Massenberg
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 1,173
- 1,370
Mara nyingi huwa tunazungumzia namna ambavyo nchi ya Tanzania inaendeshwa katika utaratibu wenye kutia aibu na fedheha kwa taifa na wananchi wake na inastaajabisha pale unapotafiti aina ya watu wenye madaraka ukilinganisha na uwezo wao.
Atachment iliyopo kwenye mada hii ndiyo fomu raia wa kigeni anayojaza pale anapoomba viza ya kuja nchini kwetu. Ni ukurasa mmoja tu ambao sehemu anayojaza ni theluthi moja tu ya kurasa hiyo.
Kwa wale ambao mmewahi kuomba viza kwenda nchi zingine naamini mtaweza kulinganisha information unazotakiwa kutoa kuhusu wewe ni nani na unafanya nini, una mahusiano gani, viambatanisho muhimu, n.k.
Ukiangalia fomu hii unaweza sasa kuelewa ni kwa nini hapa nchini kuna raia wengi wa kigeni ambao hawakupaswa kuingia nchini, watu ambao wasingethubutu kuomba viza nchi zingine, lakini kwa vile serikali imeifanya nchi kuwa shamba la bibi kwa kupitia upumbavu wa namna hii, matokeo yake ni nchi kudharaulika.
Hii ndiyo fomu iliyobuniwa na wataalam wetu waliopo uhamiaji>
Jioneeni wenyewe!