Ameokoa Injini ya gari yangu

Ameokoa Injini ya gari yangu

Hee, Mkuu, ila na wewe una moyo mgumu sana. Mtu amesimama, akakuambia tatizo, mkajadiliana, aka-ofa kukuvuta, akakuvuta, akakuaga, hata jina hukukumbuka kumuuliza na mlikuwa naye muda wote huo? Naanza kuhisi una kau-bosi bosi fulani ambako kanakufanya usiwe na silka ya kuwa mwepesi wa kushukuru. Ni kama vile umezoea kufanyiwa vitu na watu unaowalipa ambao unaona huna haja ya kuwashukuru na ukajikuta na kwa huyu bwana umejisahau.
Mkuu, jinsi nilivyo "hata mkononi sijai"

Nilimshukuru sana, lakini ajabu hatukuulizana majina wala nini, wazo lilinijia dakika moja baada ya yeye kuondoka, 'nilipigwa' na ganzi fulani hivi labda injini ndio basi tena!

Nikaazimia kuweka shukrani zangu JF, huenda akapitia uzi na kuni PM kwa kufahamiana zaidi.
 
Mhusika halisi akijitokeza, kuna vitu maalum / mambo maalum atavitaja ili kuthibitisha kuwa ni yeye.

Kweli kabisa. Akijitokeza mwambie akuandikie private message humu JF ambako mnaweza kupeana namba za simu. Pole sana na tatizo.
 
Duuh, Kweli Binadamu Wapo Na Wanyama Wapo Pia, Najiuliza Hivi Ww Ungeweza Kufanya Hivyo?
 
Umefanya jambo jema kushukuru. Na huyo mtu naye alifanya jambo jema kukusaidia. Mara zote tunapofanya tendo jema kwa mtu mwingine tunakuwa tumefanya ibada machoni pa Mungu. Mungu hufurahishwa sana na matendo ya upendo kama haya.
kumbe sometimes una akili,kujifanya chizi tu,muone kwanza,sura nzurii,ka jini.
 
Habari wadau?

Kwa jinsi nilivyo changanyikiwa wakati huo, sikuchukuwa namba yake ya simu wala kumuuliza jina lake.

Nimeona hii ni sehemu pekee ambayo ninaweza kutoa shukrani zangu kwake kwa namna alivyonisaidia.

Gari nyingine mbili zilinipita kwa kasi na kupiga honi tu, nilikuwa natembea wastani wa 100kph. Lakini ninaye mkusudia, alinipita na kuanza kunisimamisha.

Nilikuwa natokea nyanda za juu kusini kuja Dar, baada ya kupiga "rasta" za kutosha mikumi kumbe koki ya sampo ya oil ikazidi kujifungua, niliifanyia sevisi gari kabla sijaanza safari, nahisi ile koki haikufungwa vizuri.

Tukio lilitokea baada ya kupita Doma kabla ya kufika Melela. Nilihisi kitu kama jiwe kimepiga chini ya bodi ya gari, nikapunguza mwendo ili nitafute sehemu nzuri ya kuegesha na kufanya ukaguzi.

Kabla sijapata sehemu ya kuegesha ndipo zile gari mbili harrier na prado nafikiri walinipita na kunipigia honi kali, gari ya tatu ndiyo iliyonipita na kusimama na dereva kufanya juhudi ya kunisimamisha. Kama sijakosea alikuwa na Toyota Opa.

Baada ya kusimama nikashuka kwenye gari naye akashuka na kuniambia kuwa oil inamwagika, nilipokagua nikaona kuwa koki ya sampo haipo na oil ilikuwa inaendelea kumwagika, nikawahi kuzima injini.

Kwakuwa sehemu tuliyosimama haikuwa salama, aliamua kunivuta hadi kijiji cha jirani, kokolo kama.sikosei (kijiji kimoja kabla ya Melela ukitokea Doma kuelekea Morogoro)

Hapo aliniacha nikiwa salama na taratibu za kurekebisha zilianza.

Kwa kuwa sikuchukuwa jina lake wala namba ya simu, nimeona nishukuru hapa huenda akapita na kusoma huu uzi.

1. Injini haikupata hitilafu, niliwahi kuzima kabla oil haijaisha.

2. Kwakuwa ilikuwa inakaribia saa mbili usiku, niliamua kulala papohapo ili asubuhi niweze kushughulikia vizuri.

3. Baada ya kupata koki nyingine Morogoro na kuweka oil, niliiwasha injini na kuwaka maramoja, niliisikiliza kwa muda kidogo kujiridhisha hatimaye nilianza safari ya kuja Dar na nilifika salama.

4. Namshukuru sana huyo mdau, yote aliyonifanyia hakuhitaji malipo. Mbora wa walipaji ni Mwenyezi Mungu, namuombea na naamini Mungu atampa malipo yaliyo bora kabisa.

5. Pia nawashukuru abiria wangu wawili niliokuwa nao waliokuwa wakienda Morogoro, walipata usafiri mwingine na kuendelea na safiri usiku huohuo.

Sina la ziada zaidi ya shukrani, na hivi ndivyo binadamu tunatakiwa kusaidiana.

Ahsante sana mdau.

Aisee kumbe bdo unakumbuka!!! Ni mimi hapa fanya kuni pm!!
 
Pole sana, na hongera kwa kufika salama, ila nakushauri nawe lipa fadhila kwa kusaidia wengine wenye matatizo
Kweli kabisa. Ikiwa na wewe utamtendea wema mwingine yo yote katika tatizo linalomkabili utakuwa umemshukuru huyo aliyekuepusha matatizo na hivyo ndivyo nchi itakuwa inaboreka.
 
Pole kwako mkuu na hongera kwa huyo msamaria mwema.......
 
Duuh, Kweli Binadamu Wapo Na Wanyama Wapo Pia, Najiuliza Hivi Ww Ungeweza Kufanya Hivyo?
Nimeshaokoa maisha kadhaa ya watu.

Barabarani, nimeokoa Lori la mafuta (pulling) lilikuwa limeanza kuwaka moto kwenye mataili maeneo ya Ihemi, pia nimeshawahi kuokoa lori la mizigo kuwaka moto miezi kadhaa iliyopita...

Lengo halikuwa kutaja niliyowahi kuyafanya, lengo ni kumshukuru Jamaa na akipenda atani PM kwa kufahamiana zaidi.
 
Nimejifunza jambo hapa. Pamoja na kumshukuru huyo ndugu aliyemsaidia mleta mada, ni vema wenye vyombo vya moto msifanye service na kuanza safari ndefu immediately after. Ni vema uwe na muda wa kutosha kama siku mbili ama tatu baada ya service, kisha uanze safari yako. Hii itakusaidia kuyabaini makosa kama hayo. Pia endapo magurudumu yako yamefunguliwa kwa kubadilisha ama kuziba pancha, jitahidi wewe mwenyewe kuhakiki kama yamekazwa sawasawa, vinginevyo utashangaa tairi lako limetangulia mbele nawe ukabaki nyuma.
Kabisa mkuu hata mimi niliwahi pata mkasa kama huo oil filter ilikuwa haikufungwa vizuri toka Tanga mpaka segera ilianza kumwaga oil na ilikuwa naenda dar kilochoniokoa nilisimama kula kurudi naona chini pamelowa.
 
Jambo jema sana.. Mungu ndo atakaemlipa kwa wema aliokutendea nadhan na ww umepata somo hapo..
 
Siku nyingine ukumbukage kuchukua namba za simu za watu muhimu kama hao.Ndivyo familia hujengwa namna hiyo.Undugu wa kizazi hiki ni zaidi ya ndugu wa damu,kabila na ukoo wako.
 
Kwanza nampongeza Sana huyo jamaa, Mungu atamjalia. Nirudi kwako, huo ni ujumbe Kama ulikua na tabia ya Kusema "aaaa, shauri yake bwana " kwamba uwe muungwana, you never know nani atakusaidia.
 
Back
Top Bottom