American Election 2016: Kicks off in Lowa

American Election 2016: Kicks off in Lowa

Acha uzushi wako.

Weka hapa chanzo cha yeye kutaka hivyo.
Ha ha haaa! NN matumbo yanaanza kukucheza nini? Hapana natania tu kiongozi wangu, ila jamaa lenu lina maneno ya kibaguzi sana!!
 
Ha ha haaa! NN matumbo yanaanza kukucheza nini? Hapana natania tu kiongozi wangu, ila jamaa lenu lina maneno ya kibaguzi sana!!

Matumbo kunicheza ni maruerue yako tu maana sidhani kama unajua unachokiongelea kunizidi mimi.
 
Uchaguzi huu umekuwa moto moto na gumzo kwani pamoja na kufanyika Marekani moto wake umevuka mipaka na bahari na kutua katika mabara mbalimbali ulimwenguni likiwemo Bara la Afrika, wadadisi wa mambo ya kisiasa wanasema turufu kubwa "miongoni" katika uchaguzi huo ni Bara la Afrika, ungana nasi hapa kukupa habari mbalimbali zinazojiri katika uchaguzi huo.

Kuwa wa kwanza
Afrika kuwa turufu kwa namna gani? Mbona siwasikii hao wagombea wakisema lolote kuhusu Afrika?
 
Hahahahah haya mkuu.... I stand for Trump and you?
Leo Super Tuesday. Leo kuna watu kubwaga Manyanga. Natamani Rubio na Trump wabaki kwenye Nomination wawili.Tishio la Hillary ni Rubio ninavyoona .Trump ni mwepesi tu
 
Uchaguzi wa Marekani kwa namna yoyote ni lazima ufuatiliwe sana sio tu na watanzania bali sehemu zote za dunia, kwa sababu by the way USA ndio monitor wa dunia,

Ila ukweli ni kwamba yeyoye atakayeshinda hatakuwa na manufaa yoyote kwa Africa sababu Ajenda ya US ni moja na itatekelezwa na yeyote atakayeingia.
 
Leo Super Tuesday. Leo kuna watu kubwaga Manyanga. Natamani Rubio na Trump wabaki kwenye Nomination wawili.Tishio la Hillary ni Rubio ninavyoona .Trump ni mwepesi tu
Yeah ni kweli mkuu...
 
Hillary Rodham Clinton, Democratic Presidential nominee by the end of today, EST.( I'm 100% biased)
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Leo Super Tuesday. Leo kuna watu kubwaga Manyanga. Natamani Rubio na Trump wabaki kwenye Nomination wawili.Tishio la Hillary ni Rubio ninavyoona .Trump ni mwepesi tu
Rubio is in deep trouble dude!. Hajashinda State yoyote toka Primary ianze. Nadhani bado yupo kwenye hiki kinyang'anyiro kwa vile ndio chaguo la GOP Establishment!.
 
  • Thanks
Reactions: kui
Rubio is in deep trouble dude!. Hajashinda State yoyote toka Primary ianze. Nadhani bado yupo kwenye hiki kinyang'anyiro kwa vile ndio chaguo la GOP establishment!.

GOP wanataka kupoteza fursa ya ushindi....
 
Kwa mara ya kwanza nimeanza kufuatilia uchaguzi wa Marekani kutokana na huyu jamaa Donald Trump na timu yake mfano yule msemaji mkuu wa Trump mama Katrina Pierson.

Jamaa Donald Trump nilidhani mwanzoni anafanya utani lakini naona sana anaanza kuwakosesha usingizi mahafidhina (wenye chama) wa GOP a.k.a Republican party.

Ni burudani tosha kuangalia TV katika kinyanganyiro cha kutia-nia kuchaguliwa kuwa mgombea Rasmi wa Urais mwaka huu USA kupitia vyama hivi viwili Republican/ Democratic .
 
Kwa mara ya kwanza nimeanza kufuatilia uchaguzi wa Marekani kutokana na huyu jamaa Donald Trump na timu yake mfano yule msemaji kuu wa Trump mama Katrina Pierson.

Jamaa Donald Trump nilidhani mwanzoni anafanya utani lakini naona sana anaanza kuwakosesha usingizi mahafidhina (wenye chama) wa GOP a.k.a Republican party.

Ni burudani tosha kuangalia TV katika kinyanganyiro cha kutia-nia kuchaguliwa kuwa mgombea Rasmi wa Urais mwaka huu USA kupitia vyama hivi viwili Republican/ Democratic .

Hahahaaaa mimi bado siamini kama Trump yuko serious.

Mtu gani aliye serious anatoa kauli kama anazotoa yeye?
 
Hahahaaaa mimi bado siamini kama Trump yuko serious.

Mtu gani aliye serious anatoa kauli kama anazotoa yeye?

Jamaa Donald Trump tayari ana ''mapozi'' a.k.a - ana ''act'' jukwaani kama vile tayari ni POUSA (President of United States of America).

Ngoja niangalie leo Super Tuesday Showdown italeta mizuka gani !
 
Hahahaaaa mimi bado siamini kama Trump yuko serious.

Mtu gani aliye serious anatoa kauli kama anazotoa yeye?
Kuna wale die hard GOP Establishment wanadai Trump ni decoy wa Hillary Clinton!. Ila Rubio nae ameingia kwenye mtego wa Trump, anatukana tu nae siku hizi!.
 
Kuna wale die hard GOP Establishment wanadai Trump ni decoy wa Hillary Clinton!. Ila Rubio nae ameingia kwenye mtego wa Trump, anatukana tu nae siku hizi!.

Mimi siyo muumini wa conspiracy theory lakini naelewa kwa nini baadhi ya watu wanadhania hivyo.

Trump alikuwa buddy-buddies na hao kina Clinton. Keshawahi kuwachangia hata pesa kwenye ile foundation yao.

Pia, nadhani walishaenda kwenye harusi ya Trump na huyu mke aliyenaye sasa.

Sasa, hayo yote ukijumlisha na mambo ambayo Trump keshayafanya na kusema, mtu akifikia hilo hitimisho mimi sitamshangaa kabisa.

Wewe umeona wapi mtu anayetaka kuwa rais wa taifa kama Marekani anamkejeli mtu asiyejiweza, anatoa kauli za kugawanya watu, anatumia lugha mbaya dhidi ya wanawake, anashindwa kumkana David Duke na kujifanya eti IFB yake ilikuwa na matatizo!

Tabia na mienendo yake si ya ki-presidential kabisa.

Hivi kweli kwenye general election anaweza kushindana na Hillary huyu?

Na kusema ukweli Hillary yuko vulnerable sana. Huu ni mwaka wa Republicans baada ya Democrats kuwa White House kwa miaka 8.

Lakini kama Trump akiishia kupata nomination [mimi bado sidhani kama atapata] basi Hillary atapeta kiurahisi sana.

She will mop the floor with him.

CNN na ORC leo wametoa kura za maoni na Cruz na Rubio wanambwaga Hillary lakini Hillary anambwaga Trump.

GOP wakimpa Trump awapeperushie bendera yao kwenye uchaguzi mkuu nitawadharau kabisa.

But, having said all that, hawa Wamarekani saa ingine huwa hawatabiriki. Kimzaha mzaha hivi hivi tunaweza kushuhudia hiyo Novemba 8 Donald Trump akishinda uchaguzi.

Hahahaaaaa....ila siamini kinachotokea aisee. Bado kabisa nasita kuamini kama Trump yuko serious na candidacy yake.

And the thing is....Trump hatashinda majimbo yote ya leo na baada ya leo GOP establishment itabidi wabonyeze panic button na kujipanga kuhakikisha jamaa hashindi.

Mwanzoni nilikuwa neutral lakini sasa nasema hapana....I am officially in the ABT train...Anybody But Trump.
 
Back
Top Bottom