Amfuma mkewe akizini na mtoto wao, awaua

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
AMFUMA MKEWE AKIZINI NA MTOTO WAO, AWAUA

AMA kweli ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Firauni! Msemo huu unakwenda sambamba na tukio la hivi karibuni la mkazi mmoja wa Kijiji cha Nghoboko wilayani Meatu mkoani hapa, Stephano Mihilu mwenye miaka 60, kudaiwa kumfumania mkewe wa ndoa akifanya mapenzi na mtoto wao wa kumzaa.

Taarifa za kipolisi zilizotua kwenye dawati la Amani zinadai kuwa tukio hilo la aina yake lilitokea usiku wa Julai 22, mwaka huu ambapo baada Stephano kulishuhudia tukio hilo, aliwaua mama na mwanaye kwa kuwacharanga mapanga bila huruma.

“Jamaa aliporudi nyumbani, aliingia ndani na kukutana na tukio ambalo hakuwahi kulifikiria, alimkuta mkewe akifanya mapenzi na mtoto wao wa kumzaa, nadhani akili ilihama, akachukua panga na kuwacharanga wote mpaka walipokata roho,” alisema afande mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwani si msemaji wa jeshi la polisi.

HUYU HAPA KAMANDA WA POLISI WA SIMIYU

Akilizungumzia tukio hilo la kusikitisha na kushangaza, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Afande Salum Msangi aliwataja waliouawa kuwa ni Kundi Sita mwenye umri wa miaka 40, ambaye alikuwa mkewe na Boyani Stephano mwenye miaka 27 ambaye ni mtoto wao wa kumzaa.

Alidai kuwa, Mihilu alimkuta mkewe akifanya tendo la ndoa na mtoto wake wa kumzaa ndipo alipopandwa na hasira kisha kuwashambulia kwa kuwakata mapanga na baadaye kuwachinja.

Kamanda Salum alisema, baada ya mauaji hayo, mtuhumiwa huyo alikwenda mwenyewe kujisalimisha kwenye kituo cha polisi ambapo alikabidhi silaha alizotumia katika mauaji hayo ambazo ni panga na fimbo.

“Mihilu alitembea kuanzia saa 7 usiku hadi asubuhi kwenda katika Kituo cha Polisi cha Mwahuzi wilayani Meatu kwa lengo la kujisalimisha akidai kuwa hakutaka kuwasumbua wanausalama hao kwani yeye ndiye mhusika wa mauaji hayo,” alisema kamanda huyo.

WANANCHI WANALIZUNGUMZIAJE TUKIO HILO?

Wakizungumza na mwandishi wetu baada ya tukio hilo, baadhi ya wananchi wameonesha kushangazwa nalo huku wakieleza kuwa, kama ni kweli basi dunia inaelekea mwisho.

“Hivi inawezekanaje mama kufanya tendo la ndoa na mwanaye wa kumzaa? Au kuna mazingira ya ushirikina?” alihoji Juma Sagala wa Meatu.

Naye Mama Josephine, mkazi wa kijiji ambacho tukio hilo lilitokea alisema: “Hili tukio lina utata lakini kwa kuwa limeshafika kwenye vyombo vya dola, ukweli utajulikana na sheria itachukua mkondo wake ila limetushangaza sana..
GUMZO LA JIJI: AMFUMA MKEWE AKIZINI NA MTOTO WAO, AWAUA
 

Attachments

  • amuua.jpg
    amuua.jpg
    84.7 KB · Views: 140
Mama ana miaka 40, mtoto ana miaka 27, ni kweli huyo ni mwanae wa kuzaa, alizaa akiwa na 13 yrs? Basi mama ni malaya wa kutupwa
 
Huyo sidhani kama ni mtoto wa huyo mama! Atakuwa ni mtoto wa mke mwenza. Haya mambo usukumani yapo sana maana baba anaoa kibinti rika moja na watoto wake! Hapo akili mu-kichwa sasa!
 
dunia ndio inaelekea mwisho tulio nafamilia ,watoto, tumulilie Mungu atunusuru na hali hii ya kutokuwa na staha,utu nk
 
Kumbe mama alimtamani kijana wake....mmh binadamu tunazidi kwenda kubaya.
 
Kumbe mama alimtamani kijana wake....mmh binadamu tunazidi kwenda kubaya.

Akilizungumzia tukio hilo la kusikitisha na kushangaza, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Afande Salum Msangi aliwataja waliouawa kuwa ni Kundi Sita mwenye umri wa miaka 40, ambaye alikuwa mkewe na Boyani Stephano mwenye miaka 27 ambaye ni mtoto wao wa kumzaa.
yaani na ww dada unaamini ni mtoto wa kumzaa labda huko usukumani maana miaka 13 umezaa umezalishwa? hebu toa miaka ya mama 40 kwa mtoto 27 miezi 9 mimba miezi 4 kufumuliwa uro..
da magazeti wya udaku bwana
 
Mh hakika huyo sie mwanae wa kumzaa, lol
mh cku hz mtoto wa mwenzio mkubwa mwenzio....Mungu atusamehe tu duh....
 
Back
Top Bottom