Mkuu mbona ingekuwa heri kama ungelikuwa unajaza yote, Siku moja nilifika hapo kumuombea rafiki yangu visa..tatizo likaja hakujua nini cha kujaza basi nikaenda mapokezi kuuliza nijaze nini hapa? kuna mama mmoja nimemsahau jina akaniambia hapo hakuna umuhimu wa kujaza.....sehemu yenyewe inahusiana na details za msafiri au muombaji wa visa, aisee nilicheka sana.
Nchi za wenzetu, unapewa VISA baada ya kujaza maelezo mengi sana mpaka yanachosha. Na wanataka kujua mpaka unakotarajia kufikia na zababu zinazo kupeleka kwao. Kwa form hiyo ya bongo ni cha mtoto na bado mtu anakwambia haina umuhimu na kama haina umuhimu ipo pale kwa ajili ya nini? Hata wafanyakazi wengine wapo tu kwa sababu waliambiwa wakaye hapo wangoje mshiko mwisho wa mwezi basi!! Wageni waje tu kuvuna shamba la bibi.
Hao waliandaa hiyo form nadhani ni wavivu wa kufikiri. Haiwezekani hiyo form iwe iliandaliwa na mtu mwenye uzalendo na nchi yake.
Tafuta fomu za viza za nchi zingine utapata jibu lako.
Mara nyingi huwa tunazungumzia namna ambavyo nchi ya Tanzania inaendeshwa katika utaratibu wenye kutia aibu na fedheha kwa taifa na wananchi wake na inastaajabisha pale unapotafiti aina ya watu wenye madaraka ukilinganisha na uwezo wao.
Atachment iliyopo kwenye mada hii ndiyo fomu raia wa kigeni anayojaza pale anapoomba viza ya kuja nchini kwetu. Ni ukurasa mmoja tu ambao sehemu anayojaza ni theluthi moja tu ya kurasa hiyo.
Kwa wale ambao mmewahi kuomba viza kwenda nchi zingine naamini mtaweza kulinganisha information unazotakiwa kutoa kuhusu wewe ni nani na unafanya nini, una mahusiano gani, viambatanisho muhimu, n.k.
Ukiangalia fomu hii unaweza sasa kuelewa ni kwa nini hapa nchini kuna raia wengi wa kigeni ambao hawakupaswa kuingia nchini, watu ambao wasingethubutu kuomba viza nchi zingine, lakini kwa vile serikali imeifanya nchi kuwa shamba la bibi kwa kupitia upumbavu wa namna hii, matokeo yake ni nchi kudharaulika.
Hii ndiyo fomu iliyobuniwa na wataalam wetu waliopo uhamiaji>
Jioneeni wenyewe!
Kwa nini unamtaka mtu mwingine akufanyie kazi ambayo wewe uliyeleta madai kwamba fomu hii haitupi habari za kutosha unatakiwa kutufahamisha?
Duniani kuna nchi nyingi sana, hizo "nchi nyingine" unazozizungumzia ni nchi gani? Nchi tofauti zina vigezo tofauti katika kupanga matakwa shurti ya fomu, utasemaje tu "tafuta fomu za viza za nchi nyingine"? Na kwa nini Mtanzania atake kupanga matakwa ya fomu ya viza ya Tanzania kwa kuangalia nchi nyingine? Utataka kutuambia na zile nchi zisizotaka kabisa mtu kuwa na viza nazo tuzigeze? Na zile zenye kutoza mamia na maelfu ya dola kama viza processing fee nazo?
Mbona hamjajibu swala la kusema kwamba nchi masikini inayotaka kukuza utalii haiwezi ku-afford kuwa na unnecessary and bureaucratic paperwork?
Hao vinara wa dunia wana ma "paperwork reduction acts", Marekani wamekuwa so bureaucratic kwa paperwork mpaka wametunga sheria ya kupunguza paperwork. Na hata hapo nasoma "The Economist" la wiki hii, gazeti linawabalasa Wamarekani kwamba moja ya mambo yanayosababisha uchumi kuwa stagnant ni bureaucracy na a Vogon-like overkill in paperwork kiasi kwamba, the Economists correspondent says in jest kwamba hiyo 800+ page Dodd-Frank Act hakuna mtu aliyeisoma yote outside of Beijing na huyo muandishi.
Hivi itasaidia nini kama utakuwa na ki booklet cha fomu za viza wakati watu wanauza pasipoti za bongo kama njugu? Si unaongeza gharama za uendeshaji balozi tu?
United States' economy: Over-regulated America | The Economist
Angalia jibu nililolitoa hapo juu muda wa 01.05 kwa Kibunango, nadhani unaweza kuona nini ninachozungumza. Suala si mlolongo wa paperwork ila ni jinsi fomu yenye isivyo ya kisasa kwa maana kwamba kwa mfano unalazimika kui-print na kuituma au kuipeleka kwa mkono ubalozini.
Fomu za utalii wa muda mfupi katika nchi nyingi hata zilizoendea zaidi ya kwetu nazo ni fupi tu
Singapore, Malaysia, Cambodia, Vietnam, South Korea, China, Japan, Ugiriki, Ureno, Indonesia, Urussi, Dubai, ....kote fomu ni page moja tu ama unagongea airport
Hamna cha ajabu hata kimoja kwenye hiyo form ya Tanzania
Nadhani ukizingatia kichwa cha habari cha uzi huu pengine utaona tatizo ninalozungumzia. Hii fomu si ya viza ya utalii tu, ni viza yoyote mtu anayokusudia kuomba ili aje Tanzania; ukiwa unakuja kibiashara, kitalii, likizo, n.k. unajaza fomu hiyo hiyo. Moja ya matatizo yaliyo wazi ni namna ambavyo hizo sehemu za kujaza zilivyo ndogo; zaidi tena hiyo fomu inaonekana aliyeitengeneza aliwaza kuwa viza huombwa na mtu mmoja mmoja tu. Chukua mfano familia moja kubwa yenye watoto wadogo inapohitaji viza kuja Tanzania, ni kwamba kila mtu atatakiwa kujaza fomu yake na kuifikisha ubalozini wakati angejaza mzazi mmoja tu fomu moja na kuorodhesha majina ya wote anaoambatana nao.
Mkuu ushasema fomu inajazwa theluthi moja tu sasa tatizo ni lipi kama na kila mtoto kwenye familia atatakiwa kujaza yake?
Kuna mtu amesema kuwa visa ya kuombea ukazi au biashara unatakiwa ujaze na form nyengine. Lakini wewe unapingana nae wazi
Wewe una uhakika kuwa karatasi ni hii hii TU hata kwa mtu anaeomba ukazi na biashara?
Fomu za utalii wa muda mfupi katika nchi nyingi hata zilizoendea zaidi ya kwetu nazo ni fupi tu
Singapore, Malaysia, Cambodia, Vietnam, South Korea, China, Japan, Ugiriki, Ureno, Indonesia, Urussi, Dubai, ....kote fomu ni page moja tu ama unagongea airport
Hamna cha ajabu hata kimoja kwenye hiyo form ya Tanzania
ninavyojua mimi ni kwamba ukiwa raia wa kigeni unalipia dola 100 pale airport bila maswali au longolongo, au hii kuomba visa imeanza jana?
Sijui kama umeiangalia hiyo fomu; niliposema theluthi moja nilimaanisha ukubwa wa section ambayo muombaji anajaza, theluthi nyingine ni matumizi ya ofisi na nyingine ndiyo ina nembo ya nchi, anuani ya ubalozi na vinginevyo.
Ipitie tena utaona kuwa wameweka aina za viza: Transit, holiday, tourist na business. Tovuti ya ubalozi wetu Uingereza inasema bayana kabisa kuwa fomu hiyo inatumika kwa viza zote. Sasa kwa mfano mtu anayekuja Tanzania kuungana na familia yake ambayo ilikuja kuishi huku anajazaje fomu hiyo?
angalia ya ethiopia na ya chinaMbona iko sawa tu na ya nchi zingine si unajua form nyingi ni za kudesa tu, ungeongelea utaratibu wa kupata visa ningekuelewa