Ameshajua nampenda, basi ndio ananikomoa

Ameshajua nampenda, basi ndio ananikomoa

....Dahh, umempa moyo halafu mwishoni umemvisha ndoana awe chambo! Wewe #Mbayaaaaa .....

.....she's happier where she is, ndio maana haonyeshi kujali wa kuumia huko aliko, INSHORT,....ame #MoveOn with her life. Umezisoma alama za nyakati na kuzitafsiri vyema ila #Akili yako inabishana na #Roho yako si ndio?

Mleta mada wewe wajipa moyo tu, mara hivi mara namjua sana inside out aka hachomoi,..... #Mwanamke sio kitabu useme umemsoma na kumuelewa 99%.... NEVER!

Unalolitafuta wewe utalipata tu, ila usijesema #JF haikukuambia jinsi ulivyo na delusions mbaya kabisa.

....goodluck!

Samahani kama ntakuwa narudia ya wengine. Kaka swallow your pride. Kama mmekaa miaka miwili halafu mahaba yakaanza kudorora haikuwa dalili kwamba hakupendi. Hakuna mahali mahaba yanayodumu daima. Baada ya miaka miwili ndo mlikuwa mnaingia sasa kwenye uhalisia. Wengine yanadumu miezi, wengine wiki. Ukiona yaliyodumu miaka 5, 10....ujue kuna jitihada za makusudi za kuyapalilia. Ulitakiwa kuwa na subira na kama kweli ulikuwa unampenda sana sana ungekuja huku kuuliza jamani mahaba yamefifia, nipalilieje? Hapa nikikwambia utaje madhaifu yake matano uliyoyaona na kuyavumilia hiyo miaka miwili utaweza? Kwa mahaba mliyokuwa nayo sijui kama uliyaona.

Sasa mpenzi wako huyo kuondoka bila kulalamika wala kukonda haimaanishi kuwa hajaathirika. Kila mtu ana jinsi yake ya kukabiliana na changamoto. Huenda pamoja na kukupenda ameshukuru umemuacha mapema badala ya kuendelea kumpotezea muda. Ulitaka akulilie kama yule wa mwanzo ndo usikie raha ee? Kama unamkubali jishushe, omba radhi, toa sababu ni kwa nini unaona ni vyema mkarudiana na nini utafanya kumhakikishia usalama akirudi. Kujishusha na kuomba radhi ni "tabia ya kike" kwa mujibu wa wanaume ila unaweza kugusa moyo wa mwanamke kwa kumuonyesha "tabia za kike". Ukikosa omba msamaha, mpe attention,,,,Kwa ufupi poteza kidogo upate kikubwa. Usiogope kwamba anaweza kukataa. Akikataa basi, kwenye biashara kuna kupata na kupoteza. Bora ujaribu ushindwe.

Cc; BAK, King'asti



#MosKwito !
 
Last edited by a moderator:
kweli utoto tabu... inaonekana wote mpo mid 20's......mkishakuwa wakubwa mtaacha...
 
Ulichokosea kumuacha mpenz wako uliyeweka nae malengo cha muhimi mrudie wa mwanzo umuombe radhi am sure atakufahamu lkn kwa hy atakuzingua
 
Huyo bado muda wa kula maisha anao hana cha kujutia. We tafuta wa mid 30 kisha uone mtiti wake.
 
Kula ngumu mtoto wa kiume. Huo moyo utoke umfuate. Time is the best healer.
 
Kawaida, after two weeks utazoea. Wanawake wengi sana kuliko wanaume
 
Hilo ndio tatizo katika maisha"do'nt make a permanent decision for temporary feeling "ulichukuwa uamuzi mkubwa sana kwa mda mfupi bila kufikiri ulisukumwa na hisia,minakushauri katika love affairs kwa mwanaume hutakiwi kujutia uamuzi wako,thinks as a man" in life a man doesn't make a right decision but make decisions to be right"endelea kusimamia msimamo wako amin upo sahihi,coz kama huyo Dada alikuwa anakupenda baada ya kumuacha ungeona affection kwake,lazima angejitahidi kutafuta namna ya kutatua hilo tatizo kwa namna yoyote ile,kama hakuonyesha jitihada zozote zile absolutely hakupendi,halafu mwanamke kukaa na wwe mda mrefu kama 2 years,haimanishi kama alikuwa anakupenda kweli pengine labda alikuwa hana options,kuwa makini woman is unpredictable, wanatongozwa kila siku,you never know pengine labda ameshapata MTU mwingine na alikuwa anatafuta njia ya kuachana na wwe,think big!
 
Kumpenda Sana mtu unaweza kuwa kichaa na akijua unampenda Sana waliowengi atakutesa.Kama unaweza kaza moyo tafuta mwingine
 
Habarini wakuu,

Sijui naanzaje kueleza maana nshachanganyikiwa anyway let me try.

Ni hivi, kuna mwanamke mmoja nina mahusiano nae takribani miaka miwili
na nusu sasa. Sio siri/utani huyu mwanamke nimetokea kumpenda sanaa
haijawahi tokea tena maishani mwangu yote kutokana na mambo aliokua
akinifanyia.

Imefikia kiwango cha kuachana na mchumba wangu niliekuwa na malengo nae
hapo awali instead nika fall kwa huyu mwanadada mwingine. Katika kipindi
chote cha kuwa na mahusiano nae tumekua na ukaribu sanaa kiasi cha
kusema tunaishi kama mke na mume.

Miezi 9 nyuma nili note kwamba uhusiano wetu unaenda ukififia, mazoea
yame pungua. We don't hang out or talk often, hanichangamkii tena kama
zamani and stuff like that nikahisi labda ana mtu mwingine au
nimemuonyesha sanaaa hisia zangu kwake kiasi cha yeye kutumia hiyo kama
silaha kuniumiza kichwa coz nahisi ameshajua nshazimika kwake mazima.

Sasa kukata mzizi wa fitina nikaamua kuachana nae na kumwambia kila mtu
ale na time zake kwani mimi nilishakua na mtu hapo awali, istoshe nina
yangu mengi ya kufanya. Issue inakuja yeye akakubali tuachane na wala
haionyeshi kumkwaza wala kuumia kwamba nimeachana nae.

Siwezi sema ana mtu mwingine coz nimeshamchunguza sanaa na inaonyesha
hana mwanaume mwingine, ni binti aliye in her mid 20's. Asa huku upande
wangu nakua kama sitaki nataka.

Nikimuangalia mwenzangu naona anazidi kunawiri tu na mi huku nakonda kwa
mawazo na kumiss penzi lake. Asa wakuu hebu mnishauri mwanamke wa namna
hii namfanyaje ili na yeye aumie roho na kutamani kurudiana na mimi.

Kumuacha nimemuacha mwenyewe ila ni vile kama naona naumia mimi zaidi
yeye walaa. Mwisho wa siku inakua kama mimi ndio najipendekeza kwake
turudiane.

Mi nafkiri nimeeleweka, ( i'm confused ) sijawahi kuburuzwa na mwanamke
kiasi hichi.

kwi kwi kwiii sina mbavu.
1: naona anazidi kunawili
2: sijawahi kuburuzwa na m/ke dah umeniuwa leo pole kwa kuburuzwa
 
Niletee kuku wa njano na mayai viza manne....alafu uniambie unataka tumfanye nini.....???
 
Huyo hakupendi na ilikuwa ni relief kwake ulimwabia muachane! Mwanamke anayekupenda ukimwambia habari ya kuachana huwa anaumia sana.
Put that in your mind, she doesn't love me! Get distracted, avoid her. Yaani futa kila kumbukumbu yake Facebook, instagram, phone contact fanya kumsahau
 
Inawekana kakurushia jini

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom