AMIMI USIAMINI - Hii ndiyo fomu ya kuombea viza ya kuja Tanzania!

Mtoa mada naona anataka kuturudisha mwaka 1992 ambapo hata kwenda kenya au uganda lazima uwe na visa, jiulize kwa nini SADC na EAC tumefika mahala tukaondoa visa???? Lengo ni kurahisisha movement ya wananchi wetu.

Kwa hiyo form kuwa simple ni njia moja wapo ya kurahisisha mambo....
 
hivi tanzania ni nchi serious kwa mawazo yako??

Mkuu I stand to differ with you, what do you mean unaposema ni nchi serious? Sema viongozi hawako serious.

Hebu mpeni Kagame au Dr Slaa hii nchi muone mambo yatakavyokwenda.
 
The country where impossible things are possible and illegal things are legal, the country where short things are tall and where black things are more white!!!!!!!!!!!!!​

 
Hii kitu mbona siku nyingi inatumika, na kama unatoka Europa hii hujazwa mkitoka Nairobi kuja Dar, nilishawahi kukutana nayo siku moja. Sijui ndo nn sasa, unaomba VISA ukiwa tayari uko TZ na sizani kama wote waga wanaijaza hii form. Kazi kwelikweli
 
kwani Tanzania kuna wasomi? kuna wakiritimba. kuna mijitu ambayo yenyewe ili uwe na akili lazima uwe na cheti sio ufahamu wako. hii mijitu ndiyo ilileta sera ya kumpunguzia maksi mtoto aliyerudia mtihani kana kwamba kukata rufaa ya kufeli ni dhambi. hii mijitu yaani haiwazi hata moja jumlisha moja ni ngapi. na ndiyo tumeikabidhi nchi. DEGREE,MASTERS NA PHD UCHAAAAAARA! bora ya aliyeandika bongo fleva kwenye mtihani!
 
hivi, hiyo fomu imeanza kufanya kazi mwaka huu? Au mleta mada utuambie tusiyojua

Jamani, toka lini imekuwa tija kulalamika pasipo kuonyesha njia? Fomu hii pengine inamapungufu, yasemeni na mueleze mnataka yarekebishwe vipi. Kutaka fomu yetu iwe kama za wengine ni uvivu wa kufikiri. Hii inaonyesha tusivyodhamini vyetu na mara zote kudhani vya wengine ni bora kuliko vyetu.
ANGALIZO: Fomu haimuingizi mgeni nchini, kadhalika visa. Waulize uhamiaji kama wanaingiza nchini kila mgeni mwenye visa. Niwajuavyo mimi hao ni security organ na ujazaji wa visa form ni hatua moja wapo tu katika screening, na sio final. Kama mnadhani yapo marekebisho waambieni ni yepi ili wayafanyie kazi na sio ili iwe kama za nchi nyingine!
kwa kuwa mie sijawahi enda hizo nchin nyingine sijui zilivyo hivyo hata kulinganisha sitaweza. Mlioenda huko tupasheni na sio kulalamika.
 
Back
Top Bottom