Ametufanyia sherehe na msiba ndani ya mwezi mmoja

Ametufanyia sherehe na msiba ndani ya mwezi mmoja

HustlerD

Senior Member
Joined
May 15, 2021
Posts
131
Reaction score
437
Ndugu zangu,

Ama kweli hii dunia tunapita, binamu yangu wa kiume kapata mchumba, tukamsindikiza kuvalisha Pete na kutoa kishika uchumba, hiyo sherehe ndogo ikafaana kweli kweli, tukala na kunywa tani yetu, shemeji yetu alikua mjamzito pia,

Wiki iliyopita amepaki gari pembezoni mwa barabara kuu, anavuka barabara kwenda upande wa pili kununua matunda aliyokua anayapenda, ghafla kagongwa na gari kafariki [emoji24][emoji24]

Sehemu ile ile tuliyofanyia sherehe ndiyo hiyo hiyo tuliyofanyia msiba, unatamani kupiga hata yowe hadharani, unabaki kujikaza kiume, binamu nae kachanganyikiwa

Haya maisha haya , haya maisha haya, acheni tu, dada wa watu ndo kafa hivi kweli?
 
Sawa kuna mipango ya Mungu ila mengi yanayowakuta vijana leo hii ni ujuaji mwingi.

Ukweli ni kwamba mtu anapokaribia kuoa au kuolewa kiroho mwili wake huwa mwepesi kiuhalisia kila aina ya baya na ovu humuandama ni jukumu la wanaukoo au familia wa kila upande kuwafanyia vijana wao matambiko au kama imani yao hairuhusu wafanye sala kulingana na imani yao.

Ila sasa nikinyume kabisa na vijana wa kisasa uchumba watafanyia mjini bila kuwepo kwa wazazi na pia usipokuwepo mmoja kati yao mwenye msimamo ndoa pia itafanyika town na wazazi wataambiwa tu kama watu baki vile.

Pole sana kwa msiba mkuu
 
Poleni, haya maisha hayaeleweki. Kuna watu wanaishi vizuri sana, wengine wanakumbana na balaa kama zote.
 
Ndugu zangu,

Ama kweli hii dunia tunapita, binamu yangu wa kiume kapata mchumba, tukamsindikiza kuvalisha Pete na kutoa kishika uchumba, hiyo sherehe ndogo ikafaana kweli kweli, tukala na kunywa tani yetu, shemeji yetu alikua mjamzito pia,

Wiki iliyopita amepaki gari pembezoni mwa barabara kuu, anavuka barabara kwenda upande wa pili kununua matunda aliyokua anayapenda,
Ghafla kagongwa na gari kafariki [emoji24][emoji24]

Sehemu ile ile tuliyofanyia sherehe ndiyo hiyo hiyo tuliyofanyia msiba, unatamani kupiga hata yowe hadharani, unabaki kujikaza kiume, binamu nae kachanganyikiwa

Haya maisha haya , haya maisha haya, acheni tu, dada wa watu ndo kafa hivi kweli..?
Kwa experience watu wengi wenye magari ugongwa Sana kwa hali hiyo anapaki gari upande mmoja anavuka upande mwingine mara nyingi huwa siyo wasikivu sijui kwa nini. Maafa Kama haya utokea Mara nyingi. Hile hali ya kutoka kwenye gari yako unafikiri wewe ndo uko barabarani tu, wasomi wengi na matajiri wamekufa kiivyo.
 
Dunia mitihani.

Poleni kwa kupoteza nguvukazi ya jamii na Taifa.

-Kaveli-
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom