Ameokoa Injini ya gari yangu

decomm

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
726
660
Habari wadau?

Kwa jinsi nilivyo changanyikiwa wakati huo, sikuchukuwa namba yake ya simu wala kumuuliza jina lake.

Nimeona hii ni sehemu pekee ambayo ninaweza kutoa shukrani zangu kwake kwa namna alivyonisaidia.

Gari nyingine mbili zilinipita kwa kasi na kupiga honi tu, nilikuwa natembea wastani wa 100kph. Lakini ninaye mkusudia, alinipita na kuanza kunisimamisha.

Nilikuwa natokea nyanda za juu kusini kuja Dar, baada ya kupiga "rasta" za kutosha mikumi kumbe koki ya sampo ya oil ikazidi kujifungua, niliifanyia sevisi gari kabla sijaanza safari, nahisi ile koki haikufungwa vizuri.

Tukio lilitokea baada ya kupita Doma kabla ya kufika Melela. Nilihisi kitu kama jiwe kimepiga chini ya bodi ya gari, nikapunguza mwendo ili nitafute sehemu nzuri ya kuegesha na kufanya ukaguzi.

Kabla sijapata sehemu ya kuegesha ndipo zile gari mbili harrier na prado nafikiri walinipita na kunipigia honi kali, gari ya tatu ndiyo iliyonipita na kusimama na dereva kufanya juhudi ya kunisimamisha. Kama sijakosea alikuwa na Toyota Opa.

Baada ya kusimama nikashuka kwenye gari naye akashuka na kuniambia kuwa oil inamwagika, nilipokagua nikaona kuwa koki ya sampo haipo na oil ilikuwa inaendelea kumwagika, nikawahi kuzima injini.

Kwakuwa sehemu tuliyosimama haikuwa salama, aliamua kunivuta hadi kijiji cha jirani, kokolo kama.sikosei (kijiji kimoja kabla ya Melela ukitokea Doma kuelekea Morogoro)

Hapo aliniacha nikiwa salama na taratibu za kurekebisha zilianza.

Kwa kuwa sikuchukuwa jina lake wala namba ya simu, nimeona nishukuru hapa huenda akapita na kusoma huu uzi.

1. Injini haikupata hitilafu, niliwahi kuzima kabla oil haijaisha.

2. Kwakuwa ilikuwa inakaribia saa mbili usiku, niliamua kulala papohapo ili asubuhi niweze kushughulikia vizuri.

3. Baada ya kupata koki nyingine Morogoro na kuweka oil, niliiwasha injini na kuwaka maramoja, niliisikiliza kwa muda kidogo kujiridhisha hatimaye nilianza safari ya kuja Dar na nilifika salama.

4. Namshukuru sana huyo mdau, yote aliyonifanyia hakuhitaji malipo. Mbora wa walipaji ni Mwenyezi Mungu, namuombea na naamini Mungu atampa malipo yaliyo bora kabisa.

5. Pia nawashukuru abiria wangu wawili niliokuwa nao waliokuwa wakienda Morogoro, walipata usafiri mwingine na kuendelea na safiri usiku huohuo.

Sina la ziada zaidi ya shukrani, na hivi ndivyo binadamu tunatakiwa kusaidiana.

Ahsante sana mdau.
 
Pole sana, na hongera kwa kufika salama, ila nakushauri nawe lipa fadhila kwa kusaidia wengine wenye matatizo
Nashukuru mkuu, mie ni kawaida yangu kusaudia wengine barabarani na sehemu nyingine, huenda nami nimelipwa kiaina.
 
Back
Top Bottom