Kumbuka Raisi Kikwete wakati anaaga wizara ya mambo ya nje, aligusia suala zima la kifedha wakati Mkapa anachukuwa madaraka mwaka 1995. Alisema Balozi zetu zote nje zilikuwa hazina fedha na tulikuwa tunadaiwa. akamuomba Mkapa kutumia fedha ambazo Serikali ya Uganda inatulipa kufidia vita ya Nduli Amani (si maajabu hayo-eti waganda wanaopigana kila siku wanatulipa. bajeti yao kwa sasa inajitosheleza, sisi tunategemea wafadhili. Eti tunawazidi amani), hiyo fedha ndiyo ilikwenda kulipia mabalozi yetu.
Nikitumia style ya Raisi wa Iran katika Epistle yake kwa Bush, just an educated guess; Kwa kutumia hotuba ya Kikwete, Mkapa alipoingia madarakani, serikali ilikuwa imechacha kichizi. walikuwa na wanafunzi wengi nje waliokuwa wanawalipia kuzidi uwezo wa fedha walizokuwa nazo. Shule zilikuwa zikiwasumbua ofisi za balozi zetu huko UK na USA. Hali halisi ilipowakumba. Mkapa akaamua kusitisha zoezi zima. Waliokuwa wamepata kumaliza shule, wengi wao walikuwa ni watoto wa maskini lakini wajanja na baadhi ya watoto wa matajiri waliokuwa na connection.
Toka hapo, Serikali yetu ikawa haisomeshi tena watu wake nje kutoka katika mfuko wake. Zilizobaki zilikuwa ni zile za kiushikaji kama za watoto wa wakubwa kweli kweli. Hata hivyo, zikabakia zile unazosikia kwenye magazeti kuwa Serikali ya nchi fulani imetoa Scholarship kadha wa kadhaa ambazo zinapitia Serikalini. Kuna nyingine ni Scholarship za kweli, lakini kuna nyingine ni mikopo. Kama unavyojua masharti ya mikopo, Nchi tajiri kama marekani, wakikupa mkopo lazima ukutokee puani. Wanakuonyesha fedha kwenye karatasi, alafu wanasema lazima watu wako waje kusoma kwenye vyuo vyetu.
Mkiwa na viongozi mliowachagua ninyi, wanapashwa kukataa. Mzee ES anasema kule Marekani weusi si chochote wame sell out. Sasa swali la kujiuliza, ni jicho gani analotumia Bush kumuona mweusi wa Marekani ame sell out, lakini hilo jicho likamuona mweusi ambaye ni Raisi wa Tanzania, haja sell out. Ukweli ni kwamba kwa Bush, mweusi ni mweusi tu uwe Raisi wa Kenya au Jesse Jackson. Thamani yako inapatikana pale anaponufaika na weusi wako. How? ukitaka kupiga picha na Bush, nchi yako inapewa mkopo wa kuwasomesha watu wako, kwa masharti kuwa lazima waje kusoma Marekani ili zile fedha unazoziona kwenye karatasi ziende kunufaisha vyuo vyao.
wanapata faida mara mbili. 1. Vyuo vyao vinapata fedha za kujiendesha. 2. Nchi yao inapata faida kutokana na riba tutakayo lipa. kumsomesha mtu mmoja shule mpaka akamaliza, inaweza ikawa kwa makadilio ya dola elfu 30 mpaka sabini kutokana na kitu anachokuja kusomea (eg. music, what's up man?). Hilo deni la let's dola elfu 40 pamoja na riba yake unaweza kukuta tunailipa dola laki nane na tunafikia sehemu tunasema tumechoka deni halilipiki. Sasa wanakaa na kusema haya tunakusamehe deni, tunaanza kukopa upya.
Kumbuka, hata siku moja hawasemi Serikali imekopa. Serikali imepewa msaada wa dola kadha wa kadha. Mara chache sana inakuwa misaada kweli, lakini wakati wote ni mikopo. Soma magazeti kila siku. Serikali imepata msaada, mara chache watasema serikali imepata mkopo. lakini baada ya miaka kumi, unaambiwa tunadaiwa sana. Sasa hiyo fedha mmekopa lini wakati ilikuwa ni msaada siku zote. Utajaza mwenyewe....
Ndiyo maana kila nikisikia kiongozi yeyote wa nchi ya Kibepari anamsifia Raisi yeyote wa nchi masikini nasikia moyo unaniuma. Hotuba ya kiongozi wa nchi tajiri lazima uilipie gharama. Ilikuwa tofauti wakati wa vita baridi kati ya Urusi na Marekani. Wakati ule walitaka wawasomeshe bure ili muwe mapepari. Sasa hivi noma, yaani ni choo kijizi. Nashangaa kwa nini viongozi wetu hawaendi China, Russia, India, Turkey, hawa jamaa wanawasomesha vijana wetu bure kabisa bila masharti ya kukopeshwa. huu ndiyo uzalendo. Mzalendo ni yule anayekutakia mema. Japan imekuwa nayo ikitusaidia kwa elimu lakini vijana wetu wengi wanasomeshwa mambo ya vidudu dudu fulani vinatembea na kufanya kazi kama binadamu, sijuhi vinaitwa Robots au robotics (whatever). Sasa hapa Manzese kwa mfuga mbwa havitusaidii, labda kwa kutafuta ajira huko majuu na wakamwaga mapesa nyumbani ili na sisi tufungue baa za kuwanywesha ndugu zao. Lakini kuna Electronics etc.
Unyama wa Ubepari hauishii hapo. Mara nyingi, wanakuambia masharti ya mkopo huo wa shule, ukimaliza lazima urudi nyumbani. Kwa kisingizio cha kusaidia nchi yako. Ukweli ni kuwa hawataki ufanye kazi na upate fedha za kurudisha nyumbani. wanataka mbaki maskini tu. Wao wanataka fedha iingie tu. Ndiyo maana nawasifu sana vijana wa kijiweni hapa kwetu Manzese waliokuwa wanachonga Bank statement na kupeleka ubalozini. Maafisa wa ubalozi walikuwa wakihesabu zile Bank statements na kusherehekea kuwa wanaliingizia taifa lao fedha, kumbe zile ni fedha zinazotoka kwenye taifa lao kuja nyumbani Tanzania.
Hawa vijana ni majemedari na wzalendo wa kweli kuliko matabaka ya watawala yanayotuingizia kwenye mikataba ya kihuni kama hii. Hawa vijana wanatuma fedha nyumbani kwa kupitia Western union. Ingawa muhusika anapewa fedha ya madafu, lakini Serikali inapata dola bwana. Fedha ndogondogo wanazotuma watanzania zinaliingizia taifa pato la fedha za kigeni. Tukifanya utafiti, unaweza kukuta hizi fedha zinachangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa na bajeti ya nchi. Si hilo tu, wanajenga vibanda majumbani kwao kutokana na kupigika na schedule, hivyo kutoa viajira vidogo vidogo. Wanasomesha ndugu zao. wanawatunza wazazi wao.
Wazazi na ndugu zao wkitumiwa fedha, wanakwenda kununua vitu na kusababisha mzunguko wa fedha nchini kwetu. ukichunguza kwa makini, utagundua kuwa vijana wanao fanya hivyo, ni wale waliomaliza darasa la saba, kidato cha nne na sita. Hawa wangekuwa na sisi hapa kwa mfuga mbwa, wangekuwa wameliwa na funza. Ukijumlisha hawa vijana duniani kote waliko, na ukajumlisha vijifedha wanavyotuma na viajila vidogovidogo wanavyotoa, kwa ujumla wao, utakuta wanatoa ajira kwa watu wetu kuzidi serikali za mikoa mitatu au minne ya hapa nyumbani inavyotoa ajira kwa watu wake.
Bahati mbaya, wasomi wetu wanasubiri fedha za wafadhili ili waweze kufanya utafiti. na sisi ambao hatujaenda shule, tunatumia busara za wahenga ili kutambua umuhimu wa hawa vijana. Ili swala nimeliingiza kwenye mada hii ya Jamal kwa sababu linahusu uzalendo na asili ya mtu. Hawa ndiyo wazalendo kweli kweli (siongelei wale wanaoiba vile vidubwasha vya computer). Hakika tungejua kwa utafiti umuhimu wa hawa vijana kwa taifa letu, tungewapa hata hizo wanazolilia sijuhi dual nini tena? ehe, manake wape uhuru wa kufanya biashara, kuingia na kutoka nchini, kuwekeza katika nchi yao wakati wana uraia wa nchi nyingine ili wasije wakalipishwa kodi kubwa kama wageni (by the way kuna tax holidays; so who cares anyway?). Hawa ndiyo wawekezaji wa kweli. Nikama wachezaji wa timu za kulipwa walioko nje, na mara kwa mara wanarudi kulisaidia taifa lao wanapotakiwa.
Mimi naona tungewapa msaada wote wanaohitaji ili kuendeleza taifa letu. Labda nisiwe Naive kama alivyonishauri Mzee ES kwa sababu upande mwingine wa shilingi kuna madhala ya hiyo Dual thing. Uzalendo usiniponze.