habari in short...
kuna binti nilimuona siku fulani nilipokuwa nimeenda kusali....basi kabla kuingia kweny ibada tulibadilishana Namba kwa ajili ya kuwasiliana... basi siku moja nimempigia simu...ile mwishoni naaganaa nae kwenye simu AKANAMBIA ...nikwambie kitu....,,,, hapo kidogo nilisita kumuitikia nilifikiri ni mzinga anatka kuniripua...basi nikamwambia Nambie tu....BASI MIMI MWENZIO NAKUPENDA....kiukweli sikuamini nilihisi ni utani si unajua tena Mwanamke kumtamkia Mwanaume kidogo haijazoeleka kidesturi...basi nikamwambia nitaprove siku nikikuona....
SASA NDUGU ZANGU....MNANISHAURI VIPI NIENDELEE NAE....KWASABABU AMENITAMKIA MWENYEWE AU...ITAKUWA NI MBINU TU ANA LENGO LAKE....????
...
Hongera kwa kupata rafiki mpya mkuu,
ushauri:
1:Wakati mwingne akipiga simu hata mara kumi usipokee, mtafute badae
Au akituma ujumbe usijibu jibu badae
2:Akikutembelea pika matembelee
3:Muombe game uone mwitikio wake
4:Akikuombe pesa msaidie lakini si kwa nia mbaya bali kama binadamu yeyote mwenye uhitaji
5:Siku nyingne mwambie kna ishu fulani ya pesa umekwama akikutumia kaa nazo siku mbili au tatu mrudishie pesa zake kwa njia ambayo hatagundua kuw unamrudishia ela zake
visa hivo vitakusaidia kumfahamu
1:kupima uvumilivu wake anapokutana na changamoto pia kupima upendo wake kama ni og au upendo wa vifurushi
2:Kupima msimamo wake kwenye mapenzi na jinsi gani anajiheshimu
lakini kama ataitikia fasta kukupa mchezo basi huyo lengo lake ni tamaa ya kimwili tu na sio kujenga familia
3:Itakusaidia kumpima kama kweli yuko tayari kukusaidia unapopata matatizo,pia itadhihirisha jinsi gani amejitoa kwako
Angalizo:Usimfanyie visa kwa kumnyanyasa kisa amekupenda bali lengo ni kutaka kufahamu yukoje
mwisho:Muombe sana Mungu wako akupe mke mwema.
Sent using
Jamii Forums mobile app