Yaani ulimchukua akiwa hajaanza hata darasa la awali, haukumtendea haki. Manake ni wazi hata utoto wake hajaupitia, probably, ndio yupo kwenye childhood kwa sasa.. ......... kwani nilimtoa akiwa Hana hata darasa moja ila sasa nimhitimu wa chuo kikuu.,........
nduguzanzgu mm nimgeni humu ila sina kamba mguuni , nilikuwa naomba munisaidie jinsi yakuanduka post ili waione watu wote , mana naona chenga tu
Sasa ndugu hamkuzungumza chochote tangu jana,leo umemwachia nyumba kama jirani au nani na kwa makubaliano gani?Hujui na hatujui kwanini karudi je akiamua kuchoma nyumba au akifungasha kilakilichopo?Je hata kwa taratibu za kwenu mwezio alieondoka akirudi hivyo hakuna protocol za kufuata?Au mmekutana baa mkaachania baa vilevile?Hii issue si ndogo usiibebe mwenyewe:Option ya kumuua sio kabisa haitakusaidia chochote zaidi ya kufungwa maisha au kuuwawa muwatese watoto (kama mnao)Vunjeni ukimya akueleze kafuata nini?Vinginevyo asije kukuangamiza.Kupima afya kwanza in case of any reconciliation.
Nimewaambia wazazi wangu na wake wakasema nisimsemeshe nimwache jumapili watakuja na kwa Leo wanatuma mtu aende pale nyumbani wakati mi nikiwa huku kazini akazungumze nae, mi nmechoka jamani cjui kipi kitafuata
Ni sawa ila kwa kipindi hiki ni bora akakae kwa wazazi wake mpaka hiyo Jumapili.Kwanza ni hatari kuendelea kukaa nyumba moja kabla ya utatuzi wa jambo hili,Mkijibizana kidogo hasira uliyo nayo inaweza kukupeleka usikotarajia.Kama wazazi wanakaa mbali wasiliana nao akae hata kwa ndugu wa upande wake alie karibu;Ni kipindi kigumu jitahidi sana kucontrol temper na usinywe pombe nyingi kama ni mnywaji.Mlikuwa na ndoa inayotambulika? Huyo anaekwenda kuzungumza nae aondoke nae.Tumia huu muda mpaka Jpili kutafakari moyo wako unataka nini.Mwisho wa siku mwamuzi ni wewe ingawa kila mtu anaweza kukupa mawazo tofauti utakepima ni wewe kuona muamue nini kama hatima ya ndoa yenu.Pengine kadanganywa akifikiri kwa graduate mwezie maisha yangekuwa bora kumbe sivyo but ni LAZIMA awe muwazi kwako ni wapi alikuwa na kwa nini afanye hivyo.Vitu alivyofungasha karudi navyo?Kuna type ya wanawake huwa wanakusanya na kutoroka na vyombo vya nyumbani kila wakati na kurudi kuomba msamaha maisha yakishakuwa magumu.asikupitishe njia hiyo-hutapiga hatua!Pole sana
Amekurudia kasahau kukumaliza wewe,kuwa makini.Karudi peke yake sijui kasahau nini na mpaka sasa simuelewi maana kakaa kimya namwangalia Kwa uoga hapa
Mh, sijui yani kila movement nafuatilia what will happen next.nani aanze kulala au niripoti police au nimburuze nimtoe nje. Mbona mpaka sasa hajasema chochote nimfanyeje huyu.mbona simuelewi
Ukisikia ukubwa ndo huo! Kuna wakati mtu mzima unakosa majibu kwa hili huliwezi peke yako, kama alipotoweka hakwenda kwa wazazi au ndugu zake basi huyo hana sifa ya kuwa mwanamke!
watu wengine bhana mnatoa summary ya mnayokumbana nayo as if humu tunajua kilichokuwa kinaendelea.
Kimya ni jibu tosha kabisa mtizame tu ila usiache kumsalimia
Yaani ulimchukua akiwa hajaanza hata darasa la awali, haukumtendea haki. Manake ni wazi hata utoto wake hajaupitia, probably, ndio yupo kwenye childhood kwa sasa.